Kuchunguza simu ya mpenzi wangu mwisho ilikuwa 2017, siwezi na sirudii

Kuchunguza simu ya mpenzi wangu mwisho ilikuwa 2017, siwezi na sirudii

kidawisee

Senior Member
Joined
Feb 27, 2020
Posts
143
Reaction score
212
Nakumbuka nilikuwa sina sana iyo tabia kiivo na ilipelekea kila mmoja wetu kutokuwa na password katika Simu.

Iyo siku shetani alipitia na ndio uhusiano wangu ulivunjika ambao nliuamini ntazeeka nao, Tulitoka kuzika sasa si unajua ukifiwa pole nyingi na unakuwa bize kuzijibu, Tukafika home shemeji yenu njia nzima alikuwa bize na simu, tulivofika home akawa ameiacha juu ya friji akaingia kuoga, kashetani kakanipitia nkachukua, weee nliyoyakuta ndio nliyokuwa nayatafuta,

Mademu kama wa4 wote wanasema polee mme wangu, kuna demu mpya ndio anatongozwa. Kiukweli nlitaka kuzuga ila alikuta nmelala na simu, Shuka na pillow zimelowa machozi, Tukasuluhisha mpak kwa wakubwa zetu ila moyo ulishaingia mshtuko nlishindwa kukubali yaishe.

Nkamsamehe na nlikaa kwake week lengo lao tuyamalize niwe sawa, akanionea huruma maana kama nipo jela. Nalia mda mwingi kuliko kuongea nae, akanionea huruma akanirudisha kwetu nitulie hata week, Ndio nkawa nmemuacha kabsa na alipigania mno tuwe sawa nlishindwa.

Hii ilinifundisha mambo mengi, Kwanza ilinipotezea mme(kiukweli sijawahi kuhisi tupo wawili jamaa alisimama katika nafasi yake). Nlijifunza hakuna mwanaume mwenye mwanamke mmoja ila anapenda mwanamke mmoja tu,

Nkajifunza kuangalia jamaa anakuheshimu, kukujali, anasimama kwenye nafasi yake na una uhuru kwake. Nlijifunza kila mtu ashike simu yake kama unataka uhusiano Ufike utakapo na unapenda Amani . Wanawake wenzangu, Acheni kupekua simu za wanaume zenu, Malaya ni Malaya tu hata ukague vipi, Sanasana unampa kichwa kuwa huwa unafuma ana cheat ila unamsamehe.

Kwaiyo Hofu anaipunguza, hakikisha ukichunguza ukikuta majibu uwe na maamuzi magumu maana moyo bana ukiingia doa ni kasheshe.Mnaweza kupendana bila kushikiana simu japo kuna vitu hata ujapekua unaviona iyo ruksa nyumba kuwa Tarime.
 
Uandishi gani huu nimeshindwa kusoma
IMG_20210319_115219.jpg
 
Kama unajua uko na mke au mume, wakati unapokua na relation ya nje usiruhusu kujulikana.
Mawasiliano yasiwe ya wazi au ya wakati mwingi kuepusha mwanya wa kujulikana.
 
Ameongea points tupu. Mpaka yawakute makuu ndo mnajifunzaga simu ya mwenzako yanini kukagua, ili iweje. kama mnaishi kwa amani na mpenzi wako achana na mambo ya kukagua cm ila kama unamtafutia kisa ili muachane hapo sawa kagua simu yake mpaka upate sababu ya kuachania na LAZIMA UTAPATA TU KISA
 
Back
Top Bottom