Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,404
- 6,969
Wana JF, hii kasumba ya wanasiasa wa upinzani kuwa wanasubiri majanga au kadhia flani itokee alafu wao wanufaike kisiasa ni kukosa busara za kisiasa.
Sasa hivi kila mwanasiasa wa upinzani amekomaa kuikosoa serikali ya Ccm bila hata kuwa na hoja zenye mashiko.
Mfano Mkuu wa nchi anaesema tutumie mask ambazo tunao uhakika wa usalama wake kiafya, hii imekuwa kama hoja kwa upinzani na wafuasi wake. Je, hii itawabeba?
Achana na hilo, bado wapinzani walitaka kupata kick ya kisiasa kutaka kuaminisha umma na jumuia ya kimataifa kuwa serikali haijachukua hatua madhubuti kupambana na jaga la covid 19. Jambo ambalo kiuhalisia sio kweli. Mlitaka hatua zipi zichukuliwe ili muone serikali inapambana na janga hili? Maana zipo taratibu za kupambana na haya majanga na ni lazima kiwango cha hatari kijulikane.
My take; Tusidhanie kuwa Covid 19 itakuwa mtaji wa kisiasa. Kama Watanzania tuonyeshe umoja kupambana na hili janga.