#COVID19 Kudhania janga la Covid 19 litakuwa mtaji wa kisiasa ni kufilisika kisiasa

... Mfano Mkuu wa nchi anaesema tutumie mask ambazo tunao uhakika wa usalama wake kiafya, hii imekuwa kama hoja kwa upinzani na wafuasi wake. Je hii itawabeba?
Mkuu hebu twende taratibu, huenda kuna habari zimenipita jana na leo. Kuna kiongozi wa upinzani aliyetoa kauli ya kupingana na ya mkuu wa nchi kuhusu matumizi ya mask?
 
Kati ya yote uliyosema, hii changamoto ya kupumua ni ugonjwa mpya?? Najiuliza tu ni ugonjwa gani huu ambao watu wanasema tusikusanyike bila sababu, tuvae barakoa zetu na tujifukize! Ugonjwa ambao tunasema chanjo zake si salama na kushauriwa kutumia NIMCAF? Kuna asthma ambayo mtu hupatwa na changamoto ya kupumua pia. Nilidhani "changamoto ya kupumua" ni dalili ya ugonjwa - sasa naona inatumika kama jina la ugonjwa. Je ni ugonjwa gani huo?
 
Kwa hiyo unakubali kuwa hicho ndo kiliwafanya chadema na wenzake kuangukia pua uchaguzi ulioisha kwa upumbavu wao kudandia corona kwa lockdown na kukimbia bungeni?

Kwa hiyo bado hamjajifunza mnarudia makosa hayo?
 
Mkuu hebu twende taratibu, huenda kuna habari zimenipita jana na leo. Kuna kiongozi wa upinzani aliyetoa kauli ya kupingana na ya mkuu wa nchi kuhusu matumizi ya mask?
Unajua kusoma mkuu?
 
Mleta mada una PhD ya upumbavu.

Izo masks huyu mjinga mwenzio anazo sema zina corona kwani ndo mara ya Kwanzaa kuingia Tz. Tengenezeni za kwenu kama mmnauwezo huo.
 
Chukua ufuto ufute urekebishe nilipokosea. Ujumbe umeupata.
 
Mleta mada una PhD ya upumbavu,
Izo masks huyu mjinga mwenzio anazo sema zina corona kwani ndo mara ya Kwanzaa kuingia Tz. Tengenezeni za kwenu kama mmnauwezo huo
Mask kibao zinatengenezwa Tanzania bibie. Au ulitaka utengenezewe bikini ndio ulidhike?
 
Una muda wa kupima Barakoa lakini huna muda wa kupima corona?

Unahimiza watu wasivae Barakoa kwa kuzikosoa na kwamba wasaidizi wako wanaogopa kuvaa kwa sababu wewe bosi wao huvai. Unawasifu wasivaa na kuwananga wanaovaa, bado unajiona unapambana na corona?

Wapinzani hawapo tafuteni wa kusingizia.
 
Mtaji wa kisiasa ni akili yako na siyo kuficha taarifa za matatizo kwa sababu unaogopa kuwa umeshindwa,uwazi na ukweli ni mtaji wa mwanasiasa yeyote yule, Trump yuko wapi?
 
Mtaji wa kisiasa ni akili yako na siyo kuficha taarifa za matatizo kwa sababu unaogopa kuwa umeshindwa,uwazi na ukweli ni mtaji wa mwanasiasa yeyote yule,Trump yuko wapi?
Wewe hapo ulipo umefichwa taarifa gani?
 
Unazidi kufilisika kisiasa.
 
Wanasema uchaguzi mkuu utarudiwa mwaka huu[emoji3104][emoji3104][emoji3104][emoji3104]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…