#COVID19 Kudhibiti maambukizi ya COVID-19: Wasafiri kutoka Tanzania wapigwa marufuku kuingia Uingereza

#COVID19 Kudhibiti maambukizi ya COVID-19: Wasafiri kutoka Tanzania wapigwa marufuku kuingia Uingereza

Sasa mnamlaumu Jiwe kwa sababu ya South Africa covid variant? Ingekuwa Tanzania covid variant ningeelewa mantiki ya hiyo ban. Vinginevyo ni upuuzi na kuchanganyikiwa kwa hao wazungu wa UK.

Ok tumepigwa ban kuingia UK....kwa nchi na mtu anayejielewa hiyo ban should not be our problem, it is UK problem. UK ni paradiso?
Watozuiwa kuingia Airports za UK ni wale wasio raia wa Uingereza na Ireland na wazururaji wengine.

Isipokuwa kwa mfano kama wewe ni mtanzania na una makazi ya kudumu huko UK basi wapita tu kwa kufuata taratibu zilizowekwa.

Nchi ambazo mpaka sasa zimezuiwa kuingiza ndege zake UK ni Namibia, Zimbabwe, Botswana, Eswatini (Lesotho), Zambia, Malawi, Lesotho, Mozambique, Angola, Seychelles na Mauritius.

Kenya haimo kwenye hio orodha hivyo abiria kutoka Kenya wakiwemo wazungu wa kikenya bado wataingia nchini humo wakiwa na majibu hasi ya COVID-19 lakini watalazimika kujitenga kwa siku 10.

Pia kuanzia leo huenda abiria wote wa Uingereza wakapigwa marufuku kuingia nchi za Jumuia ya Ulaya na pia abiria wanoingia Uingereza wakalazimishwa kujitenga katika mahoteli badala ya kwenda kukaa nyumbani kama ilivyokubaliwa awali.

Hivyo wanosema Tanzania itaathirika kwenye Utalii waangalie uzuri hiyo kauli kwani hata nchi ya Uingereza na zingine kwa sasa zinaendelea kuathirika kiuchumi na khasa kwenye sekta ya Utalii kwani watalii wengi hawatopata fursa ya kwenda nje ya UK.

Hivyo jamaa zetu wa Ufipa Street muangalie uzuri eneo mtakalo kuingia kucheza ngoma.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Mficha ugonjwa MABEBERU watamuumbua

"tumeishinda corona kwa maombi na kujifukiza,au nasema uongo ndugu zangu" 🤣

Huyu mtu ni disaster
Mitano tena
 
Hivi hata Kiswahili unakijua kweli wewe?

"Eti mfano wako halisi." Huo kaa nao!

Eti "unasaidia" - ufinyu mkubwa wa akili. Muendelezo ule ule wa kujifanya donor kantre huku maskini hohe hahe.

Elimu yako tafadhali.
Ilimu yangu ni madrasa
 
Ufipa inaingiaje kwa maamuzi ya Uingereza? Kama huna cha maana cha kuandika ficha ujinga wako.
 
We mleta uzi. Kwahiyo kwa uelewa wako
All arrivals from Tanzania Ina manisha Watanzania?
 
Naona uanze wewe kabwera, unayeishi kwa kusaidiwa kuwaza.
Angalia usije ukawa mmoja wa wajinga wa jiwe wanaopinga ugonjwa unaoua watu kila uchwao, tafadhali acha kupinga ukweli.
 
Lakini hii sirikali yetu inachekesha sana, ni kweli maambukizi ya korona sio makubwa nchini...kuna ubaya gani wa kutoa data za hao wagonjwa?!.

Nchi yetu sio kisiwa ina muingiliano na mataifa mengine yaliyoathirika sana na wala ugonjwa huu sio wa aibu haujaanzia kwetu...kuna tatizo gani kusema hali yetu nchini kuhusu korona ikoje.

Yaani li sirikali lipo kimya japo hata kuendelea kuhamasisha raia wake kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa ambao dhahiri bado ni tishio duniani

Tutatoaje data za wagonjwa wa mafua ? Covid ni mafua makali malaria inaua kuliko covid mbona huombi data zake
 
Na sisi kama tuna ubavu tupige marufuku raia wa Uingereza kuingia humu nchini wakati tunategemea watalii kupata fedha za kigeni.

Kuna nchi zingine zitaiga hatua hii ya UK na mwisho wa siku tutajikuta tumetengwa.

Jiwe kavurunda sana kwenye issue ya Covid.

Wewe ulitakaje mkuu .. ukae ndani usifanye kazi? Kampeni zimepita kina lissu walikuwa wanakusanya watu alipata hiyo corona ?!

Haya ni mafua makali na tuna njia zetu wenyewe za kudhibiti
 
Majirani zetu Kenya, Rwanda nao wamepigwa ban?
 
Tutatoaje data za wagonjwa wa mafua ? Covid ni mafua makali malaria inaua kuliko covid mbona huombi data zake
Malaria ina dawa zake covid19 haina dawa.
 
Lakini hii sirikali yetu inachekesha sana, ni kweli maambukizi ya korona sio makubwa nchini...kuna ubaya gani wa kutoa data za hao wagonjwa?!.

Nchi yetu sio kisiwa ina muingiliano na mataifa mengine yaliyoathirika sana na wala ugonjwa huu sio wa aibu haujaanzia kwetu...kuna tatizo gani kusema hali yetu nchini kuhusu korona ikoje.

Yaani li sirikali lipo kimya japo hata kuendelea kuhamasisha raia wake kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa ambao dhahiri bado ni tishio duniani
Hapo kwenu kuna mgonjwa yeyote? Kama hakuna hayo ni mafua ya kawaida piga kazi acha blah blah
 
Lakini hii sirikali yetu inachekesha sana, ni kweli maambukizi ya korona sio makubwa nchini...kuna ubaya gani wa kutoa data za hao wagonjwa?!.

Nchi yetu sio kisiwa ina muingiliano na mataifa mengine yaliyoathirika sana na wala ugonjwa huu sio wa aibu haujaanzia kwetu...kuna tatizo gani kusema hali yetu nchini kuhusu korona ikoje.

Yaani li sirikali lipo kimya japo hata kuendelea kuhamasisha raia wake kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa ambao dhahiri bado ni tishio duniani
Walishasema na kuutangazia ulimwengu kwamba corona imetoweka nchini, sasa wataanzaje tena kutoa data za maambukizi!?

Hata kama ungekua wewe...ungeanzaje kwa mfano!
 
Back
Top Bottom