#COVID19 Kudhibiti maambukizi ya COVID-19: Wasafiri kutoka Tanzania wapigwa marufuku kuingia Uingereza

#COVID19 Kudhibiti maambukizi ya COVID-19: Wasafiri kutoka Tanzania wapigwa marufuku kuingia Uingereza

Kuna chanjo inasambazwa kwenye nchi mbalimbali duniani Tanzania bado hatujaruhusu chanjo hiyo kuingia.
Tusubiri wapate chanjo itakayodhibiti aina mbalimbali, kama wao tu wamejichanja saizi wanasema corona nyingine inatoka A. Kusini, itabidi wajichanje tena, nyingine sijui Brazil itabidi wajichanje. Tusubiri tu
 
Kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake.

Lakini lazima ufikirie kwa kutumia "capacity and critical thinking" yaani waunganisha maneno kama" What and why".

Wewe wadhani hatua zote hizo wanazochukua UK ni kwasababu wana uwezo sana?

Ni kweli ni nchi ya tano duniani kwa uchumi mkubwa lakini inside wana shida kidogo kwenye uchumi.

Ni kwa sababu hawataki madhara zaidi kwenye healthcare system yao na pia hivi sasa wapo kwenye "vaccination programs" kwa raia wao ambao ni vulnerable zaidi.

Ila travel and tourism sector na biashara zingine lukuki zinazidi kudorora.
 
We need a unified world to tackle Corona. If necessary the world "superpowers" should get rid of stupid ones making a barrier to these efforts!
The super powers are dying like nsenene - grasshoppers due to Corona! How can they be champion in monitoring others!?
 
Na sisi kama tuna ubavu tupige marufuku raia wa Uingereza kuingia humu nchini wakati tunategemea watalii kupata fedha za kigeni.

Kuna nchi zingine zitaiga hatua hii ya UK na mwisho wa siku tutajikuta tumetengwa.

Jiwe kavurunda sana kwenye issue ya Covid.
wewe mzee upo???

kwani ndio wanaanza 2021 maana uliishatabiri kutengwa tokea mwaka jana mwezi may.
sasa sisi tuwatenge watu ambao hawana madhara nasisi!!!tokea 2019 mwezi may tuliacha milango wazi,hatujawahi kumfungia mtu kuingia.

huo ndio msimamo wetu.
ajabu wanatufungia tusiende halafu wao wataendelea kuja huku[emoji1787][emoji1787],nawewe huoni nani mzinguaji hapo.
 
WHO hawalali wanahangaika usiku na mchana kupata dawa hawajakaa wakitegemea maombi, sisi (Tz) wala hatujishughulishi hata kujaribu chanjo zilizopo tunasubiri rehema za Mungu.
Raisi ametoa Challenge kwa wataalam kwa kitanzania tutengeneze dawa zetu za kupambana na magonjwa kama huo.

Hiyo ndo tabia ya kutaka kufanikiwa yaani kutafuta suluhisho la matatizo kwenye mazingira uliyopo.
 
Sasa mnamlaumu Jiwe kwa sababu ya South Africa covid variant? Ingekuwa Tanzania covid variant ningeelewa mantiki ya hiyo ban. Vinginevyo ni upuuzi na kuchanganyikiwa kwa hao wazungu wa UK.

Ok tumepigwa ban kuingia UK....kwa nchi na mtu anayejielewa hiyo ban should not be our problem, it is UK problem. UK ni paradiso?
hapa kuna kundi la wale wagonjwa wa utawala ambao wameamua kuwa wafuasi wa UK aliyechanganyikiwa.
 
Hawa Mabeberu sijui wakoje, juzi tu tulikiwa na balozi wao pale kwenye uzinduzi wa mgodi mkubwa wa Nickel....mambo swafiii sasa leo eti hatufuati kanuni za ugonjwa wa COVID-19 laah

Kweli beberu ni beberu tu anakugeuka muda wowote, hawaaminiki hawa!!
 
Ni mawazo duni sana kuchanganya ugonjwa huu hatari na siasa.

Pili kwa kutokuwa na takwimu zozote rasmi kuhusiana na ugonjwa huu, ujasiri wa kujilinganisha na yeyote kiasi cha kuhitimisha kuwa na kila mtu ajipambanie kivyake tu, unatoka wapi?

Ni wazi kuwa tumekosa viongozi wa maana wa kutuongoza kupita salama kwenye gonjwa hili. Kwa bahati mbaya hali itaendelea kuwa hivi hadi pale gonjwa hili litakapopiga sawa sawa na hasa kama likipiga pale pale penyewe.

Au nasema uongo ndugu zangu?

litapiga wapi wewe

mwaka mmoja toka Covid 19 imetangazwa!unatamani balaa litokeee lakini haiwi,umebaki kusononeka tu.
 
Tusubiri wapate chanjo itakayodhibiti aina mbalimbali, kama wao tu wamejichanja saizi wanasema corona nyingine inatoka A. Kusini, itabidi wajichanje tena, nyingine sijui Brazil itabidi wajichanje. Tusubiri tu
Hahaa kwahiyo kazi yetu ni kusubiri wengine wagundue dawa, sisi tunafanya jitihada gani hata za kuzuia kusambaa kwa ugonjwa kwani hata barakoa tu rais haonyeshi mfano wa kuvaa au maombi yanatosha.
 
Nguvu inayotumika kujengea watu hofu kuhusu corona ni kubwa mno kuhusu ukweli wa corona yenyewe
bahati mbaya wamekutana na watu wanaofikiri kabla ya kufata mkumbo.

cha kushangaza utakuta kati ya walii 10 wanaoshuka viwanja vya ndege 5 wanatoka UK,jiulize wanakujaje nchi hatari kwa afya zao??

nakumbuka hata US kipindi inatangaza raia wake warejee ubarozi ili iwarudishe nyumbani,hakutokea hata mtu mmoja maana nyumbani hali ilikuwa inatisha.
 
Naona mnashabikia ujinga wa kutokuelewa kinachohabarishwa.

Hatua hiyo ya UK itawahusu raia wote khasa wale walogundulika wanapitia Tanzania lakini wanatokea Afrika Kusini.

Mbona hata UK nao wanaelekea kuzuiwa kuingia nchi za Jumuiya ya Ulaya?
Kwa hiyo lumumba mnataka kushindana na UK? Mnafikiri hao Ni ACT? Siyo kila Vita Ni ya kupigana, nyingine unaziepuka hata kwa kutumia style ya mbuni...unafukia kichwa mchangani kiwiliwili nje unajifanya hujui.

Wee hao watu wapo wanaangalia namna gani ya kuhamishia makazi yao mwezini wewe hata matundu ya choo mashulen bado halafu eti uvimbishane nao msuli!!!!
Ngoja kwanza wapige pin afta pin akili zitakaa sawa tu.
 
Wewe ulitakaje mkuu .. ukae ndani usifanye kazi? Kampeni zimepita kina lissu walikuwa wanakusanya watu alipata hiyo corona ?!

Haya ni mafua makali na tuna njia zetu wenyewe za kudhibiti
ukute yeye ndiye alikuwa akiitikia"waaambieeee,wapigeeeee[emoji23][emoji23][emoji23]"wakati lissu anaongea.

na tuko naye hapa hajui hata barakoa inauzwaje[emoji28][emoji28]
 
hilo ni jambo la mtu au ofisi na maamuzi yake.

ofisi nyingi kama bank na taasisi kuna sanityzer bado.
Kwenye utawala huu au ujao?!!

Utawala huu mtu Unaweza kufanya uamuzi wa kiofisi kesho yake ukafukuzwa kazi au ukaambiwa nyumba yako ipo kwenye hifadhi ya chemchem hivyo Ni ya kubomoa au hata ukashtakiwa kwa uhujumu uchumi.
 
Kuna chanjo inasambazwa kwenye nchi mbalimbali duniani Tanzania bado hatujaruhusu chanjo hiyo kuingia.
kama wamechanja raia wao,wakanini bado wanaogopa muingiliano!!!

unajua watz ebu tuwe tunatumia akili basi jamani.
 
Basi serikali itoe data kwa kusema watanzania wote tuna corona hivyo hakuna maambukizi mapya
[emoji23][emoji23][emoji23]huu ndio msimamo wa vichaa fulani,ila ikitangaza hivi huwezi amini watapinga na kugalagala chini[emoji1787].
 
Rasmi nasimama na rais wangu, mabeberu hawafai na wanatumia corona kutaka kututawala.. Rais endelea na msimamo nakuunga mkono na katika maeneo nitakayokuwa naelezea jinsi ambavyo mabeberu hawafai.
 
WHO hawalali wanahangaika usiku na mchana kupata dawa hawajakaa wakitegemea maombi, sisi (Tz) wala hatujishughulishi hata kujaribu chanjo zilizopo tunasubiri rehema za Mungu.
wao kama UK wanaamini chanjo yao,wajikite kuwapa raia wake,maisha ya wengine hayawahusu.
 
Sasa mnamlaumu Jiwe kwa sababu ya South Africa covid variant? Ingekuwa Tanzania covid variant ningeelewa mantiki ya hiyo ban. Vinginevyo ni upuuzi na kuchanganyikiwa kwa hao wazungu wa UK.

Ok tumepigwa ban kuingia UK....kwa nchi na mtu anayejielewa hiyo ban should not be our problem, it is UK problem. UK ni paradiso?
Kwa wafanyabiashara na wanaokwenda kusoma inakaaje mkuu.
 
Mimi nafikiri wamefanya vyema maana serikali pamoja na mambo yote haikupaswa kupuuzia swala la chanjo.... tulipaswa kuweka msimamo juu ya chanjo wala sio jambo baya.

kuchukua chanjo na kuwapa wananchi sio kosa kabisa wala haimaanishi ndio mna corona sana bali ni kinga kwakuwa tuna muingiliano mkubwa sana.

Mbona tuna chanjo nyingi zinatumika hapa nchini? chanjo kama ya surua , oma ya ini n.k. Nafikiri wamefanya vyema labda tunaweza jifunza katika hali ngumu.
 
Back
Top Bottom