Elections 2015 Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target, Adui Mkubwa sio CCM Bali ni ...

Attachments

  • 1426352957629.jpg
    54.5 KB · Views: 634
Last edited by a moderator:
Nimenote watu wamehamasika sana na taarifa za UKAWA/Chadema, nimeona niwakumbushe washishangilie hadi ku miss the target, CCM sio target, target watu!, changing the mindset za watu!.

Pasco
 

Bwana Zimmerman nimekuvulia kofia kwa maelezo yako mafupi yenye ukweli unaotosheleza kuliko kitabu cha kinafiki cha Pasco. Ni ukweli ulio wazi kuwa adui mkubwa wa watanzania ni ccm na mfumo wao.
 

Nimenote humu watu wakishangilia kila mwanachama mmoja au kiongozi wa CCM akicross kuja upinzani!, uchaguzi wa awamu hii, CCM sio determinant tena!, the determinant ni "we the people!". Nashauri at this point Chadema iache ku deal na kuishambulia tuu CCM, i deal na the ones who matter most, we the people, ituambie itatufanyia nini?!.

Ushindi kwa Chadema kupitia njia ya EL ni mpango wa Mungu, CCM doesn't matter much, but we the people ndio tunaomatter, bado ijaona juhudu za dhati ku deal na sisi tunaomatter much.

Ili kupiga chini CCM, mashambulizi lazima yaelekee kenye the right target to hit the bull!.

P.

Pasco
 
Nafanya rejea kwa bandiko langu hili la 20th August 2012, wanasema numbers don't lie!, tafiti za number zimeanza kutoka, Nimeipata hii kwa hisani ya Mkuu Ocampo four,

Kama utafiti huu ni kweli, numbers don't lie!, then safari imewadia!.
Jumamo
si njema.
Pasco
 

the numbers dont add up; umehusianisha vitu viwili tofauti; yaliyokwisha fanyika na projection
 
CCM Imetufanya sisi kama taifa kuonekana wajinga mbele ya uso wa dunia. Hivyo hatupaswi kurudia huu ujinga
 


Wananchi Wa Tanzania wametawaliwa na
1)ujinga
2)ushamba
3)ushabiki na kutojiamini
4)kuishi kwa mazoea kutokana na kutowekwa wazi kuhusu tuko katika capitalism au socialism
5)uswahili we angalia vizuri waswahili wengi sana wanapenda taarabu ndo maana ccm wanatumia taarabu kuwa konga nyoyo zao
6) ukosefu Wa elimu na hata waliosoma bado hawajaelimika wanakosa exposure
7)uvivu Wa kufikiria na uwoga uliopitiliza
8)unafiki na umbea Wa hali ya juu


Hizo ndo sababu Kuu za ccm kutawala hapa bongo hizo zikipanguliwa ccm haitakuwepo na hata upinzani ukishika taifa litaendelea otherwise tutapiga marktime sanaaa

My take:- mtoa mada piga ela kivyako achana na wajinga wakija kistuka too late
 
the numbers dont add up; umehusianisha vitu viwili tofauti; yaliyokwisha fanyika na projection
Mkuu Zekidon, moja ya majukumu muhimu ya jf ni kuelimisha, katika kuelimishana, utanisaidia sana na kuwasaidia wengine, kama utaonyesha hivyo vitu viwili tofauti kati ya yaliyokwisha fanyika na projections, central theme yangu ni 'watu', 'we the people!", hivyo ukiniambia tofauti iliyopo nitakushukuru!.

Pasco
 

Pasco,

So far kampeni za Ukawa hadi hivi sasa zina mapungufu kadhaa.

1. Ukawa walipooza sana katika kipindi cha 2014-2015 katika kudai tume huru ya uchaguzi. Nilishangaa sana. Kwa maana tuliaminishwa kutakuwa na juhudi kubwa kuidai. Mhesabu kura na mtangaza matangazo akikugeuka ni tatizo kubwa.

2. Mwaka huu focus ya Ukawa ni ilele. Adui ni CCM. Tunataka mabadiliko CCM itoke..ikishatoka "mengine" yatafuata. Ukiwauliza Ukawa wengi mtaani kwa sauti ya upole "mengine yapi?" na "yatafuatiaje"? Utajibiwa kaa jeuri pisha kule we gamba mwaka huu tutawanyoosha.
Hata ulitoa dukuduku la jinsi Lowassa na Sumaye walivuogeuka majemedari wa Chadema huku wale askari wao machachari wakitoweka majibu uakayopewa ni makali ya yanayoshusha thamani ya utu.

Ukawa wanakosa kura za watu wengi kwa namna hii na inawaacha wapiga kura wengi wasioipenda CCM kwenye mashaka (dilema).

3. Mpaka sasa hakuna anayeongela na kufafanua kwa wananchi Ilani ya Ukawa itatekelezwaje na ahadi za mabadaliko na maendeleo zitafanyikaje.

Vipaumbele 4 vya Lowassa. Sio vipaumbele 4 vya kwenye ilani ya Chadema.

4. Watu tuliaminishwa na Chadema kwa miaka mingi, kuwa Tz si maskini. Ni tajiri sana. Ila maendeleo yake yamedumazwa na ufisadi na ufujaji mkubwa wa mali za umma na raslimali. Hadi leo tumebakia takribani mwezi mmoja kabla ya uchaguzi hakuna anayesema kwa ufasaha...huyu adui aliyetunyonya tunamwondoaje..tunapigana naye vipi....kwahiyo "we the people" tunabaki na mashaka ya hawa nao ni "wale wale" wanaenda kufanya "hii nasi ni zamu yetu".

5. Chadema na Ukawa wamejenga uadui usio na sababu za msingi na " we the people" tulio na mashaka na tunaoihoji njia ya mabadiliko. Katika kutafuta kura ni kama katika kueneza dini (siasa ni imani), nifundishe, nifafanulie, nishawishi. Kura yangu utapata.

Ni hulka ya binadamu ukimdharau na kumbeza hawezi kukupa kilicho chake. Bahati mbaya walichonacho "we the people" safri hii ni "kichinjio". Ukiwabeza na kiwatukana kuwa ni magamba watakutembezea mkasi mpaka uhisi una nuksi ya kukatwa.

Kuna ambao tunajiliwaza na idadi za mafuriko. Tume imeandikisha takribani watu milioni 23 na wanahamasa ya kupiga kura.
Mpaka sasa sidhani kuna ambaye mafuriko yake yamekwisha fikisha watu millioni 11. Kuna watu wengi wasio Ukawa au CCM wako hapo kati kati.

Kwa mfano nimeangalia mafuriko ya Jangwani wakati wa uzinduzi wa kampeni. Sijaona chama chochote kilichokusanya watu milioni 1.5 hapo jangwani. Hakuna chama kilichovuta zaidi ya robo ya wapiga kura kwenye mafuriko yake. Kujiliwaza na mafuriko ni kujihadaa "we the people" wenye vichinjio wengi wetu hatukwenda kwenye mafuriko. Tulikuwa tunakodolea kwenye TV (pale penye umeme) au kukesha JF hadi usalama wa server ukatikisika.

Yes Pasco, "we the people", na katika uchaguzi wa mwaka huu 1 vote is golden.
 
sw

Mkuu Jozi 1, kwanza asante sana kwa objectivity kwenye bandiko lako hili!. Ukipata nafasi, pitia baadhi ya nyuzi hizi kuhusu Chadema na ushindi wa uchaguzi wa October,'15.
Bada ya uchaguzi wa 2010, niliibuka humu na uzi huu
[h=3]CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga![/h] nikashauri kuchoka kwa CCM, Chadema ikutumie kama fursa, niliishia kubezwa!.
[h=3]Yametimia!, CCM Imechokwa!, CHADEMA Njia Nyeupe 2015!
[/h]Chadema walipohubiri mfuko wa cement utakuwa 5,000 na kutoa elimu bure hadi chuo kikuu na afya bure nikashauri, sasa watuletee wachumi watukokotolee uwezekano huo kiuchumi!, kwa kuonyesha CCM inakusanya kiasi hiki, inatumia vibaya kiasi hiki, ubadhirifu wa kiasi hiki, umefanya ufisadi wa kiasi hiki!, hivyo Chadema ikiingia, vyanzo vya mapato vitakua hivi, tutabana matumizi kwenye maeneo haya, hivyo tutaokoa kiasi hiki!, mahitaji ya cement ni haya, hivyo tutatamia kiasi hiki kama ruzuku!, mahitaji ya afya na elimu bure hadi chuo kikuu ni haya hivyo tutatumia kiasi hiki kugharimia afya na elimu!, hili halikufanyika!. Nilishauri Chadema iwape wananchi reasons za kuichagua besides kuchokwa kwa CCM!.
[h=3]Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa
[/h]Pia nikaeleza
[h=3]Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!...
[/h]siku ile ya mafuriko ya Ukawa Jangani, nilipita pale na kukuta watu wamewehuka na Lowassa, ila ukiwauliza sababu, why Lowassa, hawana sababu!, just Lowassa!.

Hivyo ushindi wa Lowassa utatokana na the 'spirit of victory' iliochochewa na the 'wind of change' which is sweeping accross Tanzania, watu wameichoka CCM for a reason, sasa wanataka mabadiliko, ila ataichagua Chadema na kumchagua Lowassa for no reasons at all!, just that!.
[h=3]Kuelekea Octoba 2015: Je, Hii "Vox Populi" ni "Vox Dei?"
[/h]Pasco
 
Ni kukumbushana tuu to keep the focus, and stay focused not to loose the target!, ibaki kazi moja tuu, tarehe 25 October is to hit the bull! and not to miss it!.

Pasco
 
Ni kukumbushana tuu to keep the focus, and stay focused not to loose the target!, ibaki kazi moja tuu, tarehe 25 October is to hit the bull! and not to miss it!.

Pasco
...................................................
 

With just 7 days to come, hakuna kipya cha kuwaambia wanabodi, bali ni kukumbushana tuu, tulisema nini, nini kimefanyika, nini kinafanyika sasa, na nini kitafanyika hizo siku 7 zijazo, yaani tarehe 25 October, kiukweli kabisa, sioni jinsi yoyote ya CCM kushinda tena!, Chadema inakwenda kuchukua nchi kiulaini kabisa kama imeokota!, yaani CCM inakwenda kuanguka chini kiulani kabisa kama kumsukuma mlevi!.

Lakini ili hili litimie, ni lazima kila aliyejiandikisha, ajitokeze hiyo tarehe 25, aende kupiga kura na kumchagua Edward Lowassa!.

If "Together wa can!", and "United we Stand", "Victory is ascertain!"

Nawatakia Jumapili njema!.

Pasco
 

Pasco Unaumwa na ugonjwa wako ni wa mahaba niue....Lowasa hapiti...na haamtakua rais wa nchi yoyote hapa duniani
 
Mkuu unatakiwa sasa upewe heshima ya 'Muandishi Nguli'.

Hoja yako ya mwaka 2012 inageuka hali halisi ya sasa. Hongera.
 
Pasco mwanakijiji anajaza server na operation zake zisizo na kichwa, mpe makala moja iili ajidharau
 
mwaka huu turnout itakuwa kubwa na CCM itashinda kiulaini bila hata goli la mkono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…