Wanabodi,
Katika thread moja humu jukwaani, nimekutana na mchango wa mwana jf huyu
Kutokana na kauli hiyo, nimekuwa inspired kuandika kidogo kuhusu adui mkuu wa Tanzania wengi wakidhani ni CCM, kumbe sio, bali adui mkuu wa Watanzania ni huyu nimtajae hapa chini na headline imejielekeza kwa Chadema, simplt because ndicho chama pekee so far chenye kuonyesha mwelekeo wa matumaini ya uwezekano wa kulipatia taifa letu la Tanzania, ule ukombozi wa pili wa kweli wa Mtanzania!.
Mkuu Jogi, japo umeniomba "Nikubaalie japo mara hii tu kuwa, tatizo linalotumaliza ni zimwi CCM". Samahani sana, sikukubalii, kwa maoni yangu,
1. Tatizo kubwa la Watanzania sio au adui mkubwa wa Tanzania sio CCM, CCM is just the vehicle, haikujiweka hapo ilipo, imewekwa, hivyo tatizo sio CCM iliyowekwa, bali tatizo ni walioiweka CCM hapo ilipo!. That simply means, tatizo ni sisi Watanzania tulioiweka CCM madarakani and it plays games on us again and again na sisi tukiendelea kuiweka madarakani again and again na sitashangaa kama hata 2015, tukairudisha tena!.
2. Hii dhana ya kudhania adui mkubwa wa Tanzania ni CCM, is a wrong concerpt, na ndilo kosa kubwa la wapinzani, katika chaguzi zote za nyuma kuelekeza concetration ya mashambulizi yote kwa CCM wakijihesabu ndie adui yao mkubwa, hivyo ku miss the real target ya adui halisi ni nani!.
5. CUF baada ya kujaribu mara 3 ikashindwa, ikaamua kutumia principle ya "if you can't beat them, join them", kwa mara ya 4 katika uchaguzi wa 2010, ikakubali yaishe, ikawajoin ndani ya SUK katika ndoa ya kukubali kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM, at the same time, its fighting from within, and is hitting them very hard kwa mtindo wa "kikulacho" na kikundi cha "uamsho" ni matokeo chanya ya kipigo from within, hivyo kwa 2015 upande wa Zanzibar CUF ni njia nyeupe!.
6. Kwa sasa, angalau Chadema, kupitia M4C, imeshagundua adui halisi anayewakosesha ushindi, na sasa imejielekeza kwa wananchi ambao ndio wenye maamuzi ya mwisho na wamekuwa wakiichagua CCM kwa mazoea tuu, hivyo concetration ikiwekwa kwenye "changing mindset ya wenye maamuzi, kuacha kuchagua kwa mazoea tuu, bali kuchagua kwa sababu. Wananchi, watafunguka macho, na hawatakuwa na sababu tena ya kuendelea kuichagua CCM!.
7. Mara baada ya uchaguzi wa 2010 na mafanikio makubwa upande wa Chadema, kwenye ile mada yangu ya "CCM Imechokwa, Chadema Haijajipanga", niliwaeleza kuwa wapinzani bado hawajipanga mkao wa kushika dola, lakini kwa kwa sasa kupitia M4C, Chadema wanaonyesha dalili za kujipanga japo bado wanakabiliwa na madhaifu haya na yale, yakiwemo, lile koti la ukanda, udini, ukabila na ubinafsi wa "umimi" etc.
8. Kwa leo naomba nisiingie tena kwenye udini, ukanda na ukabila wa Chadema, bali naomba nijikite kwenye ubinafsi au "umimi" kwa Chadema kujiamini kupita kiasi kuwa peke yao wataweza!, nilisema peke yao hawawezi, na leo nasema te na na tena, "Chadema peke yenu hamuwezi Kuiondoa CCM Madarakani" kwa sababu hili CCM ni dubwana kubwa sana ambalo haliwezi kung'oka bila umoja ambao ni nguvu ya Watanzania wote wenye kuliutakia mema taifa hili.
9. Kabla ya kauli ya majuzi ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda kule bungeni, nilikuwa najua ma RC na ma DC ni watendaji wakuu wa serikali mikoani na wilayani baada ya kutenganisha zile kofia mbili za chama kushika hatamu za kuiongoza serikali, kumbe wamevua tuu hizo kofia na kutovaa sare, lakini kiutendaji kumbe wako pale kuhakikisha CCM inatawala milele!, hivyo bila joint foces, hakuna jinsi ya kuipumzisha CCM na ni kweli itatawala milele!.
10. Chadema na wapinzani wengine wote wa ukweli, ni lazima wa join forces kutafuta the common working grounds na wenzenu wengine wote mu work together towards a common enemy hata na nyinyi wenyewe kwa wenyewe lazima mkubali kushirikiana kwa kukubali kutokubaliana kwa hayo madogo madogo lakini lazima mkubaliane kwenye kubwa la msingi kwa kukubali "umoja ni nguvu" vinginevyo matokeo ya 2015 yatakuwa ni yale yale ya, vyama vile vile, na watu wale wale!.
11. Mfano, japo CUF ni mke wa CCM kwa upande wa Zanzibar, hiyo ni "marriage of convinience", hivyo inavunjika wakati wowote "conveniences" zikimalizika, hivyo Chadema inacho kibarua kigumu cha kum..ngoza huyu mke wa mtu kwa kumhakikishia akikubali kutoka nje ya ndoa, yeye sasa hatakuwa mke tena, bali atageuka mume na 2015 ni yeye sasa ndie atageuka kidume na kumuoa huyo mume aliyenae sasa kwa sababu mume huyo ategeuzwa mke!.
12. Hakuna ubishi kuhusu nguvu ya CUF kule Zanzibar na Chadema itake isitake, ipende isipende, ili kujihakikishia njia nyeupe ya kuwa mpangaji wa magogoni kwa 2015, ni lazima ikubali kuisupport ya CUF kwa upande Zanzibar ili CUF nao wakubali kuisupport Chadema huku bara!. Chadema wakae chini na CUF, waainishe maeneo ya strong holds za kila mmoja na kuachiana maeneo hayo ili 2015, kuepuka kumfaidisha kunguru kwa vita vya panzi!.
13. Voting statistics
[TABLE="width: 1"]
[TR]
[TD="class: cola, bgcolor: #F3F2DE"]Registered Voters[/TD]
[TD]20,137,303[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: cola, bgcolor: #F3F2DE"]Total votes[/TD]
[TD]8,626,283[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: cola, bgcolor: #F3F2DE"]% Turnout[/TD]
[TD]42.84[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: cola, bgcolor: #F3F2DE"]Valid votes[/TD]
[TD]8,398,394[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: cola, bgcolor: #F3F2DE"]Spoilt votes[/TD]
[TD]227,889[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: cola, bgcolor: #F3F2DE"]% Spoilt votes[/TD]
[TD]2.64[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Table source
Commonwealth 2010, 31.
Results
[TABLE="width: 1"]
[TR]
[TH="bgcolor: #D45008"]Candidate[/TH]
[TH="bgcolor: #D45008"]Party[/TH]
[TH="bgcolor: #D45008"]Votes[/TH]
[TH="bgcolor: #D45008"]% Vote[/TH]
[/TR]
[TR]
[TD]Jakaya Kikwete[/TD]
[TD]Chama Cha Mapinduzi (CCM)[/TD]
[TD]5,276,827[/TD]
[TD]62.83[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]WP Slaa[/TD]
[TD]Chama Cha Demokiasia na Maendeleo (CHADEMA)[/TD]
[TD]2,271,941[/TD]
[TD]27.05[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Ibrahim Lipumba[/TD]
[TD]Civic United Front (CUF)[/TD]
[TD]695,667[/TD]
[TD]8.28[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Peter Mziray Kuga[/TD]
[TD]Progressive Party of Tanzania (PPT-MAENDELEO)[/TD]
[TD]96,933[/TD]
[TD]1.15[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Rungwe Hashim Spunda[/TD]
[TD]National Convention for Construction and Reform (NCCR-Mageuzi)[/TD]
[TD]26,388[/TD]
[TD]0.31[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Muttamwega Bhatt Mgaywa[/TD]
[TD]Tanzania Labour Party (TLP)[/TD]
[TD]17,462[/TD]
[TD]0.21[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Yahmi Nassoro Dovutwa[/TD]
[TD]United People's Democratic Party (UPDP)[/TD]
[TD]13,176[/TD]
[TD]0.16[/TD]
[/TR]
[TR="class: cola, bgcolor: #F3F2DE"]
[TD]Total[/TD]
[TD][/TD]
[TD]8,398,394[/TD]
[TD]99.99[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Table source
Commonwealth 2010, 31.
14. Kwa mujibu wa data hizo, JK amechaguliwa kura milioni 5 tuu kati ya watu milioni 40!. Waliojiandikisha ni milioni 20, lakini waliopiga kura ni milioni 8 tuu!, hii inamaanisha kuna watu milioni 12, ambao walijiandikisha lakini hawakupiga kura kwa sababu mbalimbali, ikiwemo wale waliokata tamaa na kuona kupiga kura ni wastage of time, hata upige vipi kura, matokeo ni yale yale lazima CCM ishinde, hivyo kuliko kupoteza muda wakaachana kabisa na kupiga kura!
15. Suppose 2015, Watanzania tutakuwa Milioni 50 wenye sifa za kupiga kura ni milioni 35, hawa wote wakihamasishwa kujiandikisha na kujitokeza kupiga kura, mgombea wa CCM atajipatia kura zao zile milioni 6 za wanachama wao kwa mujibu wa tovuti ya CCM, halafu hizo kura milioni 29 zimuangukie mgombea wa upinzani, hata NEC ya CCM, wachakachue vipi, there will be no way out!, hivyo adui yetu mkubwa sio CCM, bali ni Watanzania wanaipigia kura CCM!.
Wasalaam.
Pasco.
NB. Pasco wa JF, sio mwanachama, mfuasi wala mshabiki wa chama chochote cha siasa, bali ni Mtanzania wa kawaida mwenye kuweka mbele maslahi ya taifa.