Elections 2015 Kuelekea 2015: CHADEMA Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!

Mchambuzi,nashukuru sana kuja na kurespond.Sikujuwa kwamba tunakubaliana kuhusu hilo la rushwa.Umezungumza ukweli.Nilidhani kwamba ulimaanisha kuwa rushwa/ufisadi,siyo issue ambayo chadema should capitalize on kwenye mpambano wao na chama tawala.

Ni kweli rushwa ni adui wa haki.Ila jambo moja nalotaka kuweka msisitizo hapa,ni kwamba hilo neno,lilikuwa more relevant nyakati zile za mwalimu kuliko sasa.Yes ni adui wa haki,lakini it is more than that,na ndiyo maana sikushangazwa rushwa kuitwa ufisadi,kwasababu it is beyond that.

Nasema hivyo kwasababu madhara ya rushwa nyakati za mwalimu,siyo sawa kabisa na madhara haya tunayoyaona sasa,na nyakati za mwalimu hatukuwa na kina Lowassa wala Rostam Aziz just to name the few.

Rushwa kuwa adui wa haki,nyakati hizo,walengwa walikuwa ni wananchi masikini wasioweza kuhonga(rushwa kubwa wala wizi wa rasilimali havikuwepo kiasi kama chasasa) ili kupata huduma,kwani ina maana kama hawataweza kuhonga,basi hawatakuwa na haki za kimsingi.Hilo lina maana kuwa mwenye uwezo wa kuhonga,ndo mwenye kupewa haki,iwe mahakamani,kwenye huduma muhimu za kijamii,pengine kwenye upatikanaji wa rasilimali kama vile viwanja,nyumba nk.Lakini kuuza nchi kunalofanywa na watawala wa sasa ilikuwa bado!

Nyakati zile,hayo yalimake sense,yani kuishia tu kusema kuwa "rushwa ni adui wa haki"

Kumbuka pia kwamba nyakati zile,kulikuwepo na masikini wengi zaidi kuliko sasa(hapa ni relative to the total population),kwasababu pia inawezekana kuwa masikini wa sasa,ni wengi zaidi kuliko masikini wa kipindi kile(again relative to the total population).

Sasa hapa ndiyo maana statement yako kuhusu "internal development communty",msisitizo upo hapo kwamba suala la rushwa/ufisadi,limeanza kuchukuliwa kama "a development issue & development imperative" kama ulivyoainisha kwenye paragraph yako ya pili.

Nilivyosema kwenye statement ya bandiko langu uliloli quote,nimegunduwa kuwa hatukupishana kwenye hoja hiyo.Na ndiyo maana nika kumention ili uje hapa.Nilimwomba mleta mada aweke wazi kama aliku quote in what context.Lakini kufika kwako,umenisaidia kujuwa context nzima ya bandiko lako.

Pia kwenye issue ya "things right vs right things",ninakubaliana na wewe kwa kiasi flani pale uliposema kwamba dhana zote hufanya vyema kama zikitumiwa zote kwa pamoja.Lakini ndiyo maana nikamwuliza mleta hoja kwamba,je anatumia hizo dhana kwa muktadha gani wa chama cha kisiasa?ili again niweze kupata context pamoja na hoja ya kujadili.

Naona ametoa mapendekezo kwamba anaufunga mjadala huu,na wakati ukweli ni kwamba tulikuwa tukiwasubiri nyie ambao amewa quote ili tuwekane sawa kama nilivyomweleza ndugu Nguruvi3 pamoja na Mzee Mwanakijiji.

Nashukuru sana kwa bandiko lako hili pamoja na response yako.Nategemea tutaendelea kujadiliana na kuelimishana pale inapowezekana.Kiukweli napenda mijadala iende hivi,yani hoja kwa hoja,na kukubaliana pale tunapokubaliana,pia kukubaliana pale tusipokubaliana.
 
Last edited by a moderator:
Thanks Mukandara.
Nadhani hayo ni sehemu ya mabadiliko anayosema Pasco. Kwamba wabadilike kutoka hapo walipo na kurudi katika nafasi yao. Ni ukweli moja ya mambo yaliyowajenga CDM ni sehemu kama hizi, sijui kwanini wameamua kuwa 'out of touch' na public

Pasco ana point kuwa CCM wamechokwa, hata bila sababu nzito watu wamechoka kwasababu hakuna jipya. Wanajua utendaji wa serikali ya CCM, Chama na Bunge. Hawatarajii jambo lolote zaidi kwamba wamefika 'yield point' beyond that..

Matarajio ya Wananchi ni kuona Chademawanaongoza kwa mtazamo na njia tofauti.
Inaonekana huko siko wanakoelekea!
Ifike mahali wananchi waone tofauti ya vyama hivi viwili kiitikadi, kiutendaji na kuwajibika.
Endapo hawatabadilika itafika mahali watu wanasema, better the devil you know than the angel yo don't know.
There should be a clear demarcation between the past and the future.
Mkuu jmushi1, kama nilivyoahidi nipo. Ingawa mjadala unaonekana kufungwa hakika sitasita kutupa neno moja au mawili hasa kujibu hoja yako ya kuwa inaonekana nakubaliana na Pasco.

Ni kweli nakubaliana naye kwa asilimia kubwa sana hata kama si mia moja. Na sababu za kufanya hivyo ni:
1. Kama alivyosema CCM imechokwa, si tu imechokwa bali imechokwa na matendo yake. Chama kilichopo madarakani miaka 50 hakionekani kuwa tumaini kwa Wananchi, badala yake kimegeuka kuwa genge la waporaji na waporaji hao kulindwa kwa kura za wananchi licha ya kuwa uporaji ni wa kodi zao.

2.Wananchi wametafuta mbadala kwa miaka mingi na hakika 'ndele' ya kupendwa imeangukia Chadema.
Ndele hiyo inatokana na jitihada hasa zilizofanyika bungeni kuuonyesha umma wapi tatizo lilipo.
Yule mama aliyehojiwa Iringa yeye alisema 'Anaipenda chadema kwasasababu kama si wao, yeye asingejua uhuni na udhalimu unaoendelea nchi hii'.Hadi hapo Chadema wame win nyoyo za watu kwa kutambua kuwa wapo wanaosimama nao.

3.Mikutano inayoendelea ya M4C ni jambo sahihi, lakini haitoshi tu kuwa sahihi ni lazima ifanyike kwa usahihi.
Mfano, je kila baada ya mkutano kuna ufuatiliaji wa kuimarisha chama eneo husika? Au ni kugawa kadi tu na kukusanya watu na kama ni hivyo je huo ni usahihi hata kama jambo lenyewe ni sahihi?

4.Juzi tumeona picha za CDM mji mwema. Tena viongozi wakionekana kuwa makini. Aliyeleta picha ni mkereketwa wa Chadema na haikuwa na maelezo nini kimesemwa. Mkutano ni jambo sahihi, je, wamelifanya kwa usahihi? Jibu ni hapana kwasababu hawajawasiliana na umma kama ilivyokuwa mwazoni.
Wamekuwa 'out of touch' kwa public kama walivyo kwa JF.
Tayari wameshau ngazi iliyowapindisha na hiyo tu ni tatizo.

5.Pasco amesema lazima wawe tayari kukubali ushauri, na ushauri tuliwahi kutoa kwa kitengo cha mawasiliano ya umma 'public relationship' na ni wazi hawajaufanyia kazi. Hapo nakubaliana na Pasco kuhusu hoja hiyo.

6.Uwajibikaji; Tumeona panga la Arusha na Mwanza kwa madiwani.Uamuzi huo ni sahihi, lakini je wameufanya kwa usahihi? Jibu ni ndiyo na hapana. Ni ndio kwasababu wale wanaoleta vurugu wanapaswa kushughulikiwa.
Ni hapana kwasababu sheria au taratibu zinapindwa kila mara. Kama CDM ilikuwa tayari kupoteza madiwani wa Arusha na wa Mwanza hadi kufikia kupoteza hatamu za umeya katika grassroot level, imeshindikanaje kwa CDM kukubali kupoteza ubunge kwa utaratibu ule ule wanaoutumia? Mbunge mmoja na madiwani 9 ni nani muhimu katika kuimarisha chama.

7.Taratibu zinazowaangukia madiwani kwanini zisitumike kutuliza mtafaruku uliopo BAVICHA?
Ikifika hapo tofauti kati ya CDM na CCM inayowafukuzu makatibu wa matawi na kuwaacha wahalifu NEC na CC haipo.
Inaonekana kama Chadema wanafanya kazi kwa template ya CCM.
Kwa staili hiyo wananchi wataonaje tofauti ya vyama hivi katika kusimamia taratibu zao kabla ya kupewa madaraka!

Hapo ndipo niliposema Chadema lazima iwe na clear demarcation iliwatu waone mbadala walio na matumaini nao.
Ni lazima kuwe na demarcation katika kutoa misimamo ya mambo ya kitaifa. Chadema kama chama pinzani na tegemo kwa wakati mfupi ujao inapaswa kuwa mstari wa mbele katika kujibu, kupendekeza na kunyumbulisha hoja zinazohusu utaifa.
Mfano, nini msimamo wa Chadema kuhusu muungano?

8.Chadema wanapaswa kusimama kama taasisi na si kundi la watu fulani maarufu. Taasisi ina namna ya kupanga na kushughulikia mambo yanayohusiana nayo. Suala la Iringa ni mfano mzuri tu. Imewachukua wiki moja kukabiliana na uharibifu wa taswira ya chama uliohusishwa na tukio. In fact kauli ya Mbowe ilikuwa 'damage control' badala ya statement. Tatizo lisiloonekana kwa wengi ni hili la kutokuwa taasisi kikamilifu na ni ngumu kuliona kirahisi.

9.Kama Chadema hawatajipambanua kama Chama kinachosimamia na kueleza sera zake basi ipo siku wananchi watasema tofauti iko wapi? Hawa wanatenda wale wanakosoa nini kilitakiwa kifanyike!
Kwa maneno mengine ukosoaji pekee hautoshi ni lazima kuwepo na makusudi ya kueleza sera zao.

Chadema isimamie sera zake na kuzieneza na si kubaki katika makabrasha au kukaa kimya zikiporwa.
Hoja kama ya katiba, utawala wa majimbo wameziacha zimeporwa na sasa kuonekana kama za CCM.
Kwanini hili linatokea? Hoja ya katiba ilikuwa sahihi, je ilifanywa kwa usahihi?

Kwa ufupi, Chadema sasa kimekuwa na ni wakati kiongoze. Hoja za kukubaliana na CCM kama ya katiba haionyeshi mbadala. Kwangu mimi CDM walikuwa na hoja na waliwaacha wananchi porini. Nitty gritty!
Pamoja na ukosaoaji sasa ni wakati waeleze wao wana matarajio gani kwa njia gani, rasilimali gani na kipaumbele gani.

Vinginevyo wananchi watasema 'better the devil you know than the angel you don't know'.
The simple way CDM could counter act this arguement is to set a clear goal, and make a clear distinction between the past and the future.
 
Ndugu Nguruvi3,nimekupata vyema sana.

Pamoja na kwamba wewe unakubaliana na Pasco kwa asilimia 90,nimeshangazwa kwamba mimi nakubaliana na wewe kwa asilimia hizo 90 na pasco only 10%.

Sitaki kujuwa hizo asilimia 10 usizokubaliana naye ni hoja zipi hizo,however,lets move on for the sake of our country!

Kusema ukweli kuhusu kuweka distiction kuhusiana na past and the future,naomba niungane na Mag3 kwamba chadema hawajawahi kushika madaraka,na kwahiyo hawawezi kuweka distinction in terms of what they are going to do for the country zaidi ya kuelezea sera na itikadi pamoja na mipango yao kwa taifa,ina maana ni lazima watoe ahadi!Hilo wamefanya sana tu,tatizo ni kwamba ccm wanakuja kupinga,kwa mfano wanasema mfuko wa sementi hauwezi kuwa 5,000 na kwamba elimu na afya haviwezi kuwa bure!

Hayo yalishawezekana chini ya mwasisi wa ccm mwalimu Nyerere kabla hata rasilimali tulizonazo hazijaanza kutumika,na kama rasilimali zetu zikitumika vyema,hayo yanawezekana bila wasiwasi wowote ule!

Pointi yako namba 2,ime sum up everything,yani imejitosheleza kabisa,kwasababu kama wananchi wamegunduwa uhuni wa ccm,na chadema wanasema watafanya kinyume chake,na kuwaelezea wananchi kuwa watathamini mikataba na rasilimali ili viwanufaishe watanzania wote,then whats wrong with that?why doesnt it satisfy you?

Pointi namba 6 nakubaliana na wewe kwasababu kina Zitto wamefanya mabaya kuliko hata hao madiwani!Na ndiyo maana nakubaliana pia na pointi namba 7 kuhusiana na wahuni wachache ndani ya BAVICHA.

Namba 5 sina knowledge kuhusiana nalo,yani kuhusu "kitengo cha public relationship",hopefuly watakuwa wameona hilo,ila ni vyema ukagusia ili niweze kulifahamu.Pia pointi namba 8 ni kama ina uhusiano flani na hii namba 5,kwasababu zote zina mantiki ya kuhusu taasisi na organizational skills.Those are things that they can work on,lakini sidhani kama ni vitu ambavyo vitapelekea Lowassa kushinda,hata kama unakubaliana na Pasco kwa asilimia 90 ama hata 100.

Kuhusu namba 3,tusiwahukumu kabisa,labda tu tuwaulize maswali mawili matatu,kwasababu ninavyofahamu,kutokana na habari za humu,kunakuwepo na daftari la kwawaorodhesha hao wanachama kwenye mikutano yao ya m4c,na kwa maana hiyo,chama lazima kitakuwa kina keep in touch(hopefuly so),kwasababu tayari ni wanachama ambao wako accounted for.So ni lazima kuna njia ya mawasiliano na wanachama hao.(again hopefuly so)

Sasa ni wakati wa kupanda,wakati wa mavuno utakuja!cha muhimu tutakachowashauri ndugu zetu hao,ni kwamba wasipoteze mawasiliano na wanachama wao.Hayo yatahakikishwa na viongozi wao wa vijiji,kata,wilaya nk,wale wa kichama na hata madiwani na mameya.

Mkuu wangu,mwaka 2008,nilishiriki kwenye kampeni ya nyumba kwa nyumba kumsaidia Obama.Na tuliwaandikisha wananchi ambao waliandikiwa email,walitumiwa message za simu,na pia barua!Na pia kuelezwa mipango ya chama,sera nk.

Na pia walifanyiwa mawasiliano kuhakikisha kwamba wamejiandikisha kupiga kura!Those are things that we should advice them kama kweli sisi ni wapenda mabadiliko,na si kukubaliana kuwa no matter what changes they are going to make/have,kama mgombea ni Lowassa basi hawana lao.(as per Pasco)

Nakutakia usiku mwema na ninashukuru sana kwa ushauri huu na response yako.

Viongozi wa chadema hata kama hawachangii humu,wameuona ushauri huo.Nitandelea kukeep an eye ili kuona kama kuna lolote la ziada kutoka kwako na wengineo.Nimefurahishwa sana na moyo uliounyesha wa kutuelewesha humu.

May God continue to bless you,kama kuna ambapo tumepishana,ama kama sijakuelewa vyema,bado unaweza kunijibu,kwani mimi hupendelea mijadala kama hii!

Stay blessed and im looking forward for more wisdom from you!
 
Mkuu jmushi1, kitu kimoja ambacho Chadema ni lazima wa-appreciate, ni kuwa na pool ya kuchukua mawazo mengi na kuyachuja. Kuna hali inayojitokeza siku hizi kuwa watu wakitoa ushauri hata kuisuta Chadema basi wao ni 'waasi'.
Napenda nichukue nafasi kusema kuwa chama imara ni kile chenye wanachama wanaojitambua na kukitambua chama, walio tayari kujikosoa, kukosoana na kukosoa wengine.

Kama ulivyosema nadhani unajua jinsi wenzetu huko kwa Obama wanavyochachafyana ndani ya chama kabla hawajaenda public. Nadhani watu walioshiriki kampeni kubwa na zenye msuguano mkubwa kama wewe ni hazina ya bure kwa wapenda mabadiliko. Kwahiyo wanachama, wapenzi na manazi lazima wakubali challenge za kuimarisha chama.

Ninapomsoma Mchambuzi huwa najiuliza hawa CCM wamelogwa na nani. Kama wangekuwa makini na ku-tap potential kama za akina Mchambuzi pengine leo wangekuwa mtaani, siyo wodini au ICU kama ilivyo.

Kuhusu kitengo cha mawasiliano, nina maana moja kubwa. Ukisoma habari nyingi za mitandao, mitaani na kwingineko, Chadema wana advantage ya kuwa na political base ambayo imehamasika sana.
Ni wajibu wa kitengo hicho kuhakikisha kuwa kuna communications kila mara kutoka sehemu mbali mbali 'in order to keep the flame burning'.

Utasikia mkutano X eneo ABC, wapenzi na wanachama wanabaki 'tuelezeni kuna nanii huko, kimesemwa nini, nani yupo na amejibu nini', tuleteeni pic mwisho wa yote hakuna connection kati ya taarifa ya mkutano X na kile wanachama na wapenzi wanachotaka kusikia. Kitengo cha mawasiliano ya umma lazima kiwe up to date na habari na kiwe kiungo kati ya base ya chama na uongozi (two way traffic)
Niseme ukweli Marehemu Regia (R.I.P) alijaribu sana.

Kuhusu kuwa na tofauti na CCM, hapa hoja yangu kubwa ni kuwa hata kama hawajashika dola basi ndani ya chama lazima kuwe na uwajibikaji, nidhamu na taratibu.

Yasianze yale ya CCM, Rais anasema hili, Waziri mkuu lile, waziri husika hili ili mradi tu kila mtu asikike.
Endapo CDM watakubali utaratibu huo uendelee kama unavyojitokeza basi wananchi watajiuliza, hivi hawa ndani ya chama ni hivi je wakipewa serikali!!!

Yasitokee yale ya CCM kuwa wapo wanachama na wenyechama.

Ninaposema past ninamaanisha kuwa isifike mahali CDM wakawa kama CCM ambao leo wakisema jambo wananchi wanajua, itaundwa tume ya ulaghai, watakwenda mahakamani kuziba midomo na hakuna lingine n.k.

Nina maana kuwa CDM ihakikikishe kuwa ndani ya chama ni madhubuti katika sheria, taratibu na kanuni na hili halihitaji wawe wameshika madaraka.Na kupitia umadhubuti huo ndipo wananchi wataweza ku-predict future kwa uhakika
 
Najisikia raha sana ninapoona watu bado mpo kwenye right track kwenye majadiliano... msafara wa mamba hata kenge tumo. Tusamehane.

Mkuu Pasco nilitingwa kidogo nikajibu juu juu kuwa CCM ikimsimamisha ENL basi Chadema hawana chao 2015.

Mengi yamejadiliwa ila napenda kusisitiza yafuatayo:

1. CDM wajijenge kitaasisi zaidi ya kutegemea personalities.

2. Wafikie wakati wajiweke kwenye misingi ya UTAIFA badala ya kuwa na wawakilishi walio wengi waliotoka sehemu moja kama CUF.

3. CDM waanze ku recruit watu wa kuweza kuwasaidia kwenye uongozi, wasije wakaingia madarakani wakajikuta hawana watu wa kufaa kujaza nafasi nyeti.

4.CDM wawaeleze pia wananchi watawafanyia nini, waache blanket statements za Elimu bure, Afya bure etc hakuna vitu vya bure kwenye ubepari na wakumbuke serikali ya sasa imeshauza karibu vyote nadhani bado Uranium tu.

5. CDM wasijenge imani kubwa sana kwa wananchi waliochoka ambao wanakimbilia dini kama kimbilio la matatizo yao (utitiri wa makanisa ya kufufua, kupewa utajiri etc) baada ya mfumo wa serikali kushindwa kuwasaidia. Wasipokua makini wanaweza kuongoza kwa term moja tu.

Naomba niishie na machache kwa leo. Pasco mkuu, nadhani style yako ya uandishi ni mzuri ila ingekua zuri zaidi kama ungejaribu pia kuwashauri, wote nia yetu ni moja at the end of the day...Taifa zuri lenye uchumi mzuri na maisha bora kwa kila mTanzania.

Huu mjadala umenirudisha kuchangia kwa kirefu. Asanteni kwa michango mizuri
 
Mkuu Just, ukitoa ushauri bila kuombwa, ushauri huo unaweza 1. Hata usisikilizwe, 2. Ukasikilizwa na kupuuzwa 3. Ukasikilizwa na kufanyiwa kazi!.

Ukisikilizwa na kufanyiwa kazi, matokeo chanya yataonekana!. Ukupuuzwa, mambo yatabaki yale yale. Kabla ya uchaguzi wa 2010, kuna mambo Chadema ilishauriwa, ikayapuuza na matokeo ikalizwa!.

Kwa sababu sasa Chadema iko vizuri zaidi, hivyo 2015, inayo nafasi nzuri zaidi ya kuitwaa dola kiulani na kwa kishindo
stahiki!, Lakini ili ifanikiwe kutimiza lengo hilo, bado kuna yale "mambo" ambayo ni lazima yabadilike vinginevyo matokeo ya 2015 ni CCM tena!.

Sisi tusio na vyama, we are side watchers, kazi yetu ni kuangalia mema na mabaya na kuyasema tuu, Chadema inapofanya vyema huwa naipongeza na pale inapo boronga naipaka!.

Subject matter ya mada hii, tayari iko kwa uongozi, nimewashauri this time, wasikilize na kukubali kubadilika, "changes for the better"!.

P.

Pasco hii yako nayo kali sasa CDM inabidi iwe na B4C wachanganye na M4C
 
Kwa kuongezea kuhusiana na hizo dhana mbili,ambapo mwandishi amezielezea kama" double loop learning vs single loop learning",The latter is more of thinking inside the box...
Doing Things Right vs. Doing the Right Things | bSix12 - By Rainer Falle

jmushi 1: Your posting is an exceedingly educative for anyone who wants to be objective in their thinking and action. The challenge here is, what is the political environment in our country today? Is it single loop learning or double loop learning? Are our political parties in any way oriented to the better option? i.e. the double loop learning? How can this school of thought be inculcated within the political leadership which to me I see as the decisive factor in the development of Tanzania. I think Tanzania's development is not impressive after fifty years of independence under the same party ideology. Did the single loop learning influence the whole process or?
 
Mkuu jmushi1, kitu kimoja ambacho Chadema ni lazima wa-appreciate, ni kuwa na pool ya kuchukua mawazo mengi na kuyachuja. Kuna hali inayojitokeza siku hizi kuwa watu wakitoa ushauri hata kuisuta Chadema basi wao ni 'waasi'.
Napenda nichukue nafasi kusema kuwa chama imara ni kile chenye wanachama wanaojitambua na kukitambua chama, walio tayari kujikosoa, kukosoana na kukosoa wengine.

Kama ulivyosema nadhani unajua jinsi wenzetu huko kwa Obama wanavyochachafyana ndani ya chama kabla hawajaenda public. Nadhani watu walioshiriki kampeni kubwa na zenye msuguano mkubwa kama wewe ni hazina ya bure kwa wapenda mabadiliko. Kwahiyo wanachama, wapenzi na manazi lazima wakubali challenge za kuimarisha chama.

Ninapomsoma Mchambuzi huwa najiuliza hawa CCM wamelogwa na nani. Kama wangekuwa makini na ku-tap potential kama za akina Mchambuzi pengine leo wangekuwa mtaani, siyo wodini au ICU kama ilivyo.

Kuhusu kitengo cha mawasiliano, nina maana moja kubwa. Ukisoma habari nyingi za mitandao, mitaani na kwingineko, Chadema wana advantage ya kuwa na political base ambayo imehamasika sana.
Ni wajibu wa kitengo hicho kuhakikisha kuwa kuna communications kila mara kutoka sehemu mbali mbali 'in order to keep the flame burning'.

Utasikia mkutano X eneo ABC, wapenzi na wanachama wanabaki 'tuelezeni kuna nanii huko, kimesemwa nini, nani yupo na amejibu nini', tuleteeni pic mwisho wa yote hakuna connection kati ya taarifa ya mkutano X na kile wanachama na wapenzi wanachotaka kusikia. Kitengo cha mawasiliano ya umma lazima kiwe up to date na habari na kiwe kiungo kati ya base ya chama na uongozi (two way traffic)
Niseme ukweli Marehemu Regia (R.I.P) alijaribu sana.

Kuhusu kuwa na tofauti na CCM, hapa hoja yangu kubwa ni kuwa hata kama hawajashika dola basi ndani ya chama lazima kuwe na uwajibikaji, nidhamu na taratibu.

Yasianze yale ya CCM, Rais anasema hili, Waziri mkuu lile, waziri husika hili ili mradi tu kila mtu asikike.
Endapo CDM watakubali utaratibu huo uendelee kama unavyojitokeza basi wananchi watajiuliza, hivi hawa ndani ya chama ni hivi je wakipewa serikali!!!

Yasitokee yale ya CCM kuwa wapo wanachama na wenyechama.

Ninaposema past ninamaanisha kuwa isifike mahali CDM wakawa kama CCM ambao leo wakisema jambo wananchi wanajua, itaundwa tume ya ulaghai, watakwenda mahakamani kuziba midomo na hakuna lingine n.k.

Nina maana kuwa CDM ihakikikishe kuwa ndani ya chama ni madhubuti katika sheria, taratibu na kanuni na hili halihitaji wawe wameshika madaraka.Na kupitia umadhubuti huo ndipo wananchi wataweza ku-predict future kwa uhakika
Nakubaliana na wewe vitu vingi sana,ila napinga na wewe ktk hizo red...sidhani kuulizia nani yupo katika mkutano si kosa, mimi siwezi enda mkutano wa ccm wakiwepo viongozi wengi sana,ila naweza kwenda msikiliza E.L si kuwa naipenda CCM na pengine hata yeyekura yangu haitokuwepo katika hesabu zake,ila kusikia jinsi gani anajitahidi kuongea ili kujiweka katika upande bora wa historia a u hata Nyerere angekuwepo.Pia hata US wana penda peleka superstars na kuhitaji endorsement za watu waliojijengea taswira njema.

Kuhusu ya wenye chama na wanachama hata CDM nao wanalijua hilo ndio maana huwa wanapenda CCM ikaza masaburi kidogo ili nao wapate upinzani na achievements zao zisiwe za "kimbatiambatia" au za upendeleo.
 
Najisikia raha sana ninapoona watu bado mpo kwenye right track kwenye majadiliano... msafara wa mamba hata kenge tumo. Tusamehane.

Mkuu Pasco nilitingwa kidogo nikajibu juu juu kuwa CCM ikimsimamisha ENL basi Chadema hawana chao 2015.

Mengi yamejadiliwa ila napenda kusisitiza yafuatayo:

1. CDM wajijenge kitaasisi zaidi ya kutegemea personalities.

2. Wafikie wakati wajiweke kwenye misingi ya UTAIFA badala ya kuwa na wawakilishi walio wengi waliotoka sehemu moja kama CUF.

3. CDM waanze ku recruit watu wa kuweza kuwasaidia kwenye uongozi, wasije wakaingia madarakani wakajikuta hawana watu wa kufaa kujaza nafasi nyeti.

4.CDM wawaeleze pia wananchi watawafanyia nini, waache blanket statements za Elimu bure, Afya bure etc hakuna vitu vya bure kwenye ubepari na wakumbuke serikali ya sasa imeshauza karibu vyote nadhani bado Uranium tu.

5. CDM wasijenge imani kubwa sana kwa wananchi waliochoka ambao wanakimbilia dini kama kimbilio la matatizo yao (utitiri wa makanisa ya kufufua, kupewa utajiri etc) baada ya mfumo wa serikali kushindwa kuwasaidia. Wasipokua makini wanaweza kuongoza kwa term moja tu.

Naomba niishie na machache kwa leo. Pasco mkuu, nadhani style yako ya uandishi ni mzuri ila ingekua zuri zaidi kama ungejaribu pia kuwashauri, wote nia yetu ni moja at the end of the day...Taifa zuri lenye uchumi mzuri na maisha bora kwa kila mTanzania.

Huu mjadala umenirudisha kuchangia kwa kirefu. Asanteni kwa michango mizuri
well sasa mh E.L wa nini kama CCM hawahitaji personalities?Au ndio vise versa?kwamba CDM waondoke katik personalities warudi kulipo washinda CCM na CcM waende walipowaweza CDM.I doubt kama wataweza hata.

Pia mjue watu wanaongea very small idea.Arnold alipata ugavana wa Cali kwa persoanilty yake.
 
Mkuu jmushi1, kama nilivyoahidi nipo. Ingawa mjadala unaonekana kufungwa hakika sitasita kutupa neno moja au mawili hasa kujibu hoja yako ya kuwa inaonekana nakubaliana na Pasco.

Ni kweli nakubaliana naye kwa asilimia kubwa sana hata kama si mia moja. Na sababu za kufanya hivyo ni:
1. Kama alivyosema CCM imechokwa, si tu imechokwa bali imechokwa na matendo yake. Chama kilichopo madarakani miaka 50 hakionekani kuwa tumaini kwa Wananchi, badala yake kimegeuka kuwa genge la waporaji na waporaji hao kulindwa kwa kura za wananchi licha ya kuwa uporaji ni wa kodi zao.

2.Wananchi wametafuta mbadala kwa miaka mingi na hakika 'ndele' ya kupendwa imeangukia Chadema.
Ndele hiyo inatokana na jitihada hasa zilizofanyika bungeni kuuonyesha umma wapi tatizo lilipo.
Yule mama aliyehojiwa Iringa yeye alisema 'Anaipenda chadema kwasasababu kama si wao, yeye asingejua uhuni na udhalimu unaoendelea nchi hii'.Hadi hapo Chadema wame win nyoyo za watu kwa kutambua kuwa wapo wanaosimama nao.

3.Mikutano inayoendelea ya M4C ni jambo sahihi, lakini haitoshi tu kuwa sahihi ni lazima ifanyike kwa usahihi.
Mfano, je kila baada ya mkutano kuna ufuatiliaji wa kuimarisha chama eneo husika? Au ni kugawa kadi tu na kukusanya watu na kama ni hivyo je huo ni usahihi hata kama jambo lenyewe ni sahihi?

4.Juzi tumeona picha za CDM mji mwema. Tena viongozi wakionekana kuwa makini. Aliyeleta picha ni mkereketwa wa Chadema na haikuwa na maelezo nini kimesemwa. Mkutano ni jambo sahihi, je, wamelifanya kwa usahihi? Jibu ni hapana kwasababu hawajawasiliana na umma kama ilivyokuwa mwazoni.
Wamekuwa 'out of touch' kwa public kama walivyo kwa JF.
Tayari wameshau ngazi iliyowapindisha na hiyo tu ni tatizo.

5.Pasco amesema lazima wawe tayari kukubali ushauri, na ushauri tuliwahi kutoa kwa kitengo cha mawasiliano ya umma 'public relationship' na ni wazi hawajaufanyia kazi. Hapo nakubaliana na Pasco kuhusu hoja hiyo.

6.Uwajibikaji; Tumeona panga la Arusha na Mwanza kwa madiwani.Uamuzi huo ni sahihi, lakini je wameufanya kwa usahihi? Jibu ni ndiyo na hapana. Ni ndio kwasababu wale wanaoleta vurugu wanapaswa kushughulikiwa.
Ni hapana kwasababu sheria au taratibu zinapindwa kila mara. Kama CDM ilikuwa tayari kupoteza madiwani wa Arusha na wa Mwanza hadi kufikia kupoteza hatamu za umeya katika grassroot level, imeshindikanaje kwa CDM kukubali kupoteza ubunge kwa utaratibu ule ule wanaoutumia? Mbunge mmoja na madiwani 9 ni nani muhimu katika kuimarisha chama.

7.Taratibu zinazowaangukia madiwani kwanini zisitumike kutuliza mtafaruku uliopo BAVICHA?
Ikifika hapo tofauti kati ya CDM na CCM inayowafukuzu makatibu wa matawi na kuwaacha wahalifu NEC na CC haipo.
Inaonekana kama Chadema wanafanya kazi kwa template ya CCM.
Kwa staili hiyo wananchi wataonaje tofauti ya vyama hivi katika kusimamia taratibu zao kabla ya kupewa madaraka!

Hapo ndipo niliposema Chadema lazima iwe na clear demarcation iliwatu waone mbadala walio na matumaini nao.
Ni lazima kuwe na demarcation katika kutoa misimamo ya mambo ya kitaifa. Chadema kama chama pinzani na tegemo kwa wakati mfupi ujao inapaswa kuwa mstari wa mbele katika kujibu, kupendekeza na kunyumbulisha hoja zinazohusu utaifa.
Mfano, nini msimamo wa Chadema kuhusu muungano?

8.Chadema wanapaswa kusimama kama taasisi na si kundi la watu fulani maarufu. Taasisi ina namna ya kupanga na kushughulikia mambo yanayohusiana nayo. Suala la Iringa ni mfano mzuri tu. Imewachukua wiki moja kukabiliana na uharibifu wa taswira ya chama uliohusishwa na tukio. In fact kauli ya Mbowe ilikuwa 'damage control' badala ya statement. Tatizo lisiloonekana kwa wengi ni hili la kutokuwa taasisi kikamilifu na ni ngumu kuliona kirahisi.

9.Kama Chadema hawatajipambanua kama Chama kinachosimamia na kueleza sera zake basi ipo siku wananchi watasema tofauti iko wapi? Hawa wanatenda wale wanakosoa nini kilitakiwa kifanyike!
Kwa maneno mengine ukosoaji pekee hautoshi ni lazima kuwepo na makusudi ya kueleza sera zao.

Chadema isimamie sera zake na kuzieneza na si kubaki katika makabrasha au kukaa kimya zikiporwa.
Hoja kama ya katiba, utawala wa majimbo wameziacha zimeporwa na sasa kuonekana kama za CCM.
Kwanini hili linatokea? Hoja ya katiba ilikuwa sahihi, je ilifanywa kwa usahihi?

Kwa ufupi, Chadema sasa kimekuwa na ni wakati kiongoze. Hoja za kukubaliana na CCM kama ya katiba haionyeshi mbadala. Kwangu mimi CDM walikuwa na hoja na waliwaacha wananchi porini. Nitty gritty!
Pamoja na ukosaoaji sasa ni wakati waeleze wao wana matarajio gani kwa njia gani, rasilimali gani na kipaumbele gani.

Vinginevyo wananchi watasema 'better the devil you know than the angel you don't know'.
The simple way CDM could counter act this arguement is to set a clear goal, and make a clear distinction between the past and the future.
Mkuu Nguruvi3, asante sana kwa post hii, mimi kama binadamu, nilifika mahali, nikwazika, na sasa ndio nimeelewa kwa nini baadhi ya members, huwa wanaikimbia jf, wengine ni kwa kumwaga manyanga, mambo ya humu yanakuwa yamewashinda, lakini wengine ni kwa ku kwazika, kwa member wengine kuwakwaza wenzao!, bandiko hili limenipa faraja, na nimelitumia as closing remarks za kuufunga huu mjadala, asante.
Pasco.
 
Naimalizia hii mada kama ifuatavyo.
UPDATE 3: CLOSING REMARKS YA MKUU NGURUVI3

Mkuu jmushi1, kama nilivyoahidi nipo. Ingawa mjadala unaonekana kufungwa hakika sitasita kutupa neno moja au mawili hasa kujibu hoja yako ya kuwa inaonekana nakubaliana na Pasco.

Ni kweli nakubaliana naye kwa asilimia kubwa sana hata kama si mia moja. Na sababu za kufanya hivyo ni:
1. Kama alivyosema CCM imechokwa, si tu imechokwa bali imechokwa na matendo yake. Chama kilichopo madarakani miaka 50 hakionekani kuwa tumaini kwa Wananchi, badala yake kimegeuka kuwa genge la waporaji na waporaji hao kulindwa kwa kura za wananchi licha ya kuwa uporaji ni wa kodi zao.

2.Wananchi wametafuta mbadala kwa miaka mingi na hakika 'ndele' ya kupendwa imeangukia Chadema.
Ndele hiyo inatokana na jitihada hasa zilizofanyika bungeni kuuonyesha umma wapi tatizo lilipo.
Yule mama aliyehojiwa Iringa yeye alisema 'Anaipenda chadema kwasasababu kama si wao, yeye asingejua uhuni na udhalimu unaoendelea nchi hii'.Hadi hapo Chadema wame win nyoyo za watu kwa kutambua kuwa wapo wanaosimama nao.

3.Mikutano inayoendelea ya M4C ni jambo sahihi, lakini haitoshi tu kuwa sahihi ni lazima ifanyike kwa usahihi.
Mfano, je kila baada ya mkutano kuna ufuatiliaji wa kuimarisha chama eneo husika? Au ni kugawa kadi tu na kukusanya watu na kama ni hivyo je huo ni usahihi hata kama jambo lenyewe ni sahihi?

4.Juzi tumeona picha za CDM mji mwema. Tena viongozi wakionekana kuwa makini. Aliyeleta picha ni mkereketwa wa Chadema na haikuwa na maelezo nini kimesemwa. Mkutano ni jambo sahihi, je, wamelifanya kwa usahihi? Jibu ni hapana kwasababu hawajawasiliana na umma kama ilivyokuwa mwazoni.
Wamekuwa 'out of touch' kwa public kama walivyo kwa JF.
Tayari wameshau ngazi iliyowapindisha na hiyo tu ni tatizo.

5.Pasco amesema lazima wawe tayari kukubali ushauri, na ushauri tuliwahi kutoa kwa kitengo cha mawasiliano ya umma 'public relationship' na ni wazi hawajaufanyia kazi. Hapo nakubaliana na Pasco kuhusu hoja hiyo.

6.Uwajibikaji; Tumeona panga la Arusha na Mwanza kwa madiwani.Uamuzi huo ni sahihi, lakini je wameufanya kwa usahihi? Jibu ni ndiyo na hapana. Ni ndio kwasababu wale wanaoleta vurugu wanapaswa kushughulikiwa.
Ni hapana kwasababu sheria au taratibu zinapindwa kila mara. Kama CDM ilikuwa tayari kupoteza madiwani wa Arusha na wa Mwanza hadi kufikia kupoteza hatamu za umeya katika grassroot level, imeshindikanaje kwa CDM kukubali kupoteza ubunge kwa utaratibu ule ule wanaoutumia? Mbunge mmoja na madiwani 9 ni nani muhimu katika kuimarisha chama.

7.Taratibu zinazowaangukia madiwani kwanini zisitumike kutuliza mtafaruku uliopo BAVICHA?
Ikifika hapo tofauti kati ya CDM na CCM inayowafukuzu makatibu wa matawi na kuwaacha wahalifu NEC na CC haipo.
Inaonekana kama Chadema wanafanya kazi kwa template ya CCM.
Kwa staili hiyo wananchi wataonaje tofauti ya vyama hivi katika kusimamia taratibu zao kabla ya kupewa madaraka!

Hapo ndipo niliposema Chadema lazima iwe na clear demarcation iliwatu waone mbadala walio na matumaini nao.
Ni lazima kuwe na demarcation katika kutoa misimamo ya mambo ya kitaifa. Chadema kama chama pinzani na tegemo kwa wakati mfupi ujao inapaswa kuwa mstari wa mbele katika kujibu, kupendekeza na kunyumbulisha hoja zinazohusu utaifa.
Mfano, nini msimamo wa Chadema kuhusu muungano?

8.Chadema wanapaswa kusimama kama taasisi na si kundi la watu fulani maarufu. Taasisi ina namna ya kupanga na kushughulikia mambo yanayohusiana nayo. Suala la Iringa ni mfano mzuri tu. Imewachukua wiki moja kukabiliana na uharibifu wa taswira ya chama uliohusishwa na tukio. In fact kauli ya Mbowe ilikuwa 'damage control' badala ya statement. Tatizo lisiloonekana kwa wengi ni hili la kutokuwa taasisi kikamilifu na ni ngumu kuliona kirahisi.

9.Kama Chadema hawatajipambanua kama Chama kinachosimamia na kueleza sera zake basi ipo siku wananchi watasema tofauti iko wapi? Hawa wanatenda wale wanakosoa nini kilitakiwa kifanyike!
Kwa maneno mengine ukosoaji pekee hautoshi ni lazima kuwepo na makusudi ya kueleza sera zao.

Chadema isimamie sera zake na kuzieneza na si kubaki katika makabrasha au kukaa kimya zikiporwa.
Hoja kama ya katiba, utawala wa majimbo wameziacha zimeporwa na sasa kuonekana kama za CCM.
Kwanini hili linatokea? Hoja ya katiba ilikuwa sahihi, je ilifanywa kwa usahihi?

Kwa ufupi, Chadema sasa kimekuwa na ni wakati kiongoze. Hoja za kukubaliana na CCM kama ya katiba haionyeshi mbadala. Kwangu mimi CDM walikuwa na hoja na waliwaacha wananchi porini. Nitty gritty!
Pamoja na ukosaoaji sasa ni wakati waeleze wao wana matarajio gani kwa njia gani, rasilimali gani na kipaumbele gani.

Vinginevyo wananchi watasema 'better the devil you know than the angel you don't know'.
The simple way CDM could counter act this arguement is to set a clear goal, and make a clear distinction between the past and the future.

CLOSING REMARKS.
Wababodi, baada ya 25 pages each with twenty posts, with a total 500 Posts Plus, imethibitika pasi shaka kuwa uchaguzi wa 2015, Ikulu ni ya Chadema, hivyo sasa kuelekea 2015, kila dalili zinaelekeza Chadema kuchukua nchi, ila kwa maoni ya wengi serious waliochangia thread hii (ukiondoa wale wa ushabiki), wengi wamekubali Chadema iko on the right track, ila ili kutimiza lengo hilo la kubisha hodi ikulu, na kukubaliwa kuwa mpangaji rasmi wa jengo lile, lazima Chadema ikubali kubadilika, apart from doing the right thing kama inavyofanya sasa, it got to do things right!.

Baada ya maneno haya, sasa kwa heshima na taadhima naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa hawa wafuatao.
  • Mkuu Mkandara, topic yako ya ndio was the inspiration ilionifanya kuanzisha hii thread na niliepuka kukutaja wala kukuquote popote kwa sababu maalum. Asante kwa kujitanabaisha kama mwana Chadema ambaye uko tayari kusimama na ukweli, "no matter what"
  • Mzee Mwanakijiji , ile quote yako niliyoitumia humu, imekuwa kama ndio "colabo" ya hit single kwa mwanamuziki mchanga, kumshirikisha "star mkubwa" ili atoke!, ndivyo ilivyokuwa hii thread, imefikisha record hits kwa mada yangu yoyote kufikisha posts 500 in two days, hii ndio mara yangu ya kwanza, na naamini kuna wachangiaji walichangia thread hii kwa ajili ya quotation yako. Ingawa wewe binafsi hukuchangia kwa sababu ambazo ninazifahamu fika, thanks for being you, who you are!.
  • Mkuu Mchambuzi, ule uzi wako wa ndio the subject matter ya hii mada, kwa jinsi ninavyokusoma humu, naamini wewe ni genius kwenye politics zetu, kama Chadema wanakusoma na kuzifanyia kazi hoja zako, 2015, hatuzungumzii ushindi wa Chadema, bali how big the margin is, kati ya mshindi na mshindwa!.
  • Mkuu Nguruvu3, wewe ni other political genius wetu humu, nilikufahamu kupitia theory yako ya "demage control" na kuendelea kukufuatilia kule kwenye Jukwaa lako, hii closing remarks yako, ni faraja kubwa kwangu, kuendelea kuibua topic ambazo sio popular kwa wana jf wengi, ila huu ndio ukweli halisi ambapo siku zote, kweli itasimama.
  • Na mwisho, napenda kuwashukuru, wachangiaji wote mlioungana nami katika mada hii, ni vigumu kumtaja kila mtu, lakini shukrani za pekee ziende kwa wachangiaji changamoto akiwemo Mag3, J Mushi, Nicholas, na wengine wengi ambao japo hatukubaliani, lakini tumeishia kukubali kutokubaliana na hii ni healthy kwenye mjadala wowote. Mimi pia ni binadamu kama binadamu wengine, huwa nakwazika na kuwakwaza wengine, na especial kwenye mada yoyote inayomhusu "yule mgombea wangu"! tusameheane na tuzidi kusonga mbele kwa maslahi ya taifa.

Nakufikia hapa, naomba sasa ku declare rasmi, mjadala huu, umefungwa rasmi!
this Topic is officially Closed by the thread starter!!
 
Huku ikiwa imebakia miaka mitatu kamili kuelekea uchaguzi mkuu wa urais hapa nchini (2015) sioni kama kuna mipango madhubuti kwa upinzani (hususani CHADEMA) kuingia ikulu, hii ni kutokana na mwenendo wa upinzani katika kuimarisha mshikamano ndani ya chama.

Ikumbukwe tu CHADEMA kimekuwa mstari wa mbele katika kufukuza madiwani wake (rejea arusha na mwanza) hali inayopelekea jamii ya maeneo husika kugawanyika juu ya mtazamo wao kwenye chama.

Mgawanyiko huu umekuwa mtaji mzuri kwa chama tawala (vita vya panzi furaha kwa kunguru). Ikumbukwe pia nchi yetu haina misingi mizuri ya kidemocrasia kama ilivyo kwa nchi nyingi za kiafrika, hali inayozidisha ukweli kuwa chama tawala hakitakubali kuiachia nchi kirahisi.

Kumaliza tofauti kwa njia ya kuvumiliana na kupatana ni bora kuliko kutengana na kuwaambia watu anaetaka kuendelea na mimi aendelee asiyetaka amue pa kwenda
 
Mkuu mbona umekurupuka ? nani kakukurupua ghafla?... ka vipi piga kiloba kwanza... wapi kuna mpasuko? M4c Huioni Kujipanga aje?
 
Fukuza madiwani wote wakapokonywa umeya maamuzi mengine kama yanamsukumo wa viroba.Mnashindwa kuwapatanisha madiwani wenu something is wrong somewhere
 
kwahiyo wataka walee uvundo ndio uone mshikamano?cdm cyo kama magamba wanaolea uchafu ndani ya chama,na maandalizi ya kuingia ikulu huyaon? M4C huon mkuu?
 
Kweli nakwambia ni mara 1000 chadema washindwe kuchukua dola kuliko kuendekeza Rushwa kwenye chama eti tu sababu watapoteza wanachama, kama hujui kinachofanya chadema kiwe na wapenzi wengi ni kitu kimoja muhimu ambacho inabidi chadema wakizingatie sana, ni utaifa.. kulinda maliasili. na kupambana na mafisadi mpka ieleweka. nawapenda chadema kwa msimamo. hakuna unafki wala kubembelezana eti kwasababu ukitoka watu watapungua. kama chadema kitasimama katika hili baada ya miaka kadhaa watu watakielewa sana.
 
sina uhakika, lakini nasikia sumaye aliomba kuingia chadema ili agombee urais. kama chadema wakimkubalia, basi bila shaka chadema kitapoteza wana chama wengi tu na kitaanguka vibaya. kama kimewaza kufika hapa bila kuwategemea hao mafisadi ambao wakishindwa ndiyowana ona umuhimu wa chadema. na nina uhakika chadema wana mtaji mzuri tu wa kuandaa viongozi bora wanaoweza kugombea nafasi ya urais
 
Nalazimika kuamini kuwa uwanja huu umeingiliwa na wanafunzi wa sekondari za kata, hivi mwenye macho anaambiwa tazama? Je, kama madiwani hao walifukuzwa kwa sababu za Rushwa, ubadhilifu na utovu wa nidhamu kwa kuvunja miiko ya chama watabembelezwaje? CDM ni chama makini kinachojali utaratibu na kina miiko yake ambayo inamhusu kila mwanachama. Rushwa na ndugu zake ni adui mkubwa wa chama kwa sababu kinawanyima wananchi haki zao. Ukikiuka taratibu unapigwa chini bila kuangalia nafasi yako.
 
Back
Top Bottom