Wanabodi, Preamble: "Kwa opinion yangu, Uchaguzi wa 2015, Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!"!Trend za Upepo wa Kisiasa kuelekea 2015, zinavuma kwa Kasi ya Ajabu kuelekea Direction ya Mabadiliko (The Wind of Change, is Sweeping Across Tanzania) na kila dalili inaonyesha na kuelekeza Chadema is gaining momentum and there is nothing to stop it kuchukua nchi mwaka 2015 iwapo...
- Hakuna ubishi kuwa siku zote, CCM imekuwa ikishinda chaguzi mbalimbali "kihalali" na mtaji wao mkubwa wa ushindi ni "watu".
- Hakuna ubishi kuwa CCM kama chama, kimechoka, dalili zote za chama kichovu kinachosubiri kifo, tayari, zimeisha jitokeza kwa CCM, kinachosubiriwa sasa its only a matter of time ni lini kitaangwa rasmi, hiyo 2015 naiona kama vile ni mbali, unless wamsimamishe their one and only jewel!.
- Hakuna ubishi kuwa wengi wa hao "watu", wamekuwa wakiichagua CCM sio kwa sababu wanaipenda sana!, (waipende kwa lipi?), la hasha!, "watu" wamekuwa wakiichagua CCM kwa mazoea tuu!.
- Hakuna ubishi, kuwa wengi wa hao "watu" waliokuwa wakiichagua CCM kwa mazoea tuu, sasa wameichoka, hivyo uchaguzi wa 2015, hawatachagua tena chama kwa mazoea, bali watachagua chama kwa "sababu"!.
- Hakuna ubishi kuwa Chadema, ndicho chama kinachokubalika zaidi kwa sasa kuliko CCM, hivyo ule mtaji mkubwa wa CCM iliyoutegemea kwa miaka nenda miaka rudi, sasa umehamia Chadema!.
- Kama ambavyo CCM imekuwa ikichaguliwa kwa mazoea tuu, na sasa CCM imechokwa, vivyo hivyo kwa sasa Chadema haina lolote la kukifanya kipendwe, bali kinapendwa kwa sababu "watu" wameichoka CCM!.
- Kama uchaguzi utaitishwa leo, Chadema itashinda kwa kishindo kikubwa cha ajabu, lakini ukiwauliza hao watakaokipa Chadema ushindi, ni sababu zipi za kuichagua Chadema, hawatakupa sababu yoyote zaidi ya kuichagua Chadema kwa sababu wameichoka CCM!.
- ili Chadema iweze kupata ushindi wa Tsunami kwa uchaguzi wa 2015, lazima Chadema ikubali kubadilika, isiendelee kuutegemea huu umaarufu wa muda kwa kushangiliwa na umati wa watu walioichoka CCM, bali Chadema sasa lazima iwape Watanzania sababu za kuichagua Chadema!.
- So far so good, Chadema is doing a good job chini ya Uongozi Shupavu wa Kamanda Mbowe na kinara wa M4C, Dr. Wibroad Slaa, Chadema is doing the right thing!. Doing the right thing alone, doesn't guarantee sweet clear victory for Chadema, it got to do things right!. Hii inamaanisha ili Chadema ishinde kwa kishindo kinachotakiwa, lazima ikubali kubadilika and start doing things right besides doing the right thing!.
- Hivyo ndugu zangu viongozi wa Chadema najua 2015 mmedhamiria kwa dhati kuchukua nchi kwa ushindi wa kishindo!, lakini ili lengo hili litimie, ni lazima kwanza mkubali kusikiliza, pili mkubali kuzifanyia kazi hizi hoja na tatu mkubali kubadilika!.
Naomba kumalizia kwa nukuu kutoka kwa mmoja wa wanachama wetu humu jf.Kwa wale wapenzi wa Chadema, for sure, Uchaguzi wa 2015, Chadema inaweza kabisa Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If "Itabadilika" and provided that CCM haitamsimamisha yule mgombea wangu!. Japo ni vema kuwa na great expectations on Chadema kuchukua nchi 2015, only if Chadema itabadilika, vinginevyo keep hopping for the best na kama Chadema haitabadilika, you better get prepared for the worst kwa sababu 2015 itakuwa ni CCM Tena!.NB. Msiniulize Chadema wabadilike nini, wahusika wameshaambiwa imebaki kusikiliza na kutekeleza!.Naomba kuwasilisha.Pasco.UP DATE 1.Kufuatia maswali mengi kuhusu Chadema wabadilike nini, naomba kumnukuu mmoja wa great thinkers wetu humu jukwaani
NB. Kwa maswali yoyote kuhusu haya mambo ambayo Chadema inahitaji kubadilika, naomba uyaelekeze moja kwa moja kwenye thread husika hapa.
CHADEMA: Tujadili Utayari wa Kutawala Nchi 2015
UPDATE 2: Input ya Mchambuzi.
UPDATE 3: CLOSING REMARKS YA MKUU NGURUVI3
CLOSING REMARKS.
Wababodi, baada ya 25 pages each with twenty posts, with a total 500 Posts Plus, imethibitika pasi shaka kuwa uchaguzi wa 2015, Ikulu ni ya Chadema, hivyo sasa kuelekea 2015, kila dalili zinaelekeza Chadema kuchukua nchi, ila kwa maoni ya wengi serious waliochangia thread hii (ukiondoa wale wa ushabiki), wengi wamekubali Chadema iko on the right track, ila ili kutimiza lengo hilo la kubisha hodi ikulu, na kukubaliwa kuwa mpangaji rasmi wa jengo lile, lazima Chadema ikubali kubadilika, apart from doing the right thing kama inavyofanya sasa, it got to do things right!.
Baada ya maneno haya, sasa kwa heshima na taadhima naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa hawa wafuatao.
- Mkuu Mkandara, topic yako ya ndio was the inspiration ilionifanya kuanzisha hii thread na niliepuka kukutaja wala kukuquote popote kwa sababu maalum. Asante kwa kujitanabaisha kama mwana Chadema ambaye uko tayari kusimama na ukweli, "no matter what"
- Mzee Mwanakijiji , ile quote yako niliyoitumia humu, imekuwa kama ndio "colabo" ya hit single kwa mwanamuziki mchanga, kumshirikisha "star mkubwa" ili atoke!, ndivyo ilivyokuwa hii thread, imefikisha record hits kwa mada yangu yoyote kufikisha posts 500 in two days, hii ndio mara yangu ya kwanza, na naamini kuna wachangiaji walichangia thread hii kwa ajili ya quotation yako. Ingawa wewe binafsi hukuchangia kwa sababu ambazo ninazifahamu fika, thanks for being you, who you are!.
- Mkuu Mchambuzi, ule uzi wako wa ndio the subject matter ya hii mada, kwa jinsi ninavyokusoma humu, naamini wewe ni genius kwenye politics zetu, kama Chadema wanakusoma na kuzifanyia kazi hoja zako, 2015, hatuzungumzii ushindi wa Chadema, bali how big the margin is, kati ya mshindi na mshindwa!.
- Mkuu Nguruvu3, wewe ni other political genius wetu humu, nilikufahamu kupitia theory yako ya "demage control" na kuendelea kukufuatilia kule kwenye Jukwaa lako, hii closing remarks yako, ni faraja kubwa kwangu, kuendelea kuibua topic ambazo sio popular kwa wana jf wengi, ila huu ndio ukweli halisi ambapo siku zote, kweli itasimama.
- Na mwisho, napenda kuwashukuru, wachangiaji wote mlioungana nami katika mada hii, ni vigumu kumtaja kila mtu, lakini shukrani za pekee ziende kwa wachangiaji changamoto akiwemo Mag3, J Mushi, Nicholas, na wengine wengi ambao japo hatukubaliani, lakini tumeishia kukubali kutokubaliana na hii ni healthy kwenye mjadala wowote. Mimi pia ni binadamu kama binadamu wengine, huwa nakwazika na kuwakwaza wengine, na especial kwenye mada yoyote inayomhusu "yule mgombea wangu"! tusameheane na tuzidi kusonga mbele kwa maslahi ya taifa.
Nakufikia hapa, naomba sasa ku declare rasmi, mjadala huu, umefungwa rasmi!
this Topic is officially Closed by the thread starter!!