RaiaMbishi
JF-Expert Member
- Jan 18, 2012
- 252
- 127
Kwa upande mmoja, iwapo Lowassa atateuliwa kuwa mgombea, Chama kitameguka kupitia watu kama kina Sitta, Membe, Mwakyembe, Nape, Mwandosya, Salma Kikwete, Ridhiwani, Mengi na wafuasi wao mbalimbali ambao watahamishia nguvu zao kwa chama kingine cha upinzani.
Kwa upande mwingine, iwapo Jina la Lowassa litakatwa na sekretarieti ya Kamati Kuu ya CCM katika hatua za awali, Chama kitameguka kupitia ushawishi wake mkubwa kwenye NEC, UWT, UVCCM, "Wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa", na marafiki zake nchi nzima wenye mafanikio kibiashara ambao ndio wafadhili wakubwa wa CCM katika maeneo yao.
Maswali muhimu yanayofuatia ni je:
a) Mpasuko upi ni nafuu kwa CCM? Kwanini/kivipi?
b) Mpasuko upi ni kheri kwa Chadema? Kwanini/kivipi?