Elections 2015 Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa...

Elections 2015 Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa...

Kwa upande mmoja, iwapo Lowassa atateuliwa kuwa mgombea, Chama kitameguka kupitia watu kama kina Sitta, Membe, Mwakyembe, Nape, Mwandosya, Salma Kikwete, Ridhiwani, Mengi na wafuasi wao mbalimbali ambao watahamishia nguvu zao kwa chama kingine cha upinzani.....
RaiaMbishi,
Kwenye italic nyekundu umekosea Big Time! Nakupa dondoo ndogo tu hapa chini kwa snap shot za tweet za Mengi ukishindwa kuelewa muulize Pasco wa JF
1005728_581975848519890_1270926761_n.jpg

 
Last edited by a moderator:
Wazalendo yetu macho tu hata nyie CDM kama mnajua kuna mtu bora zaid ya waliowahi kugombea muandaeni mapema...tena kwa nia safi

2015 makunyanzi sio hoja tena...

Suala la nani anafaa ni juu ya vyama husika na kamati zao ila asije mtu kutaka kubadili uamuzi dakika ya tisini wakati muda ndo huu wa kufanya maandalizi
 
Hapo kwenye RED:
Mada yako inaweza ikawa na malengo mazuri lakini hoja zake ni KAPUT na kama sivyo hivyo basi zitakuwa ni hoja za KIUDAKU na ama siyo za kiudaku basi wewe utakuwa ni Lowassa au mtu aliye karibu sana na Lowassa.

Utajenga vipi hoja kwa jambo ambalo halipo?. Kwani Lowassa katangaza kuwa atagombea na zaidi kabisa, hujasema kile atakacho gombea.
Wewe kaa tu usubiri press conference mapema mwaka 2015 akiwa mzima na sisi tukiwa wazima, kama njia yako ya kujihakikishia kwamba atagombea;
 
RaiaMbishi,
Kwenye italic nyekundu umekosea Big Time! Nakupa dondoo ndogo tu hapa chini kwa snap shot za tweet za Mengi ukishindwa kuelewa muulize Pasco wa JF
1005728_581975848519890_1270926761_n.jpg

Tangia ya Kibanda yamkute yaliyomkuta, Pasco hana ujasiri tena kwani anahitaji macho yake kushuhudia uchaguzi wa 2015 na meno yake kutafuna ndafu kusheherekea ushindi wa CCM au Chadema kutegemeana ataegemea wapi;
 
Humu kuna wajuvi wa mambo na mahayawani......kama wewe sio hayawani nionyeshe ni wapi Lowassa kasema anagombea urais 2015?

Pengine ulitaka nianze na neno "iwapo", haya basi jumuisha hilo; vinginevyo kaa ukisubiri press conference 2015, iwapo (again) yeye na sisi tutakuwa bado wazima;
 
Wewe kaa tu usubiri press conference mapema mwaka 2015 akiwa mzima na sisi tukiwa wazima, kama njia yako ya kujihakikishia kwamba atagombea;
Hicho ndicho nilikuwa ninakitaka kiwe msingi wa hoja yako kuliko kuanza kujadili kitu ambacho hatufahamu kama kitatokea.
 
Kwa upande mmoja, iwapo Lowassa atateuliwa kuwa mgombea, Chama kitameguka kupitia watu kama kina Sitta, Membe, Mwakyembe, Nape, Mwandosya, Salma Kikwete, Ridhiwani, Mengi na wafuasi wao mbalimbali ambao watahamishia nguvu zao kwa chama kingine cha upinzani.

Kwa upande mwingine, iwapo Jina la Lowassa litakatwa na sekretarieti ya Kamati Kuu ya CCM katika hatua za awali, Chama kitameguka kupitia ushawishi wake mkubwa kwenye NEC, UWT, UVCCM, "Wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa", na marafiki zake nchi nzima wenye mafanikio kibiashara ambao ndio wafadhili wakubwa wa CCM katika maeneo yao.

Maswali muhimu yanayofuatia ni je:

a) Mpasuko upi ni nafuu kwa CCM? Kwanini/kivipi?
b) Mpasuko upi ni kheri kwa Chadema? Kwanini/kivipi?
cha msingi wajiandae tu kukabidhi madaraka kwa wananchi.
 
Atakae mkimbia lowassa na kwenda upinzani basi itakua ndi mwisho wake kwenye game ya siasa.... ukikimbia ushindi basi wewe umeshindwa. Kwa mtiZamo wa wananch wenye mawazo chanya tunahitaj mzalendo wale wenye uvivu na uzembe kwenye maofis yao ndo itakua mwisho wao.
 
nionavyo mimi,lowasa anarudisha chenji ya kile alichoiba kwa kusaidia vikundi mbalimbali. wakijiroga wakapitisha jina lake, bas chadema waanze tu kupanga barraza la mawaziri mapema,ila nakubaliana kuwa wakikata jina lake watapata cha kusema hawa zz m
 
CCM Haina mtu sahihi atakaye wakomboa kwenye mikono safi ya CDM YANI 2015 Ndio ALFA NA OMEGA WA ccm VIVA CDM
 
Aina ya watu kama Lowasa na Mwigulu wanaotaka kutawala (si kuongoza) kwa gharama yoyote ni hatari sana kwa nchi hii. Hawa ni wagonjwa wa ugonjwa mbaya kabisa unaoweza kumpata binadamu, wangekuwa mbwa tungesema wana 'rabbies' ugonjwa ambao unatibiwa kwa ...........
 
Hata kama hajasema inasemwa mtawatambua kwa matendo yake matendo yake yanaonyesha ana nia hiyo sana wala haiitaji kwenda maabara kugundua hilo,umefika Monduli? unajua maisha ya wana monduli? ni wema gani wa kujitolea kuwachangia wana Mwanza na watu wanaoishi Lendikinya hawana hata maji sembuse maji masafi wala barabara kwanini hao marafiki zake wasimsaidie jimboni kwake huu ni mfano wa eneo moja tu la Monduli acheni ujuha Lowassa anataka Urais na wala haiitajiubishi.
 
Kwa ombwe lililopo serikalini na CCM hakuna wa kusimamisha UCHU wa uraisi wa Lowasa, ni UCHU wake huo huo uliopitiliza ndio utakaommaliza! He will overshoot the runway, wait and see.
 
Ukikosa njia heri ukae hapo hapo kiliko kwenda popote, EL kakosa njia ya urais kweli sasa anakwenda popote hata makanisani, misikitini , tutaona mengi subiri kidogo tu, ataanza na misabani, viwanjani na harusini, harusi yako anatoa mikwanja zaidi ya bajeti yako, upo hapo
 
nchi hiii lazima iongozwe na chadema 2015 - 2020 hata asimame ndani ya ccm,,,, labda mungu, lakn binadam yeyote akisimama ndani ya ccm nachagua jiwe:love:chadema the rulling part of united republic of tanzania:A S-fire1::A S-fire1::A S-fire1:
 
Mpaka sasa kuna kila dalili kuwa mgombea urais wa CCM 2015 huenda akawa Edward Lowassa kutokana na nguvu ya kisiasa aliyonayo ndani ya CCM kwa sasa hususani kwa wajumbe wengi wa vikao vikuu vya juu vya maamuzi ndani ya CCM(Kamati kuu, Halmashauri kuu na Mkutano Mkuu).
Wakati huo huo kama kuna jambo wanachama wa CHADEMA wangependa kuliona basi ni Lowassa kuwa mgombea urais wa CCM 2015.
Kwa sababu zifuatazo:

1/Moja ya hoja zilizoipa nguvu sana na Umaarufu mkubwa sana CHADEMA ni Vita dhidi ya Ufisadi, Lowassa ni mtu anaaminiwa kama fisadi zaidi kuwahi kutokea ndani ya CCM, hivyo kutaipa nguvu zaidi CHADEMA katika harakati zao.

2/Kumbukumbu isiyofutika ya kitendo cha Lowassa kujiuzuru uwaziri mkuu kutokana na kuhusika katika Ufisadi mkubwa wa mkataba tata wa kampuni ya kufua Umeme wa dharura(Richmond).

3/Vita ya kufa na kupona kati ya Lowassa dhidi ya makundi mengine ya wanaCCM wenzie wanaoutaka urais pia, ambao wamekuwa kila mara wakianikana baadhi ya maovu yao hadharani. Katika hili atakosa 'Support' muhimu kutoka kwa wanaCCM wengine 'muhimu' wanaomchukia.
 
Back
Top Bottom