Elections 2015 Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa...

Elections 2015 Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa...

zomba usihangaike sana ukapoteza nguvu zako iko hivi CDM ni chama kizuri sana cha upinzani lkn ukweli bado muda wa sisi kukipa madaraka makubwa. kimsingi nakuambia Lowassa ndiye mtu anayeweza kutawala chi hii ukilinganisha na cv za wengine wote ambao wanajiita wanasiasa mashuhuri

Huo ndio ukweli wasioupenda hawa wapinzani wakuu.
 
ha ha ha mzee uko kwenye payroll ya Fred Lowasa nini?

Hapana. Akigombea Zitto, kura yangu itaenda kwa Zitto. Akigombea Sitta na Slaa, simpigii yeyote kati yao. Akigombea Lowassa na yeyote mwingine chadema kura yangu kwa Lowassa.

Zimwi likujualo halikuli likakwisha.
 
Wanabodi,

Baada ya kumsikiliza kwa makini Waziri Mkuu "Mstaafu", Edward Lowassa katika two- series za kipindi cha Dakika 45 cha ITV, kwanza nimekubali sana huyu jamaa!, pili kama yeye ndiye angekuwa rais, ile 2005,
Tanzania tusingefikia hapa tulipofikishwa sasa na utawala wa JK, ila kikubwa zaidi, (kama ni kweli afya yake sio mgogoro kama anavyodai yuko fit, japo he looks sick), CCM ikimsimamisha yeye kugombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, them matokeo ya urais kwa 2015, ni CCM tena!. Mkubali, mkatae!.

Hizi ni baadhi tuu ya sababu, kwanini CCM itashinda tena, endapo and only if itamsimamisha Lowassa!.

1. Uwezo wa Kupanga, Kusema, Kusimamia na Kutenda.
Viongozi karibu wote waliopo CCM, wana uwezo mkubwa sana kupanga wa kusema tuu, (Mkukuta, Mkumbita, Mkurabita, Mkuza, na sasa Dira 2025), lakini hawana uwezo wa kusimamia na kutenda!, mipango mingi iliyopangwa, inaishia kwenye maneno na vitendo sifuri!. Edward Lowassa sio msemaji, bali ni mtendaji, yeye sio mtu wa maneno mingi, ni mtu wa vitendo virefu, he is an action oriented man!.

Tulipopata uhuru miaka ya 60, maadui wetu wakuu watatu, walikuwa ni Elimu, Umasikini na Maradhi, na tulijiwekea misingi yetu mikuu minne ya maendeleo kuwa ili tuendelee, tulihitaji vitu vinne: Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora!. Kwenye hiyo misingi, tulisema Pesa sio msingi, pesa ni matokeo!, hili ndilol lililokuwa kosa pekee la Mwalimu, kutofautiana na misingi ya ukweli ya uchumi, kama ilivyofundishwa na Adam Smith (land, labor, capital na interpreneureship)!. Kwenye ile mising minne tulisahau capital!.

Watu tunao na ardhi ya kutosha, yenye rutuba, vyanzo lukuki vya maji, madini, maliasili etc etc tunazo. Tulikuwa na tatizo la siasa safi na uongozi bora, ndio maana nchi tulizopata nazo uhuru, wao wakiwa ni masikini wa kutupwa with nothing, kana Tiger nations, leo wako mbali!, sababu pekee iliyowafikisha wenzetu pale walipo, wakati sisi tunaendelea kupiga mark time ni Elimu!. Sisi tulitaja tuu kuwa Elimu ni adui, lakini we never invested because we had no capital. Nyerere aligombana na maprofesor wa uchumi, Kina Prof. Rweyemamu, wakajitimkia zao, akagombana na IMF, WB etc matokeo tunayajua!.

Lowassa na timu yake ya Boys II Men, walipoingia tuu madarakani, akafanya study tour ya tulioanza nao kwanini wao wamefanikiwa, wako mbali na sisi wametuacha nyuma sana!, akagundua wali invest kwenye elimu!. Akarudi akahamasisha kila kata iwe na shule ya sekondari ili kila Mtanzania apate kwanza elimu, mengine yote, yatafuatia!.

Baada ya kujiuzulu, serikali ya JK ikazi abandon zile shule za EL ili kumkomoa!. Jana alipozungumzia umuhimu wa kuwaelimisha kwanza watu wetu, amenigusa sana!. Tungekuwa tumeelimika, tusingeibiwa hivi madini yetu, tumeibiwa madini kwa sababu hatuna elimu ya madini, sasa tumegundua gesi,serikali inakimbilia kugawa vitalu kwa umiliki wa miaka 99 huku Watanzania hatuna hili wala lile kuhusu elimu ya gesi, kwa kifupi, hutujui lolote na tutaishia kuibiwa tena gesi yetu kwa kukosa elimu ya gesi!. EL ameshauri, lets invest kwenye elimu kwanza ili kuwa empower watu wetu kielimu ndipo tuingie kwenye ambitious projects kama za kilimo kwanza gesi etc!.

Kwa hili pekee, CCM ikimsimamisha EL, Tanzania itapata ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania!.

Nimesema, CCM ikimsimamisha EL, 2015, itakuwa ni CCM tena, kwa sababu katika wapinzani wote, hakuna hata mgombea mmoja anayewa kusimama na Lowassa kwenye urais na bado akaambulia kura!, there is none, no one!.

Mwenye masikio na asikie!.

2. Dhambi Kubwa ya Lowassa ni Richmond Tuu!.

Najua wapinzani wa dhana ya ukweli, watakuja na hoja za dhambi kubwa ya Lowassa ni Richmond!, then time will tell, hiyo ni mizigo tuu ya watu, alijitolea kuibeba ili kwa kuteswa kwake, wao waokoke, wakati muafaka ukifika, hili litawekwa wazi na Watanzania mtawafahamu wenye zigo lao!. Wenye akili wameshang'amua ile metarmophosis process from Richmond -Dowans -Simbion na kwa msio jua, mkae mkijua Tanesco bado inailipa Simbion capacity charge ile ile ya dola 152 kama Richmond na Dowans, hivyo tumeruka majivu na kukanyaga moto, tumeruka maji na kukanyaga tope, na kwa usafi tumeruka nyasi, tukakanyaga ma..!.

3. CCM Haina zaidi ya EL na Upinzani hana wa Kushindana Nae!.

Wanabodi ni mimi niliwahi kusema, CCM imechokwa na Chadema Haijajipanga, baadae nikasema CCM imechokwa mpaka basi!, Baada ya Chadema kuanza kujipanga nikasema Chadema, Njia Nyeupe Ikulu, lakini sasa baada ya kumsikia Edward Lowassa, kama ni kweli CCM itamsimamisha, then, 2015, ni CCM tena, kinyume cha hapo, CCM ikimsimamisha mwingine yoyote, 2015, Chadema inachukuwa nchi kiulaini kama kumsukuma mlevi!.


Mwisho.

Namalizia kwa swali moja tuu, Jee CCM inaujasiri wa kuukubali huu ukweli mchungu wa kumsimamisha Edward Lowassa ili kuweza kujiokoa? au itaendeleza kiburi uongozi na jeuri ya uchama tawala kusubiria kifo cha mende huki inajiangalia kwa kutegemea itaendeleza uking'ang'anizi wake kwa kuamini this time pia itashinda tena kwa kuutumia uwongo ule ule, na mbinu zile zile za uchakachuaji ule ule, kwa kutegemea katiba mpya ita provide opportunities za aina ile ile ya miaka ya nyuma, kuwa ita endelea "to fool all the people all the times?!.

Asante.

Pasco.

NB. Japo Pasco wa JF sio mwanachama wa Chama chochote cha siasa, kwa CCM ni Pro Lowassa, kwa Chadema ni Pro ZZK na kwa CUF ni Pro-Jussa!.

Umefikishwa wapi? mwandishi wa habari huwa haongei udaku, ongea ujulikane unachokisema, una maana Lowassa asingestaafu?
 
Mkuu wacha kubabaika na huyo fisadi, kama amekutuma kampigia debe basi ameisha shindwa kabla mbio hazijaanza!!! Kama CCM watamweka huyo kama mgombea basi kazi ya CHADEMA itakuwa nyepesi saana, pole ndugu yangu huyo hauziki!!!

Chadema hawana mgombea mpaka sasa. Mwenyekiti alishabwagwa vibaya sana na Kikwete mpaka raundi ya pili akashindwa kuingia ulingoni.

Slaa aliyepokea kijiti nae akabwagwa ikabaki gwandaz wanasusa-susa. Sasa ni nani wakusimama na Lowassa chadema? Labda mumsimamishe Leticia Nyerere.
 
Wana JF, Sasa yupi bora kati ya Mtu mwema na mwadilifu, asiyejua kuchukua cha mtu lakini hawezi kukemea wezi wa mali ya umma wanaoiba mchana kweupe na vingine wanadodndoshea miguuni pake na wala aiyewezi kupanga wala kusimamia mkakati ya maendeleo na mtu mwingine tunayesema ni mwizi lakini anauwezo wa kupanga na kusimamia mipango ya maendeleo lkn wizi wake ana-invest humu humu nchini??? niambieni yupi bora?????? KURA YANGU NAMPA EL
 
Three sides of the story, it is only the truth that pulls towards the center with some centripetal force.
 
Umefikishwa wapi? mwandishi wa habari huwa haongei udaku, ongea ujulikane unachokisema, una maana Lowassa asingestaafu?
Mkuu Zomba, nilipokuwa nakusoma nilikudhania wewe ni mwelewa!. Ina maana mpaka leo bado hujaelewa sababu za kujiuzulu kwa EL?!. Hivi hujanote jinsi serikali ya JK ilivyo pwaya baada ka kujiuzulu huyu jamaa?. Hivi hujui yeye ndiye mkombozi pekee anayeweza kuunusuru CCM 2015, vinginevyo CCM ikimsimamisha mwingine yeyote, 2015, Chadema inachukua nchi kiulaini kama kumsukumiza mlevi?.
 
Wana JF, Sasa yupi bora kati ya Mtu mwema na mwadilifu, asiyejua kuchukua cha mtu lakini hawezi kukemea wezi wa mali ya umma wanaoiba mchana kweupe na vingine wanadodndoshea miguuni pake na wala aiyewezi kupanga wala kusimamia mkakati ya maendeleo na mtu mwingine tunayesema ni mwizi lakini anauwezo wa kupanga na kusimamia mipango ya maendeleo lkn wizi wake ana-invest humu humu nchini??? niambieni yupi bora?????? KURA YANGU NAMPA EL
Mkuu Fugwe, baeleze baelewe!.
 
Mkuu Pasco ni kweli Laigwanani ni mchapakazi kama angekuwa bado yuko serekalini hata hili deni la RICHMOND lisingelipwa ha ha ha ha.

Mkuu Zomba, nilipokuwa nakusoma nilikudhania wewe ni mwelewa!. Ina maana mpaka leo bado hujaelewa sababu za kujiuzulu kwa EL?!. Hivi hujanote jinsi serikali ya JK ilivyo pwaya baada ka kujiuzulu huyu jamaa?. Hivi hujui yeye ndiye mkombozi pekee anayeweza kuunusuru CCM 2015, vinginevyo CCM ikimsimamisha mwingine yeyote, 2015, Chadema inachukua nchi kiulaini kama kumsukumiza mlevi?.
 
Last edited by a moderator:
Utasemaje hivyo wakati kina Kiranga wameonyesha udhaifu wa siasa za kujadili watu badala ya itikadi kitambo tu?

Utasemaje hivyo wakati watu tushaongea humu kwamba the very label "Ujamaa na Kujitegemea" carries within itself an inherent oxymoronic contradiction if at all you value the individual as the well and litmus test of ideologies?

Upo sahihi Mkuu,
Nilitamka hayo kwa sababu nimeona kuna mwenendo wa wachangiaji wengi humu kukimbilia threads zinazojadili watu badala ya masuala, lakini ni dhahiri wapo wengine wengi ambao hawapo katika kundi hilo, wewe ukiwa mmoja wapo kwani nimekuwa nakusoma sana;

Unakuta mtu anakuja na thread ya mgombea kipenzi chake na kuanza kutulazimisha kwamba hawezekaniki kwa hoja za ovyo ovyo tu na zilizojaa ushabiki na ubabe kwa sababu wanayo dola kwa hivi sasa badala ya kujenga hoja za msingi kwani pengine hilo lingeweza kushawishi watu wengi waunge mkono hoja hizo au wagombea wao lakini badala yake wanazidi kuwaharibia aidha kwa kujua au kutojua; Na cha kushangaza zaidi, unakuta watu zaidi ya mia wakishiriki mijadala ya ovyo kama hiyo ambayo literally inawapa more room waleta hoja za ovyo ovyo kama kuzidi kutuambukiza siasa za WATU vis-a-vis MASUALA, siasa ambazo wao wamekuwa ni mabingwa hasa kwa kuchafua wenzao; Vinginevyo kuna mijadala mingi sana muhimu kwa taifa letu kama vile ya katiba mpya, muungano n.k, lakini unakuta ushiriki wa watu katika mijadala ya namna hii sio ya kurudisha;

Ni hayo tu mkuu lakini ujumbe wako nina hakika wengi wanauelewa;
 
Mkuu Pasco ni kweli Laigwanani ni mchapakazi kama angekuwa bado yuko serekalini hata hili deni la RICHMOND lisingelipwa ha ha ha ha.
Mkuu Ngongo, sio tuu lisingelipwa mkataba tungevunja na mitambo tungetsifisha!. Hiyo capacity charge tuu tunayowalipa, ilishatosha zamani kununua mitambo mipya, wala kusingekuwepo na hii Simbion!. Tatizo mhusika mkuu ni muzeiye na ndivyo walivyokubaliana kwenye secret code yao! "Scratch my back, I'll scratch yours!". The only thing that will stop him is his ill heathy na atahamishia majeshi yake kwa Membe.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Zomba, nilipokuwa nakusoma nilikudhania wewe ni mwelewa!. Ina maana mpaka leo bado hujaelewa sababu za kujiuzulu kwa EL?!. Hivi hujanote jinsi serikali ya JK ilivyo pwaya baada ka kujiuzulu huyu jamaa?. Hivi hujui yeye ndiye mkombozi pekee anayeweza kuunusuru CCM 2015, vinginevyo CCM ikimsimamisha mwingine yeyote, 2015, Chadema inachukua nchi kiulaini kama kumsukumiza mlevi?.

Tafadhali, achana na uelewa wangu binafsi, uelewa wangu ni mdogo sana lakini mimi singoji wala sipokei kibahasha.

Lowassa hana ukombozi kwa CCM, Lowassa ana harakati za kujikombowa yeye mwenyewe kwa sasa, na natumai atakuwa kisha jiweka sawa ifikapo 2014, kama afya haitamtatiza zaidi, kwani nahisi ana Parkinson disease kutokana na muonekano wake.

Mtazamo wangu ni kuwa Lowassa hana upinzani Chadema ikiwa atagombea. Kama unataka tuongee uwezo wa Lowassa ndani ya CCM, hiyo ni mada nyingine kabisa na hapa si mahala pake. Jee, unaweza kufunguwa nyuzi tumjadili Lowassa ndani ya CCM? kama huwezi tafadhali sana tena sana, Lowassa was made into being na Kikwete. Kikwete humjui ipasavyo na hawa watu hawajakutana mitaani, unataka tuanze kuchambuwa wamekutana wapi na ilikuwaje? funguwa nyuzi.

Jee, ni nani ndani ya chadema wa kuchuana na Lowassa akiamuwa kugombea Urais?
 
Upo sahihi Mkuu,
Nilitamka hayo kwa sababu nimeona kuna mwenendo wa wachangiaji wengi humu kukimbilia threads zinazojadili watu badala ya masuala, lakini ni dhahiri wapo wengine wengi ambao hawapo katika kundi hilo, wewe ukiwa mmoja wapo kwani nimekuwa nakusoma sana;

Unakuta mtu anakuja na thread ya mgombea kipenzi chake na kuanza kutulazimisha kwamba hawezekaniki kwa hoja za ovyo ovyo tu na zilizojaa ushabiki na ubabe kwa sababu wanayo dola kwa hivi sasa badala ya kujenga hoja za msingi kwani pengine hilo lingeweza kushawishi watu wengi waunge mkono hoja hizo au wagombea wao lakini badala yake wanazidi kuwaharibia aidha kwa kujua au kutojua; Na cha kushangaza zaidi, unakuta watu zaidi ya mia wakishiriki mijadala ya ovyo kama hiyo ambayo literally inawapa more room waleta hoja za ovyo ovyo kama kuzidi kutuambukiza siasa za WATU vis-a-vis MASUALA, siasa ambazo wao wamekuwa ni mabingwa hasa kwa kuchafua wenzao; Vinginevyo kuna mijadala mingi sana muhimu kwa taifa letu kama vile ya katiba mpya, muungano n.k, lakini unakuta ushiriki wa watu katika mijadala ya namna hii sio ya kurudisha;

Ni hayo tu mkuu lakini ujumbe wako nina hakika wengi wanauelewa;
Mkuu Mchambuzi, with due respect,
kwani Watanzania huwa wanachagua nini?. Wanachagua sera, hoja au mtu?. Kwani JK alichaguliwa kwa lipi?. Ninachofanya mimi ni kuwapa mwanga wa kitakachotokea 2015, Watanzania hawachagui sera wala hawasikilizi hoja, wao wanachagua mtu tena kwa kumuangalia sura!.

Nilipokuwa mtaani nilidhani wasomaji wakuu wa magazeti pendwa ni wale std 7 na school drop outs, nilipokuwa UD sikuamini magazeti hayo ndio choice no. 1 kwa wanafunzi wa chuo sasa nimeichukulia hiyo ndio sampling ya Watanzania!.

Kwa sisi waandishi big names makes big news, EL ndie the biggest name in Tanzania politics akisimama, hakuna wa kusimama nae!.

Japo jf is ment to be the home of great thinkers ambao wana discuss ideas, ordinary mind pia wapo wanao discuss events na sisi simple mind pia tupo ambao tuna discuss people!.

Great minds, ordinary minds na simple minds all together tukubali tukatae the name EL is the determinant factor nani anakuwa the next president wa nchi yetu come 2015!.

Wenzetu ma great thinkers endeleeni kupandisha threads za ideas, huku ma ordinary wakiendelea kutuhabarisha trends of events na sisi ma simple minds tukiendelea kuwatajieni watu posible wa kuchukua nchi 2015!.

Pasco.
 
Pasco.
Tulipopata uhuru miaka ya 60, maadui wetu wakuu watatu, walikuwa ni Elimu, Umasikini na Maradhi, na tulijiwekea misingi yetu mikuu minne ya maendeleo kuwa ili tuendelee, tulihitaji vitu vinne: Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora!. Kwenye hiyo misingi, tulisema Pesa sio msingi, pesa ni matokeo!, hili ndilol lililokuwa kosa pekee la Mwalimu, kutofautiana na misingi ya ukweli ya uchumi, kama ilivyofundishwa na Adam Smith (land, labor, capital na interpreneureship)!. Kwenye ile mising minne tulisahau capital!.

Mimi huwa natatizwa sana na fikra za kufikiria Ukombozi wa Mtanzania kwa kufuata vitabu vya wale walonacho wanatazama nini..Huwezi kusema kosa pekee la Nyerere lilikuwa kutofuata misingi ya ukweli kwa sababu Adam Smith kasema haya wakati hailingani na mazingira wala Mantiki ya Mtanzania. Hivi kweli wewe unategemea mtu maskini, Mjinga na mwenye maradhi ataweza vipi kuzungumzia CAPITAL ikiwa hata kula yake mwenyewe ni shida.. Au nambie yule ombaomba unayemuona Mtaani unaweza vipi kumshauri ili atoke ktk Umaskini wa kutembea na kopo maana ukisema atafute Capital utakuwa unamtukana.

Mawazo ya kina Lowassa hayana Tofauti na JK kuhusu Capital na fedha kuwa msingi wa maendeleo... Kwa maskini hii kufanya Umalaya tu kwa sababu tunachokitaka ni zaidi ya uwezo wetu maana hatuna fedha. Mtaji wa maskini siku zote ni nguvu zake nakama tutafikiria nje ya nguvu hizi ambazo zinatokana na UTU wetu sidhani kama tutafika popote hata kama akija Obama kutawala. Ninachoweza mnimi kushauri tu ni kuitazaa tuna uwezo gani sisi wenyewe na maadam sio walemavu inatakiwa tutupe magongo na miwani ya kuficha upofu wetu maana hatuna upofu huo isipokuwa Ujinga. Vita ya kuondoa Umaskini, Ujinga na Maradhi ni vta tofatui kabisa na vita ya kupata Maendeleo.

Pengine niseme tafsiri ya hili neno MAENDELEO ndipo penye tofauti kubwa kati ya maskini na tajiri. I mean tazama nchi zao utakuwa only 3 to 5% ya population yao wapo engaged na Primary economic activities na hao hao kina Adam Smith wanajienga kama ni 'agriculture, (both subsistence and commercial), mining, forestry, farming, grazing, hunting and gathering, fishing, and quarrying. The packaging and processing of the raw material associated with this sector is also considered to be part of primary economic sector. Wakati sisi unakuta zaidi ya asilimia 80 wapo ktk primary sectors. Haya nambie tutafikiri vipi sawa na kina Adam Smith.. wao hiyo asilimia 3 tu ya nguvu kazi inaweza kutosheleza mahitaji ya ngazi zingine zote za kiuchumi sisi pamoja na kuwa na asilimia 80 tunashindwa hata kutosheleza viwanda...

Ndio maana tulimsikia Nyerere akisisitiza sana kuzingatia MAHITAJI yetu muhimu kama maskini badala ya kuota Utajiri kana kwamba Maendeleo ni kamari au lotto. Anachfanya EL ni kutupa ndoto tu ya utajiri kama unavyowez akumuahidi ombaomba sadaka ya kila jumapili. Katika uchumi kuna misingi yake nakaa haifuatwi basi nchi hiyo haiwezi kuendelea hata siku moja. Kuna Primary, Secondary (viwanda na Ujenzi), Tertiary (services), Quaternary na Quinary..

Na hao wenzetu walivyokwisha tuacha utakuta hesabu kubwa ya nguvukazi au waajiriwa wapo ktk Tertiary karibu sawa na ajira za sisi ktk Primary na bado tunashindwa kuzalisha ku feed viwanda na ujenzi. Tumeingia ktk Huduma -services pasipo mkuwa ma malighafi kutoka chini isipokluwa kuhudumia mashika ya nje.. Hivi kweli mnafikiri tutatoka kweli halafu tunamtaka EL atuongoze ktk ndoto hii ya kuwapatia vijana ajira za ulanguzi na Udalali.
- Ama kweli tumekwisha!
 
Mkuu Mchambuzi, with due respect,

kwani Watanzania huwa wanachagua nini?. Wanachagua sera, hoja au mtu?. Kwani JK alichaguliwa kwa lipi?. Ninachofanya mimi ni kuwapa mwanga wa kitakachotokea 2015, Watanzania hawachagui sera wala hawasikilizi hoja, wao wanachagua mtu tena kwa kumuangalia sura!.

Nilipokuwa mtaani nilidhani wasomaji wakuu wa magazeti pendwa ni wale std 7 na school drop outs, nilipokuwa UD sikuamini magazeti hayo ndio choice no. 1 kwa wanafunzi wa chuo sasa nimeichukulia hiyo ndio sampling ya Watanzania!.

Kwa sisi waandishi big names makes big news, EL ndie the biggest name in Tanzania politics akisimama, hakuna wa kusimama nae!.

Japo jf is ment to be the home of great thinkers ambao wana discuss ideas, ordinary mind pia wapo wanao discuss events na sisi simple mind pia tupo ambao tuna discuss people!.

Great minds, ordinary minds na simple minds all together tukubali tukatae the name EL is the determinant factor nani anakuwa the next president wa nchi yetu come 2015!.

Wenzetu ma great thinkers endeleeni kupandisha threads za ideas, huku ma ordinary wakiendelea kutuhabarisha trends of events na sisi ma simple minds tukiendelea kuwatajieni watu posible wa kuchukua nchi 2015!. Pasco.



Mkuu Pasco,

Nashukuru kwa majibu yako. Naomba nianze kwa kusema kwamba: Nina uhakika wa karibia asilimia mia moja kwamba Founders wa JamiiForums walipokuja na wazo la kuanzisha mtandao huu wa kijamii miaka sita iliyopita, THEY ENVISIONED (among other things), to develop an intellectual body which would serve AS A MIRROR THAT PROVIDES OUR SOCIETY WITH ITS OWN IMAGE. Bila shaka, Founders wa Jamii Forums watakubaliana na mimi kwamba katika vitu walivyotegemea ni kwamba makundi ya watanzania wenye professions au wanaofanya shughuli ndani ya professions mbalimbali kama vile - Lawyers, Economists, Scientists, JOURNALISTS n.k, wangejiunga na mtandao huu na kuja kutueleza watanzania, JE: HOW DO WE LOOK AS A SOCIETY – Are we Handsome? Are We Ugly? Are we Corrupt, Are we Uncivilized…?

Mkuu Pasco, kwa maelezo yako hapo juu, hata kama utaendelea kukataa, you definitely belong to the Intellectual body ambayo Founders wa huu mtandao walikuwa wanawalenga, contrary to that, Utakuwa UNAKIMBIA KIVULI CHAKO MWENYEWE, kwani kwa nafasi yako as a Professional journalist (kwani naamini wewe sio journalist wa kuunga unga), You are supposed to articulate hopes and fears za watanzania; you are supposed to warn watanzania of the IMPENDINF DANGERS and parade them into action;

Mkuu Pasco, Party politics by default ni partisan politics; zina akisi na kukidhi only partial interest za jamii, kwani zaidi zina akisi, zinakidhi na vile vile zinaitikia expediency of power; Partisan politics zina muda mdogo sana to reflect over larger and more important social issues katika nchi yetu; Na hapa ndipo viongozi kama Dr. W.P Slaa wanaibuka na points wanaposema kwamba Chadema kwa kawaida hakijadili WATU BALI MASUALA; Pamoja na ukweli kwamba ni vigumu kwa Chadema kufanikisha hili in Practice, lakini suala muhimu hapa ni NIA ambayo hakuna kiongozi wa CCM aliyewahi kuionyesha katika nyakati hizi;

Mkuu Pasco, katika nyakati hizi ambapo sisi kama Watanzania bado hatujapata a firm direction ya wapi tunataka kwenda kimaendeleo (kijamii na kiuchumi) na bado hatuna dira inayotambulika kitaifa, na inayo inspire watanzania, tukiendeleza utamaduni huu wa ku-over play partisan politics in the midst of hali mbaya na za kusikitisha among watanzania walio wengi, hasa utamaduni wa kuegemea zaidi kujadili WATU (WAGOMBEA) badala ya MASUALA muhimu kwa taifa ambayo ndio inatakiwa tuyajengee hoja kisha tuyatafutie WATU wa kuyasimamia na kutekeleza, kufanya kinyume ya haya ni kujijengea mazingira ya kupata madhara makubwa sana siku za usoni.

Mkuu Paso, kwa mtazamo wangu ambao pengine utauona ni finyu sana, tunahitaji the kind of bodies and institutions ambazo zita raise above partisan politics na kujihusisha zaidi na larger and more important social and national issues ambazo tukishafikia muafaka kama taifa kwamba ni zipi tuzipe kipaumbele, then ndio mchakato wa ku-scrutinize wagombea kwa kuwapima wanasimamia wapi katika ndoto zenu, matakwa yetu, matarajio yetu n.k, ndio ufuate. Mimi ninadhania kwa asilimia kubwa sana, founders wa Jamiiforums walilenga kutengeneza mazingira ya namna hii;

Mkuu Pasco, watanzania wanategemea intellectuals kama wewe kuwasaidia TO GIVE MEANING TO & READ MEANING INTO, WHAT MAY LOOK LIKE THE OBVIOUS (kwa mfano imani kwamba Lowassa hana mshindani); watanzania wanakutegemea mkuu Pasco kuwapa meaning to and read meaning into things that are perceived to be ‘Unobjectionable' (e.g. mtu akisimamishwa tu kuwa mgombea wa CCM, yeye ndiye rais wa Tanzania) and Mundane (routine) [kwa mfano CCM haiwezi kushindwa uchaguzi Tanzania); Mkuu Pasco, hili ni muhimu zaidi: Whereas Wanasiasa PRETEND TO THINK FOR THE SOCIETY, INTELLECTUALS (including wewe mkuu) HAVE A DUTY TO HELP THE SOCIETY THINK FOR ITSELF!

Mkuu Pasco, given this critical role ya intellectuals kwenye jamii, ndio maana sio ajabu kwa viongozi wengi wa chama tawala na serikali yake kuchukia independent and critical thinkers – kwa mfano critical Economists, critical Lawyers (kama Issa Shivji), critical journalists (kama Samson Mwigamba, Jenerali Ulimwengu, Saed Kubenea) na wengine wengi; Mkuu Pasco, ukijikuta upo upande tofauti na hawa katika siasa za Tanzania, basi your intellectual capacity has to be questioned, ingawa kukimbia kivuli chako kidogo inatoa taswira juu ya nini kinaendelea;

Mwisho naomba nimalizie kwa kusema kwamba Siasa za kumuunga Mkono Lowassa for CCM, Zitto for Chadema na Jusa for CUF kwa uchaguzi wa 2015 zinapwaya kwani zipo BIASED, SELF - OPINIONATED & SUBJECTIVE. Yote haya ni contrary to maadili ya Journalism as a profession. Vile vile hoja za namna hii hazitoshi kutuaminisha kwamba Pasco sio mwanachama wa chama chochote cha siasa na badala yake tunazidi kuamini kwamba wagombea wote hawa watatu wana mahusiano maalum kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015; Kwa vile ni wewe ndio umekuwa unawaunganisha kwa ustadi mkubwa, ni wajibu wako kutuaminisha vinginevyo.
 
Ningeomba nilisemee suala la CAPITAL kidogo:

Historia ina tabia moja ya ajabu sana: KUJIRUDIA. Mara tu baada ya uhuru, tulielezwa kwamba sisi ni nchi maskini kwa sababu WE LACK CAPITAL. Tukaambiwa kwamba tulikuwa na nguvu kazi ya kutosha (labour), lakini ili tuendelee, WE MUST invite and import FOREIGN CAPITAL. Ili kukafinisha hili, LAZIMA tuweke mazingira ya kutoa incentives – kama vile tax holidays, easy repatriation of profits, restrict labor laws ili kuweka hali ya nidhamu viwandani n.k. Ili kukidhi hili, TANU mwaka 1962 ikapitisha Sheria iitwayo: Foreigh Investments (Protection) Act ya mwaka 1962, na vile vile sheria mbalimbali juu ya trade unions na zile dhidi ya migomo ya wafanyakazi zikapitishwa.

Pamoja na yote haya, Foreign Investment haikuja kama ilivyotegemewa, badala yake CAPITAL FLIGHT WAS THE ORDER OF THE DAY. By the time Azimio la Arusha linaingia, FOREIGN INVESTMENT ilikuwa imeingia kidogo sana Tanzania. Cha kustaajabisha ni kwamba, ni baada ya AZIMIO LA ARUSHA ndipo Foreign Capital ikaanza kuingia kwa wingi sana.

Kipindi cha 1960s-1970s, tulikuwa tunajaribu sera za industrialization za import substitution kwa kiasi kikubwa, na export orientation kwa kiasi kidogo, kwa kutumia STATE CAPITAL, kiasi kidogo sana cha LOCAL PRIVATE CAPITAL huku kiasi kikubwa zaidi kikiwa ni FOREIGN CAPITAL. Suala muhimu kulitazama hapa ni kwamba: In the process, viwanda vingi (hasa mass goods industries) kama vile vya nguo, oil na ngozi vilianzishwa kwa mafanikio makubwa sana. Hivi vilikuwa ni viwanda ambavyo VILITUMIA ZAIDI LOCAL CAPITAL kuliko FOREIGN CAPITAL.

Kuanzia miaka ya 1980s tukaanza shuhudia Liberalization, Privatization & Marketization vikiingia kwa kasi ya ajabu chini ya IMF na World Bank, and this marked the beginning of the process of DE-INDUSTRILIZATION IN TANZANIA. Cha ajabu ni kwamba: Vile viwanda that were more useful to our economy, na ambavyo tulivijenga kwa more local capital kuliko foreign capital – Textiles, Leather, Oil and food processing industries were the ones HIT THE HARDEST.

Kwa kweli, kama nilivyosema awali, historia ina tabia moja ya ajabu sana: KUJIRUDIA. George Kahama alikuwa mkuu wa kwanza na NDC – iliyopewa jukuku TO PARASTATALIZE OUR ECONOMY - uanzishwaji wa viwanda vyetu baada ya uhuru wakati wa Ujamaa; Na ni George Kahama huyu huyu akaja kuwa Mkuu wa Kwanza wa Investment Promotion Centre in the 1990s (leo hii inaitwa TIC), iliyopewa jukumu to DE-PARASTATALIZE OUR ECONOMY.

Kuna kila dalili kwamba when it comes to CAPITAL, KUNA HAKI YA MUNGU na HAKI YA MZUNGU kwani definitely Mungu ametujalia na kutupa haki katika maeneo mengi sana ya kimtaji - (Madini, Gesi, Ardhi, Misitu, Rasilimali Watu n.k), lakini tunaaminishwa hata na watawala wetu wanaowapapatikia WAZUNGU kwamba sisi hatuna uwezo wa ku exploit such CAPITAL kwa manufaa yetu, na badala yake Mzungu ndiye mwenye uwezo huo. Lakini katika hili, historia haijirudii kwani hatujaona popote pale ikisema kwamba MZUNGU aliendelezwa na jamii nyingine.

Kinachojirudia ni 'CAPITAL FLIGHT' kama ilivyokuwa kabla ya azimio la Arusha, at the expense of Mtanzania kuzidi kudidimia. Haya ni moja ya MASUALA ambayo WATU tunaowataka watuongoze 2015 lazima wwe na majibu yasio ya kumumunya, hasa katika kutueleza watayafanyia kazi kwa namna gani. Ndio maana nazidi kuhimiza, hata nikichukiwa kiasi gani kwamba - mijadala ya MASUALA vis-a-vis WATU ni muhimu zaidi katika nyakazi hizi kuliko the other way round; Vinginevyo, kama Mwalimu alivyosema, IKULU NI MZIGO, kwani hata kwenye suala hili dogo tu nililojadili hapa, ni wazi kwamba Urais wa nchi hii ni kazi nzito sana, ni kazi ya kuogopwa na kila mgombea, hasa kama hajajipanga na majibu YA KWELI kwa maswali mengi ya watanzania waishio vijijini (zaidi ya 70% ya watanzania);
 
Hakuna kazi ngumu kama kumkampenia EL, Pasco you are on MISSION IMPOSSIBLE

attachment.php

Loading..!
 
Hakuna anayebisha kuhusu "WANATOKEA", kilicho relevant katika discussion yangu ni Wanaoishi kule kama wapiga kura; Vinginevyo KUTOKEA sehemu sio kigezo, kwani wapo watu ambao wanajua wametokea kwenye matumbo ya mama zao lakini hawana heshima kwa wanawake, wengine hata mama zao wazazi;

Hata wapiga kura wakubwa ndio hao-hao wa vijijini, hauna sababu ya kuwaona kuwa wako inferior.
 
Mkuu Pasco, tuko pamoja niwekee siti kwenye basi hili, na ukitangulia usitusahasie wa mikoani.

1.lowassa+by+g.sengo+17.jpg
 
Back
Top Bottom