Elections 2015 Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa...

Tumekusikia ndugu kuwa wewe humtaki Lowassa. Tueleze wewe unadhani ni nani akipitishwa na CCM itapata ushindi wa kishindo.

January Makamba

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Hakuna yeyote atakayepitishwa aifanye CDM ishindwe.Bora muweke hata kunguni agombanie.......
 
ah mbona wasiwasi umewaingia ghafla? kwani 2015 uchakachuaji hakuna? au waimanisha hata mkichakachua kura hazitatosha?
 
Mwigulu Nchemba atakuwa mgombea urais wa ccm.

Akishinda Musa Tesha atakuwa IGP

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
hahahaaa. we ni mfuasi wa chama cha wazinzi na wasagaji nini!

Ndiyo kipi hicho ambacho TISS na polisi wanakiangalia tu na msajili wa vyama hajakifuta? Jamani nisaidieni. Which party is this?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Walishakubaliana tangu kikwete hajaingia madarakani,wamwaachie Kikwete aanze,Lowasa atachukua baada yake,Lowasa tatizo tu ni fisadi ndicho kinachochafua CV yake,ila ni mchapa kazi sana,kitu kingine ana share Voda,ila urais akiupata ni hela nyingi katumia kununua urais wake na atakuwa rais wa kwanza kununua nafasi ya Ikulu kwa Tanzania yetu,
 
Ukisema kuwa CCM ikimsimamisha LOWASSA 2015 itakuwa rahisi CDM kushinda eti kwa vile Lowassa ni Fisadi,sio kweli.
CHADEMA itashinda kwa kuwa Watanzania wamechoka na CCM kwa kuwa imepewa ridhaa ya kuongoza kwa zaidi ya miaka 50 lakini hadi leo huduma muhimu za kijamii km Maji,barabara,Afya na Elimu imekuwa km Hadisi pamoja na rasilimali nyingi tulizo nazo!

Lakini sio hivyo tu! Ndani ya CCM hakuna alie msafi.ukingangana kusema Lowassa ni Fisadi,ni kutaka kutudanganya ili tumsaidie NAPE na kundi lake kutimiza malengo yao ya kisiasa ya kutaka kumtoa Lowassa KAFARA ili kuiponya CCM ambayo ipo mahututi huku ikingojea kuzikwa 2015 ktk kaburi la Sahau.
 
nchi hiii lazima iongozwe na chadema 2015 - 2020 hata asimame ndani ya ccm,,,, labda mungu, lakn binadam yeyote akisimama ndani ya ccm nachagua jiwe:love:chadema the rulling part of united republic of tanzania:A S-fire1::A S-fire1::A S-fire1:

labda nchi ya uchaggani lakini sio tanzania.. Nitakubali kupoetza kila nilichonacho ili machadema yasikaribie ikulu
 
Edward ngoyaye lowassa namfananisha na jamaa mmoja aliyekuwa na ukimwi huku akiwa na utajiri wa kutosha. Jamaa huyu baada ya kujijua kuwa ameathirika, alijitahidi kutumia nguvu za kifedha na kuwahonga wanawake wengi huku akiwaambukiza ukimwi. Walipokuja kushtuka walikuwa tayari ameisha waunganisha kwenye mtadao. Ukisha nasa hutoki.
Huu ndiyo utaratibu wa edward lowassa, ametumia fedha zake ambazo sijui anazipata wapi na kuwahonga viongozi wa dini, vijana na makundi mbalimbali ya kijamii. Lengo tinalijua anataka urais, lakini akisha pata kila mtu atatambua kuwa alikuwa ameathirika sasa ni kila mtu kusubiria kifo. Akisha ingia ikulu watanzania mtaelewa hatari ya kukukutana na mbogo aliyejeruhiwa, visasi vitatawala na ufisadi ndipo utakapochanua maua yake na kila mtu atatambua.
 
Mkuu Pasco hata mimi nakuunga mkono kwa hizo hoja zako zenye mashiko na kweli tupu kwa mtanzania mwenye uchungu na mpenda maendeleo.

Unajua huyu bwana Lowasa vision yake katika suala la elimu ilikuwa nzuri sana, mwanzo alikuja na suala la kujenga shule nyingi za kata. Baadae alikuwa na lengo la kutatua shida ya walimu kwa kuwa majengo ya madarasa, nyumba za walimu na maabara tungelikuwa tumeshakamilisha kuvijenga.

Unajua hapa kinachowasumbua watu wengi kwa kukosa imani na huyu bwana Lowasa ni ile issue ya RICHMOND tu. Kwenye hili la Richmond hapa ni kama alitolewa kafara tu ili serikali isianguke. Na kwa kuwa huyu bwana ni mzalendo na mtiifu kwa serikali yake basi alikubali kutolewa kafara ili ainusuru serikali ya CCM.

Shime watanzania wapenda maendeleo tumpe nafasi huyu bwana Lowasa atufanyie hayo tunayoyaota kila kukicha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…