Elections 2015 Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa...

Elections 2015 Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa...

Tumekusikia ndugu kuwa wewe humtaki Lowassa. Tueleze wewe unadhani ni nani akipitishwa na CCM itapata ushindi wa kishindo.

January Makamba

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Hakuna yeyote atakayepitishwa aifanye CDM ishindwe.Bora muweke hata kunguni agombanie.......
 
ah mbona wasiwasi umewaingia ghafla? kwani 2015 uchakachuaji hakuna? au waimanisha hata mkichakachua kura hazitatosha?
 
Mwigulu Nchemba atakuwa mgombea urais wa ccm.

Akishinda Musa Tesha atakuwa IGP

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
hahahaaa. we ni mfuasi wa chama cha wazinzi na wasagaji nini!

Ndiyo kipi hicho ambacho TISS na polisi wanakiangalia tu na msajili wa vyama hajakifuta? Jamani nisaidieni. Which party is this?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Walishakubaliana tangu kikwete hajaingia madarakani,wamwaachie Kikwete aanze,Lowasa atachukua baada yake,Lowasa tatizo tu ni fisadi ndicho kinachochafua CV yake,ila ni mchapa kazi sana,kitu kingine ana share Voda,ila urais akiupata ni hela nyingi katumia kununua urais wake na atakuwa rais wa kwanza kununua nafasi ya Ikulu kwa Tanzania yetu,
 
Ukisema kuwa CCM ikimsimamisha LOWASSA 2015 itakuwa rahisi CDM kushinda eti kwa vile Lowassa ni Fisadi,sio kweli.
CHADEMA itashinda kwa kuwa Watanzania wamechoka na CCM kwa kuwa imepewa ridhaa ya kuongoza kwa zaidi ya miaka 50 lakini hadi leo huduma muhimu za kijamii km Maji,barabara,Afya na Elimu imekuwa km Hadisi pamoja na rasilimali nyingi tulizo nazo!

Lakini sio hivyo tu! Ndani ya CCM hakuna alie msafi.ukingangana kusema Lowassa ni Fisadi,ni kutaka kutudanganya ili tumsaidie NAPE na kundi lake kutimiza malengo yao ya kisiasa ya kutaka kumtoa Lowassa KAFARA ili kuiponya CCM ambayo ipo mahututi huku ikingojea kuzikwa 2015 ktk kaburi la Sahau.
 
Ukisema kuwa CCM ikimsimamisha LOWASSA 2015 itakuwa rahisi CDM kushinda eti kwa vile Lowassa ni Fisadi,sio kweli.
CHADEMA itashinda kwa kuwa Watanzania wamechoka na CCM kwa kuwa imepewa ridhaa ya kuongoza kwa zaidi ya miaka 50 lakini hadi leo huduma muhimu za kijamii km Maji,barabara,Afya na Elimu imekuwa km Hadisi pamoja na rasilimali nyingi tulizo nazo!

Lakini sio hivyo tu! Ndani ya CCM hakuna alie msafi.ukingangana kusema Lowassa ni Fisadi,ni kutaka kutudanganya ili tumsaidie NAPE na kundi lake kutimiza malengo yao ya kisiasa ya kutaka kumtoa Lowassa KAFARA ili kuiponya CCM ambayo ipo mahututi huku ikingojea kuzikwa 2015 ktk kaburi la Sahau.
 
nchi hiii lazima iongozwe na chadema 2015 - 2020 hata asimame ndani ya ccm,,,, labda mungu, lakn binadam yeyote akisimama ndani ya ccm nachagua jiwe:love:chadema the rulling part of united republic of tanzania:A S-fire1::A S-fire1::A S-fire1:

labda nchi ya uchaggani lakini sio tanzania.. Nitakubali kupoetza kila nilichonacho ili machadema yasikaribie ikulu
 
Edward ngoyaye lowassa namfananisha na jamaa mmoja aliyekuwa na ukimwi huku akiwa na utajiri wa kutosha. Jamaa huyu baada ya kujijua kuwa ameathirika, alijitahidi kutumia nguvu za kifedha na kuwahonga wanawake wengi huku akiwaambukiza ukimwi. Walipokuja kushtuka walikuwa tayari ameisha waunganisha kwenye mtadao. Ukisha nasa hutoki.
Huu ndiyo utaratibu wa edward lowassa, ametumia fedha zake ambazo sijui anazipata wapi na kuwahonga viongozi wa dini, vijana na makundi mbalimbali ya kijamii. Lengo tinalijua anataka urais, lakini akisha pata kila mtu atatambua kuwa alikuwa ameathirika sasa ni kila mtu kusubiria kifo. Akisha ingia ikulu watanzania mtaelewa hatari ya kukukutana na mbogo aliyejeruhiwa, visasi vitatawala na ufisadi ndipo utakapochanua maua yake na kila mtu atatambua.
 
Wanabodi,

Baada ya kumsikiliza kwa makini Waziri Mkuu "Mstaafu", Edward Lowassa katika two- series za kipindi cha Dakika 45 cha ITV, kwanza nimekubali sana huyu jamaa!, pili kama yeye ndiye angekuwa rais, ile 2005, Tanzania tusingefikia hapa tulipofikishwa sasa na utawala wa JK, ila kikubwa zaidi, (kama ni kweli afya yake sio mgogoro kama anavyodai yuko fit, japo he looks sick), CCM ikimsimamisha yeye kugombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, them matokeo ya urais kwa 2015, ni CCM tena!. Mkubali, mkatae!.

Hizi ni baadhi tuu ya sababu, kwanini CCM itashinda tena, endapo and only if itamsimamisha Lowassa!.

1. Uwezo wa Kupanga, Kusema, Kusimamia na Kutenda.
Viongozi karibu wote waliopo CCM, wana uwezo mkubwa sana kupanga wa kusema tuu, (Mkukuta, Mkumbita, Mkurabita, Mkuza, na sasa Dira 2025), lakini hawana uwezo wa kusimamia na kutenda!, mipango mingi iliyopangwa, inaishia kwenye maneno na vitendo sifuri!. Edward Lowassa sio msemaji, bali ni mtendaji, yeye sio mtu wa maneno mingi, ni mtu wa vitendo virefu, he is an action oriented man!.

Tulipopata uhuru miaka ya 60, maadui wetu wakuu watatu, walikuwa ni Elimu, Umasikini na Maradhi, na tulijiwekea misingi yetu mikuu minne ya maendeleo kuwa ili tuendelee, tulihitaji vitu vinne: Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora!. Kwenye hiyo misingi, tulisema Pesa sio msingi, pesa ni matokeo!, hili ndilol lililokuwa kosa pekee la Mwalimu, kutofautiana na misingi ya ukweli ya uchumi, kama ilivyofundishwa na Adam Smith (land, labor, capital na interpreneureship)!. Kwenye ile mising minne tulisahau capital!.

Watu tunao na ardhi ya kutosha, yenye rutuba, vyanzo lukuki vya maji, madini, maliasili etc etc tunazo. Tulikuwa na tatizo la siasa safi na uongozi bora, ndio maana nchi tulizopata nazo uhuru, wao wakiwa ni masikini wa kutupwa with nothing, kana Tiger nations, leo wako mbali!, sababu pekee iliyowafikisha wenzetu pale walipo, wakati sisi tunaendelea kupiga mark time ni Elimu!. Sisi tulitaja tuu kuwa Elimu ni adui, lakini we never invested because we had no capital. Nyerere aligombana na maprofesor wa uchumi, Kina Prof. Rweyemamu, wakajitimkia zao, akagombana na IMF, WB etc matokeo tunayajua!.

Lowassa na timu yake ya Boys II Men, walipoingia tuu madarakani, akafanya study tour ya tulioanza nao kwanini wao wamefanikiwa, wako mbali na sisi wametuacha nyuma sana!, akagundua wali invest kwenye elimu!. Akarudi akahamasisha kila kata iwe na shule ya sekondari ili kila Mtanzania apate kwanza elimu, mengine yote, yatafuatia!.

Baada ya kujiuzulu, serikali ya JK ikazi abandon zile shule za EL ili kumkomoa!. Jana alipozungumzia umuhimu wa kuwaelimisha kwanza watu wetu, amenigusa sana!. Tungekuwa tumeelimika, tusingeibiwa hivi madini yetu, tumeibiwa madini kwa sababu hatuna elimu ya madini, sasa tumegundua gesi,serikali inakimbilia kugawa vitalu kwa umiliki wa miaka 99 huku Watanzania hatuna hili wala lile kuhusu elimu ya gesi, kwa kifupi, hutujui lolote na tutaishia kuibiwa tena gesi yetu kwa kukosa elimu ya gesi!. EL ameshauri, lets invest kwenye elimu kwanza ili kuwa empower watu wetu kielimu ndipo tuingie kwenye ambitious projects kama za kilimo kwanza gesi etc!.

Kwa hili pekee, CCM ikimsimamisha EL, Tanzania itapata ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania!.

Nimesema, CCM ikimsimamisha EL, 2015, itakuwa ni CCM tena, kwa sababu katika wapinzani wote, hakuna hata mgombea mmoja anayewa kusimama na Lowassa kwenye urais na bado akaambulia kura!, there is none, no one!.

Mwenye masikio na asikie!.

2. Dhambi Kubwa ya Lowassa ni Richmond Tuu!.

Najua wapinzani wa dhana ya ukweli, watakuja na hoja za dhambi kubwa ya Lowassa ni Richmond!, then time will tell, hiyo ni mizigo tuu ya watu, alijitolea kuibeba ili kwa kuteswa kwake, wao waokoke, wakati muafaka ukifika, hili litawekwa wazi na Watanzania mtawafahamu wenye zigo lao!. Wenye akili wameshang'amua ile metarmophosis process from Richmond -Dowans -Simbion na kwa msio jua, mkae mkijua Tanesco bado inailipa Simbion capacity charge ile ile ya dola 152 kama Richmond na Dowans, hivyo tumeruka majivu na kukanyaga moto, tumeruka maji na kukanyaga tope, na kwa usafi tumeruka nyasi, tukakanyaga ma..!.

3. CCM Haina zaidi ya EL na Upinzani hana wa Kushindana Nae!.

Wanabodi ni mimi niliwahi kusema, CCM imechokwa na Chadema Haijajipanga, baadae nikasema CCM imechokwa mpaka basi!, Baada ya Chadema kuanza kujipanga nikasema Chadema, Njia Nyeupe Ikulu, lakini sasa baada ya kumsikia Edward Lowassa, kama ni kweli CCM itamsimamisha, then, 2015, ni CCM tena, kinyume cha hapo, CCM ikimsimamisha mwingine yoyote, 2015, Chadema inachukuwa nchi kiulaini kama kumsukuma mlevi!.


Mwisho.

Namalizia kwa swali moja tuu, Jee CCM inaujasiri wa kuukubali huu ukweli mchungu wa kumsimamisha Edward Lowassa ili kuweza kujiokoa? au itaendeleza kiburi uongozi na jeuri ya uchama tawala kusubiria kifo cha mende huki inajiangalia kwa kutegemea itaendeleza uking'ang'anizi wake kwa kuamini this time pia itashinda tena kwa kuutumia uwongo ule ule, na mbinu zile zile za uchakachuaji ule ule, kwa kutegemea katiba mpya ita provide opportunities za aina ile ile ya miaka ya nyuma, kuwa ita endelea "to fool all the people all the times?!.

Asante.

Pasco.

NB. Japo Pasco wa JF sio mwanachama wa Chama chochote cha siasa, kwa CCM ni Pro Lowassa, kwa Chadema ni Pro ZZK na kwa CUF ni Pro-Jussa!.

Mkuu Pasco hata mimi nakuunga mkono kwa hizo hoja zako zenye mashiko na kweli tupu kwa mtanzania mwenye uchungu na mpenda maendeleo.

Unajua huyu bwana Lowasa vision yake katika suala la elimu ilikuwa nzuri sana, mwanzo alikuja na suala la kujenga shule nyingi za kata. Baadae alikuwa na lengo la kutatua shida ya walimu kwa kuwa majengo ya madarasa, nyumba za walimu na maabara tungelikuwa tumeshakamilisha kuvijenga.

Unajua hapa kinachowasumbua watu wengi kwa kukosa imani na huyu bwana Lowasa ni ile issue ya RICHMOND tu. Kwenye hili la Richmond hapa ni kama alitolewa kafara tu ili serikali isianguke. Na kwa kuwa huyu bwana ni mzalendo na mtiifu kwa serikali yake basi alikubali kutolewa kafara ili ainusuru serikali ya CCM.

Shime watanzania wapenda maendeleo tumpe nafasi huyu bwana Lowasa atufanyie hayo tunayoyaota kila kukicha.
 
Back
Top Bottom