Elections 2015 Kuelekea 2015: Kama CCM Itamsimamisha Edward Lowassa...

 
Mkuu Tanganyika Tanu, pole sana, hii kitu yako imeunganishwa kwangu!. Ili kukutendea haki, nimeiweka kule juu kwenye main post.
Pasco.
 
Richmond ndio hiyo hiyo Kagoda, ndio hihi Simbion!. Wenye akili zao, wameisha jua ni nini kinaendelea!. Dodoki linasubiriwa tuu kwenda kusafishia ule uchafu wa bungeni!. Tena hoja utakapowasilishwa ile 2014!, utashuhudia wale wale walioishadidia Richmond, ndio hao hao utawashuhudia wakiisifia Simbion!.

Mimi nitamshamshauri kwanza Mwakiembe akiseme kile ambacho hakukisema kule kwenye tume yake, kisha EL atakomelea msumari wa mwisho kwenye jeneza la issue ya Richmond kuwa ilikufa ikazikwa hatimaye ikafufuka kama Simbion huku imetakasika!, hadi Obama na JK kuichezea muziki!.
P.
 
Pasco na njaa zake ni majanga tuliyonayo ndani ya jamii...Lowassa kuwa Rais????????????????? labda ahera ambako na Nchemba atakuwa Waziri mkuu
 
Laigwanan anawafuasi wengi, hawa akina pasco wote ni wafuasi, nilikuwa sijui.
Mkuu Mjuni Lwambo!, Pasco wa jf, sio mfuasi wa mtu yoyote, hana chama, hana upande na wala sio shabiki, ila anazungumza ukweli daima!. Wengi wanadhani jua linapochomoza Mashariki ile asubuhi, na kuzama Magharibi ile jioni, wengi wanadhani jua ndilo linalozunguka, hivyo huo ndio ukweli wao wanaouamini, ila ukweli halisi, ni jua limesimama hapo lilipo, ni dunia ndio inayozunguka!. Watu wanapenda kuushabikia ukweli wao lakini sio ukweli halisi!. Pasco wa jf, anasimama na ukweli halisi!. Subiria mpaka baada ya 2015 ndipo utawajua wafuasi halisi wa EL, mimi usinihesabu, kwa sababu kazi yangu ni kukupeni tuu ukweli halisi!.
P.
 
Pasco na njaa zake ni majanga tuliyonayo ndani ya jamii...Lowassa kuwa Rais????????????????? labda ahera ambako na Nchemba atakuwa Waziri mkuu
Mkuu Ngisi, hili la njaa, ni kweli!.. ila pia jifunze kusoma kwa kituo!. hAPA NAZUNGUMZIA Lowassa kuwa rais au nazungumzia CCM imsimamishe nani?!. Kumbe na wewe umeishaujua ukweli halisi kuwa mgombea atakayesimamishwa na CCM ndie lazima awe rais!?. Endelea kuniona janga, 2015 tutakumbushana!.
P.
 
Pasco mzee wa njaa..
 
Last edited by a moderator:
"Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watashibishwa"-Nabii ...
Aisee Pasco,
Hebu nipigie pande nijiunge #Team Lowasa 2015" ili nami nijilie mema ya Nchi,
Tafadhali mkuu wangu.
Maana nami nina njaa kweli:help:
 
Last edited by a moderator:
Pasco, katika thread hii post yako ya awali umedai afya ya mzee EL inadorora. Labda ni nini kinamsibu?

Halafu zipo tetesi kuwa by 2015 mzee huyohuyo wa Monduli ataachia jimbo lake, na sasa vimeshaanza vikumbo chinichini kutafuta mrithi.

Hapa najaribu kunasibisha haya matukio na msimamo wako kihoja wa EL asimame kiti cha urais kupitia CCM.

Hebu nieleweshe kwa kadri uyajuavyo mambo.
 
Last edited by a moderator:


Hawa ndiyo wanakaopokezana vijiti.

Cc; Pasco,
Mkuu Ritz, huu ndio ukweli mchungu kwa wengi humu kuumeza!. Mimi sina mashaka kabisa na uwezo wa mpokeaji, natatizwa kidogo hali ya afya ya mpokeaji kijiti, if you look very closely with the "third eye", utaona fire in his eyes, and the fear is the weapon in his heart!.
Pasco.
 

Porojo za pasco.
 
Last edited by a moderator:
Aisee Pasco,
Hebu nipigie pande nijiunge #Team Lowasa 2015" ili nami nijilie mema ya Nchi,
Tafadhali mkuu wangu. Maana nami nina njaa kweli:help:
Mkuu Al Adawi, ingekuwa inaruhusiwa kujiapiza humu jf, ningeapa kwa Jina la Mungu aliye Juu!, WaLahi!
Pasco wa JF sio member wa Team EL!. Mimi kazi yangu ni kuandika ukweli tuu!.
Kama kwa kusema ukweli kunapelekea mimi kuonekana ndio team EL, then its ok with me!.
Watu wa ukweli, huwa hawatatizwi kabisa na hoja za wale watu ambao kazi yao ni kudhania tuu!.
P.
 
Bwa mdogo umeandika vizuri lowassa hotoshinda urais kwa sababu ya utendaji wake ni kwasababu ya hela yake na ccm kama hawatamchagua yeye basi ccm watapoteza 95% lowassa ananguvu kubwa ndani ya ccm kuliko unavyo fikiria
 
Mkuu Rock City, hii ni thread ya 2012 wakati EL alipozungumza ITV. Alisema yeye yuko fiti kabisa kwa lolote!. Nilichosema mimi humu, ni ukweli usiopinginga kuwa kwenye watu wote CCM iliyoo nao, EL the the one and only best option ya kuwapatia ushindi 2015, ila ninavyomuona mimi, kwa uonekano wake machoni, he is not fit!. He looks sick!.

Kwa vile he looks sick, lakini anasema yuko fit!, kwa kuujua ukweli huu, hivyo 2015, hatagombea sio urais wala sio ubunge!, atajipumzikia!. Kwa maoni yangu honestly, naamini hizi juhudi zote za kuonyesha kuutaka urais wa 2015, ni "sauti tuu ya mtu aliye nyikani", kunyoosha tuu mapito ya "yeye yuajaye!", ili kuzuia "mafisi!", "kunguru!" na "many'ang'au!" wasiisonge njia ya bwana!.

Naomba usiniulize hao "mafisi!", "kunguru!" na "many'ang'au!" ni akina nani, sambamba na "huyo yuajaye!".
Pasco.
 
Bwa mdogo umeandika vizuri lowassa hotoshinda urais kwa sababu ya utendaji wake ni kwasababu ya hela yake na ccm kama hawatamchagua yeye basi ccm watapoteza 95% lowassa ananguvu kubwa ndani ya ccm kuliko unavyo fikiria
Mkuu Cute, kumbe hata 2015 Watanzania watakwenda kumpigia kura mtu kwa sababu ya mihela yake!, na sio uwezo wake?!.

Kwa vile Lowassa ana nguvu kubwa ndani ya CCM kuliko ninavyofikiria, inaamani kwa uchaguzi wa 2015, mgombea mwenye nguvu kubwa ndani ya CCM ndie atakayekuwa rais wetu?!.

Nimekusikia!, mwenye masikio na asikie!".
P.
 
Porojo za pasco.
Hata dunia ilianza kwa porojo tuu! Hapo mwanzo, alikuwako Neno. Huyo. Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye. Nenoalikuwa Mungu.
Mungu katika uumbaji, alitumia porojo tuu "Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka".

Ule msemo wa mdomo huumba, maana yake kauli huumba!. Mfano hapa nilipo, depending on my powers of will and the justification iliyopo juu yako, nikitamka kwa kauli unazoziita porojo kuwa "Wewe Matola Utakufa Usiku wa Leo!", amini usiamini Mkuu Matola kesho huamki!. Sina sababu ya kutamka hivi ili kuthibisha uwezo, bali sitamki kwa sababu bado tunakuhitaji humu jf!, kama unabisha, nibishie nitamke na kukupotezea jumla!. Kesho itapandishwa thread na Invicible "Tanzia Mwana JF Mwenzetu .....Ametutoka!".
Usicheze na kauli thabiti kwa kuziita porojo!.
Pasco
 

Nimekupata vema Pasco, nimeelewa mantiki ya lugha uliyotumia.

PAMOJA.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…