Kuelekea Euro 2016: Timu zipi unazipa nafasi ya kufanya vyema?

Kuelekea Euro 2016: Timu zipi unazipa nafasi ya kufanya vyema?

Kuna timu zina wachezaji wenye majina makubwa lakini sio ndio garantii ya kufanya vyema hasa linapokuja suala la Tournament kubwa kama hii ya Euro 2016 ambayo itafanyika Ufaransa kwanzia 10 June mpaka 10 July na kushirikisha jumla ya timu 24.

Leo nataka tujadiliane timu ambazo zitafika mbali yani kwanzia nusu fainali mpaka fainali kutokana na uhodari wa vikosi vyao, kujituma kwa wachezaji pamoja na makundi waliyopo.
1009302-___n-1450013811-956-640x480.jpg


Mimi nazipa nafasi timu hizi nne kufika mbali zaidi.
1.Ufaransa
Licha ya kuwa wenyeji tu bali pia wana kikosi cha dhahabu kama vile Pogba, Martial, Griezmann, Laporte, Coman, Benzema na wengineo wengi.

2.Ubelgiji
Kikosi kingine ninachokipa nafasi kwa kuwa timu yenye wachezaji wenye muunganiko mzuri.

3.Ujerumani
Never underestimate the Germans.
Kitu pekee ninachowapa nafasi hawa jamaa ni uwezo wao wa kuwa na wachezaji wenye kujituma sana hasa linapokuja suala la kuvaa jezi ya timu ya taifa. Wana wachezaji ambao huwa hawavumi sana katika klabu zao ila wanapafomu vizuri timu ya taifa. Rejea kuhusu mkongwe aliyestafu Miroslav klose.

4.Croatia
Watu wengi hawazungumzii kuhusu Croatia ila balaa lake ni moto wa kuotea mbali kuna mafundi wa kutosha wasioimbwa ulaya kama akina Kovacic, Modric, Rakitic na wengineo.

Karibu utuambie na wewe timu unazozipa nafasi kufanya vyema kwenye Euro 2016 pale Ufaransa.

========================================================================================================

Ratiba kamili na muda hii hapa chini
CfdApuQXEAAAeUN.jpg

CkdfMTtXIAAR8i_.jpg
Kete yangu inaenda kwa aidha Germany, Italy au Croatia.
 
Hii game hii. Croatia own possession so far, lakini Portugal wamekuwa aggressive tangu mwanzo.
 
Modric kawafunika viungo wote wa ureno, hii timu inahitaji kocha mwenye mbinu mpya, maana wana wachezaji wote wazuri Lakini mpira vumbi tupu,
Ronaldo leo anacheza beki 3 naona
 
Back
Top Bottom