Kuelekea game na Wydad: Wajibu wa benchi la ufundi kwa Onyango!

Kuelekea game na Wydad: Wajibu wa benchi la ufundi kwa Onyango!

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583
Wakuu,

Beki kisiki Josh Onyango amekuwa ni mhimili wa ulinzi Simba lakini amekuwa akifanya makosa yanayofanana mara nyingi. Josh akiachwa kwenye kasi akili yake ni kucheza rafu bila kuangalia eneo alilopo na uwezekano wa kupata msaada.

Bado hatuna beki bora kuliko Onyango na mapungufu yake kwasasa ni wajibu wa benchi la ufundi nje ya kuangalia mfumo ni lazima kuwe na special assignment kurekebisha makosa ya Onyango. Tuna mabeki bora duniani waliocheza kwa umri mkubwa na wasio na kasi kubwa lakini wamefanya vizuri zaidi.

Wachezaji waliopo ndio wataotumika, bado inawezekana kabisa tukafanya vizuri kama tuki focus vizuri kwenye kuandaa Wachezaji kama timu na individually.

Ushauri,
Simba waajiri special consultancy team wenye experience kwenye defence mechanisms. Hii iwe ni project fupi kwaajili ya hatua hii ya robo fainali. Makocha Robertinho na Mgunda wamecheza kama washambuliaji enzi zao! Nahisi kwenye ulinzi wa kupambana na timu kama Wydad ni muhimu washauriwe na independent consultant.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
FB_IMG_1680371672550.jpg
 
Tatizo yawezekana Ikawa UMRI wake kujirudia kwamakosa yake haizuiliki labda umri urudi kawaida
Kwa energy aliyonayo bado umri si tatizo. Onyango tuliambiwa hayo mapungufu toka anakuja Simba. Kuna Mkenya alihojiwa na kuonya juu ya makosa haya haya ya Onyango. Sasa ni vizuri kumjenga upya kiufundi, kisaikolojia na shape ya kumsaidia.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Onyango ni beki mzuri hana masihara na kazi sioni kama kuna wa kucover nafasi yake kwa sasa,
Apewe tu ushauri nini afanye adui akiwa kwenye eneo la hatari na siyo kufanya faul za kukamata mchezaji,anarudia hayo makosa mara kwa mara tusipokuwa makini waarabu watafanya kila namna hapo pawe uchochoro wa kwenda kumchungulia manula
 
Onyango anakosa unyumbufu na Kasi Kwaiyo wachezaji wenye maarifa wanatengeneza mazingira ya kukutanae 1vs 1 ukisha mdanganya wewe mlazimishe lazima acheze faul.

Kwenye ligi yetu onyango anacheza sana faul za 1 vs 1 ila marefa wetu Wana Mlinda Kwa Ukubwa wa timu anayo chezea.

Watangazaji wakampa jina la mtu chuma ila Onyango, Kanuti, Mzamiru ao wachezaji ukiwalazimisha watacheza faul tu kwakua hawana Kasi na wanakosa maarifa ya kudhibiti wenye Kasi.
 
Onyango anakosa unyumbufu na Kasi Kwaiyo wachezaji wenye maarifa wanatengeneza mazingira ya kukutanae 1vs 1 ukisha mdanganya wewe mlazimishe lazima acheze faul.

Kwenye ligi yetu onyango anacheza sana faul za 1 vs 1 ila marefa wetu Wana Mlinda Kwa Ukubwa wa timu anayo chezea.

Watangazaji wakampa jina la mtu chuma ila Onyango, Kanuti, Mzamiru ao wachezaji ukiwalazimisha watacheza faul tu kwakua hawana Kasi na wanakosa maarifa ya kudhibiti wenye Kasi.
Ndugu, mzamiru hana kasi??? Onyango hana sifa zozote za modern defender. Ni kama tu Kagere wote hao ni outdated players. Onyango si mzuri akiwa na mpira, passing ability yake ni duni na pia tactically na game awareness yupo chini sana ki uwezo.

Mfano Dickson Job ni a complete modern player labda tu kimo ndio changamoto kwake ila kuanzia footwork, game intelligence yupo vizuri sana the same Bacca. Onyango ni nguvu nyingi akili kisoda ukikuta mpinzan mzuri lazima uone madhaifu yake. Shida ya ya Management ya Simba wanalea sana wachezaji eg Mkude hana cha kuipa tena Simba na benchi la ufundi hawatoi nafasi kwa wachezaji wa akiba
 
Kila ukimpita Onyango anachokiwaza ni kukushika na mikono au kukusukuma. Hii ni dalili tosha kuwa umri umemtupa.

Bado siku chache tu mnakutana na Yanga - Wtapita hapo sebuleni kwenu kama wanamsukuma mlevi.

Mpeni nafasi Outara amalizie ligi kisha mwambieni MO aache ubahili afanye usajili wa maana
 
Back
Top Bottom