Kuelekea Klabu Bingwa Afrika | Simba SC na Al Ahly SC, Mechi ya Kibabe kwa Wababe wa Soka

Kuelekea Klabu Bingwa Afrika | Simba SC na Al Ahly SC, Mechi ya Kibabe kwa Wababe wa Soka

Status
Not open for further replies.
Jambo TANZANIA na Duniani Kote..!

Naaaam..!

Jumanne ya February 23, 2021 muda wa saa 10:00 Alasiri, kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, kutakuwa mchezo wa kundi A' wa Klabu Bingwa Barani Afrika ambapo Mnyama Mkali Kuliko Wote Mwituni Simba SC, anakwaruzana na Mabingwa Watetezi Al Ahly SC kutoka nchini Misri.

Patashika hii ya aina yake inatarajiwa kuwa kali mno, na ya kusisimua kwa wote wa muda wote dakika 90 kwa kila timu kuhitaji ushindi na kujikusanyia alama tatu muhimu.

Timu zote mbili katika michezo yao ya kwanza waliweza kushinda, ambapo Simba SC waliweza kuibuka na ushindi ugenini wa bao 1-0 dhidi ya AS Vita Club na Al Ahly SC wakiwachapa Al Merrikh kwa mabao 3-0 nchini Misri.

Kutoka Simba SC "Ni jukumu la kuteta heshima ya soka TANZANIA na Afrika Mashariki lipo kwetu hivyo maandalizi ya kuleta heshima tutakapowakabili Mabingwa namba tatu wa dunia inaendelea.

Mechi ya Kibabe, mechi ya wanaume wa shoka, wababe wa soka Afrika, siyo ya kukosa, vita ndani ya uwanja kuhakikisha tunabeba alama zote tatu za mchezo"
taarifa ya Simba SC imeeleza.

Jambo kubwa kwetu kama Watanzania, Wanachama na Mashabiki wa Simba SC pamoja na Wadau wa soka ni kuwaombea dua wanajeshi wetu.

Si mchezo mwepesi lakini kuna jambo tunakwenda kulifanya kuelekea mchezo huo, hivi ni vita zaidi ya vita vya Kimbari, hivyo kunahitaji jitihada na nguvu ya pamoja kuweza kushinda vita. Hivyo tujipange na tuweze kushinda na kuipeperusha vema bendera yetu..Mungu Ibariki Simba, Mungu Ibariki TANZANIA.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

Utapata yanayojiri kuanzia leo mpaka siku ya mchezo kutoka kwa Jopo la WanaJF sembo, OKW BOBAN SUNZU, Shunie, NAWATAFUNA, Mwifwa, Dam55, mjingamimi, Root, rodrick alexander, mmteule, Payrol Saint Ivuga, King Ngwaba, Scars na wengine chini ya Nahodha...Ghazwat View attachment 1708072View attachment 1708073

Update;

Wachezaji wa Simba SC wamefanya mazoezi leo jioni ya February 21 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa

Tayari kabisa kuwakabili Al AhlyView attachment 1708571

..MO Dewji

Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba SC na Mwenyekiti Murtaza Mangugu pamoja na Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez, wamehudhuria mazoezi leo kuona namna timu inavyojiandaa kuwakabili Al Ahly.

..Kocha Msaidizi Suleiman Matola

"Si rahisi ni mechi ngumu ikichukulia kwamba tulipata matokeo katika mchezo uliopita, na ukiangalia ligi ya mabingwa Afrika hakuna mtu rahisi.

Lakini tumejipanga pamoja kwa kwamba tunakutana timu ambayo iko nzuri na bora zaidi, lakini lazima tuhakikishe tunapata matokeo katika mchezo wetu wa nyumbani".

..Kocha wa Al Ahly Pitso Mosimane

"Tupo tayari kwa mchezo hakuna la kuhofia na muda wa mechi sio sababu ya kubadili kikosi, tupo tayari kwa mapambano.

Simba ilicheza Kinshasa na kushinda dhidi ya As Vita na hicho ndo kitu ambacho kinatufanya tuwe makini zaidi dhidi ya Simba.

Walicheza vizuri sana hiyo inaashiria benchi la ufundi linafanya kasi nzuri.

Ina wachezaji wazuri wa kigeni, Luis ni mchezaji mzuri nilimsajili kutoka Msumbiji wakati nikiwa Mamelodi na tukamtoa kwa mkopo kuja Simba, ni mchezaji muhimu

Claotus ni mchezaji anayependa kucheza mpira, tulikutana naye wakati anachezea Zesco, ni mchezaji mzuri

Washambuliaji ni wazuri, mchezaji namba 7 [Mugalu] halafu wana mchezaji mkongwe namba 14 [Kagere] ni top player na kuna kiungo mwingine wa Zambia [Bwalya]".
Huyu kocha wa Al Ahyl anaonekana anawajua vizuri wachezaji wa Simba.kwa namna navyojua Mimi ukimjua mtu vizuri ni rahisi kumkabili kila la heri Simba ila mjipange mechi ni ngumu sana kwa Simba msipojipanga vizuri mtapigika kipigo Cha kufa mtu.Kwa sababu hawa Al Ahyl wamekamilika akitoka mtu anaingia mtu Simba hawana ukamilifu huo Ni wachezaji wale wale uwezo uleule kiasi kwamba hawana mbadala wa kubadilisha mchezo.
 
Acha nitoe utabiri wangu bado mapema wa kikosi Cha Simba Vs Al Ahly:

1. Aishi Manula
2. Shomary Kapombe
3. Mohamed Hussein
4. Paschal Wawa
5. Joash Onyango
6. Peter Muduhwa/Erasto Nyoni
7. Luis Miquissone
8. Thadeo Lwanga
9. Chriss Mugalu
10. Lary Bwalya
11. Clotas Chama

Formation 3:4:2:1

Huu mfumo ni mzuri wa kuwa na mabeki watatu nyuma Timu inakuwa na uwiano mzuri wa kushambulia na kuzuia rejea mechi ya Simba Vs Platinum pale kwa Mkaba...
Wachezaji Ni hao hao hawana mbadala . Sasa wale waarabu wana uwezo wa kubadilisha timu nzima.
 
Benchi la ufundi la simba lipo vizuri, yule mtaalamu wa video keshawachambua vizuri.

Siku hiyo Gomes atawashangaza waarabu kwa mfumo na aina ya uchezaji watakaokuja.nao Simba utawashangaza.

Simba ndio timu ya kwanza kuwa na uhakika wa.kufuzu ili kundi.
Haya ndugu.Ngoja tuone.Muda utasema,Leo Mwarabu anataka kujihakikishia kuongoza kundi na kuvuka hatua .Simba ndiyo mtajua Kama mna benchi la Ufundi au mna kikundi Cha wahuni ambao Wana uwezo wa kumsoma mpinzani na kumkabili .Najua baada ya hii mechi kutakuwa na kulaumiana sana kwamba hapa tatizo ni fulani na fulani hawatufahi waondoke
 
Senzo na Pitso wamefanya kazi pamoja Mamelodi, wanajuana, na wote ni wasauzi
Hivi kama Senzo angekuwa bado CEO wa Simba SC, siku moja kabla ya mchezo angekwenda Hotel kisa wanajuana?

Na kwanini asisubiri baada ya mchezo...! Ndo maana tunasema huyu ametangaza Vita na Mnyama Mkali.
 
What a day....KUN FAYAKUN
giphy.gif
 
Hivi kama Senzo angekuwa bado CEO wa Simba SC, siku moja kabla ya mchezo angekwenda Hotel kisa wanajuana?

Na kwanini asisubiri baada ya mchezo...! Ndo maana tunasema huyu ametangaza Vita na Mnyama Mkali.
we acha hizo mbona ceo wa simba barbara alikutana na kocha wa vita ibenge hotelini, tena siku chache kabla ya mechi
 
Mkuuu Ghazwat kama unaweza huu huu uzi ndio tubadili tittle uwe wa LIVE UPDATE tuliamshe hapa hapa mpaka kieleweke... The point of No Return
Ndiyo Mkuu mmteule wazo bomba hili, ngoja tuwaatarifu Moderator watubadilishie Tittle uwa Live Update..!

Heading

Uwanja wa Benjamin Mkapa | Klabu Bingwa Afrika, Simba SC Vs Al Alhy SC, Vita zaidi ya Vita.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom