Kuelekea Klabu Bingwa Afrika | Simba SC na Al Ahly SC, Mechi ya Kibabe kwa Wababe wa Soka

Kuelekea Klabu Bingwa Afrika | Simba SC na Al Ahly SC, Mechi ya Kibabe kwa Wababe wa Soka

Status
Not open for further replies.
Refa wa pambano keshajulikana, anatoka Cameroon ni Sidi Aliom.
Ndiye aliyechezesha fainali ya (AFCON) mwaka 2019kati ya Algeria na Senegal
Mwaka 2014 alichezesha fainali za kombe la dunia lililofanyika Brazil na kuweka rekodi ya kuwa refa mdogo zaidi katika mashindano ya mwaka huo. Pia amewahi kuchezesha kombe la duniaa la vijana chini ya umri wa miaka20 na piaa kombe la dunia la vijana chini ya miaka 17 atasaidiwa wasaidizi 2 na refa wa akiba ambao wote watatoka Cameroon.
Kamishina wa Mchezo atatoka Kenya.
Msimamizi mkuu atatoka Sudan wakati mtathimini wa kiufundi wa masuala ya luninga atatoka Tunisiawakato ofisa wa masuala ya vipimo vya covid 19 atatoka Tanzania.
CAF imeona ukubwa wa pambano hadi ikachagua refa makini kuchezesha hili pambano.
Hao tunawamudu
 
Jambo TANZANIA na Duniani Kote..!

Naaaam..!

Jumanne ya February 23, 2021 muda wa saa 10:00 Alasiri, kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, kutakuwa mchezo wa kundi A' wa Klabu Bingwa Barani Afrika ambapo Mnyama Mkali Kuliko Wote Mwituni Simba SC, anakwaruzana na Mabingwa Watetezi Al Ahly SC kutoka nchini Misri.

Patashika hii ya aina yake inatarajiwa kuwa kali mno, na ya kusisimua kwa wote wa muda wote dakika 90 kwa kila timu kuhitaji ushindi na kujikusanyia alama tatu muhimu.

Timu zote mbili katika michezo yao ya kwanza waliweza kushinda, ambapo Simba SC waliweza kuibuka na ushindi ugenini wa bao 1-0 dhidi ya AS Vita Club na Al Ahly SC wakiwachapa Al Merrikh kwa mabao 3-0 nchini Misri.

Kutoka Simba SC "Ni jukumu la kuteta heshima ya soka TANZANIA na Afrika Mashariki lipo kwetu hivyo maandalizi ya kuleta heshima tutakapowakabili Mabingwa namba tatu wa dunia inaendelea.

Mechi ya Kibabe, mechi ya wanaume wa shoka, wababe wa soka Afrika, siyo ya kukosa, vita ndani ya uwanja kuhakikisha tunabeba alama zote tatu za mchezo"
taarifa ya Simba SC imeeleza.

Jambo kubwa kwetu kama Watanzania, Wanachama na Mashabiki wa Simba SC pamoja na Wadau wa soka ni kuwaombea dua wanajeshi wetu.

Si mchezo mwepesi lakini kuna jambo tunakwenda kulifanya kuelekea mchezo huo, hivi ni vita zaidi ya vita vya Kimbari, hivyo kunahitaji jitihada na nguvu ya pamoja kuweza kushinda vita. Hivyo tujipange na tuweze kushinda na kuipeperusha vema bendera yetu..Mungu Ibariki Simba, Mungu Ibariki TANZANIA.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

Utapata yanayojiri kuanzia leo mpaka siku ya mchezo kutoka kwa Jopo la WanaJF sembo, OKW BOBAN SUNZU, Shunie, NAWATAFUNA, Mwifwa, Dam55, mjingamimi, Root, rodrick alexander, mmteule, Payrol Saint Ivuga, King Ngwaba, Scars na wengine chini ya Nahodha...Ghazwat View attachment 1708072View attachment 1708073

Update;

Wachezaji wa Simba SC wamefanya mazoezi leo jioni ya February 21 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa

Tayari kabisa kuwakabili Al AhlyView attachment 1708571

Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba SC na Mwenyekiti Murtaza Mangugu pamoja na Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez, wamehudhuria mazoezi leo kuona namna timu inavyojiandaa kuwakabili Al Ahly.

Kocha Msaidizi Suleiman Matola

"Si rahisi ni mechi ngumu ikichukulia kwamba tulipata matokeo katika mchezo uliopita, na ukiangalia ligi ya mabingwa Afrika hakuna mtu rahisi.

Lakini tumejipanga pamoja kwa kwamba tunakutana timu ambayo iko nzuri na bora zaidi, lakini lazima tuhakikishe tunapata matokeo katika mchezo wetu wa nyumbani".

Kocha wa Al Ahly Pitso Mosimane

"Tupo tayari kwa mchezo hakuna la kuhofia na muda wa mechi sio sababu ya kubadili kikosi, tupo tayari kwa mapambano.

Simba ilicheza Kinshasa na kushinda dhidi ya As Vita na hicho ndo kitu ambacho kinatufanya tuwe makini zaidi dhidi ya Simba.

Walicheza vizuri sana hiyo inaashiria benchi la ufundi linafanya kasi nzuri.

Ina wachezaji wazuri wa kigeni, Luis ni mchezaji mzuri nilimsajili kutoka Msumbiji wakati nikiwa Mamelodi na tukamtoa kwa mkopo kuja Simba, ni mchezaji muhimu

Claotus ni mchezaji anayependa kucheza mpira, tulikutana naye wakati anachezea Zesco, ni mchezaji mzuri

Washambuliaji ni wazuri, mchezaji namba 7 [Mugalu] halafu wana mchezaji mkongwe namba 14 [Kagere] ni top player na kuna kiungo mwingine wa Zambia [Bwalya]".
Wengine wanahudhuria mazoezi kuhakikisha wachezaj wanajiandaa vizuri kwa mchezo wengine wanaita waandishi wa habari kuwaambia wanasusia ligi. 😂😂
 
Wengine wanahudhuria mazoezi kuhakikisha wachezaj wanajiandaa vizuri kwa mchezo wengine wanaita waandishi wa habari kuwaambia wanasusia ligi. [emoji23][emoji23]
Ndo tofauti ya Timu Bora na Kubwa Barani Afrika (Mnyama) na Timu Kongwe! Uto[emoji12]
 
Mwamba Senzo vs Pisto


[emoji16][emoji16][emoji16] Kamati ya roho mbaya
jamestupatupa-___CLmoIxjn7ZW___-.jpg

Mwamba Senzo Msingisa
 
Nimerejea jukwaani tena baada ya kimya ya majuma kadhaa kupita, nimekuwa nikitoa maoni/Utabiri wangu kuhusiana ushiriki wa Simba kwenye klabu bingwa msimu huu kwanzia game ya kwanza dhidi ya plateau United ya Nigeria.

Haya leo tena ni siku nyingine nzuri kwa wapenzi na mashabiki wa pande zote mbili yaani Simba na Yanga pia maana inapigwa bonge moja la mechi kwenye dimba la Mkapa. Hivyo wapenzi wa mpira wa miguu tutaona burudani ya aina yake siku ya leo.

Sasa kama wewe ni mpenzi ama mshabiki wa Yanga au pengine sio mpenzi wa Yanga lakini moyoni mwako umetokea tu kuichukia timu ya Simba, basi leo nakushauri fanya hivi ili mechi ikiisha uwe na furaha na chuki zako.

Chukua kiasi cha pesa ulichokuwa tayari kukipoteza kama sehemu ya kupata furaha yako, kama ni sh 10,k 20k, 50k, au 100k n.k kisha hiyo pesa mpe Simba double chance (mpe simba au sare) kwenye mechi ya leo Simba amepewa point nyingi kwenye double chance (1.65) hivyo ukitia mzigo wako unaambulia ela ya maana tu

Nini faida yake?
Faida yake ni kwamba moyo wako unakuwa upo neutral yaani unakuwa hauna presha kubwa katika kutamani jambo fulani litokee kwasababu matokeo ya namna yoyote yatakayotokea kwako ni furaha. Ikitokea Simba amefungwa utakuwa na furaha kwasababu ya kuwachukia Simba. Na pia ikitokea Simba ameshinda au katoa sare basi utakuwa na furaha kwavile wamekuingizia hela.

Kwa shabiki yeyote yule asiyeipenda Simba basi leo afanye hivyo ili kuepuka kuangalia mpira huku umenuna au sura umeikunja kama umelamba ndimu. Ukifanya hivyo unaangalia mpira huku ume relax kabisa moyo tuliiii.
 
Utopolo kila wanapogusa pa Moto, Simba SC [emoji881] anakiwasha Tena hatoki mtu.

#TOTAL WAR; POINT OF NO RETURN#

ALL THE BEST LIONS
 
Faida zingine za kuipenda Simba ni pamoja na:
1)Unaongeza uwezo wa mapafu kuwa na oksijen ya kutosha,tatizo la upumuaji litakua historia kwako.

2)Kuongeza vitamin mwilini.

3)Thinking capacity inaongezeka siku baada ya siku.

4)Kiwango cha kipato chako kuimarika,mashabiki wa Simba atunaga njaa,atuna strees za maisha,kipindi cha mvua atusombwi na mafuriko.
 
Utajiri wa mwamedi mnaona ni wa baba zenu
Faida zingine za kuipenda Simba ni pamoja na:
1)Unaongeza uwezo wa mapafu kuwa na oksijen ya kutosha,tatizo la upumuaji litakua historia kwako.
2)Kuongeza vitamin mwilini.
3)Thinking capacity inaongezeka siku baada ya siku.
4)Kiwango cha kipato chako kuimarika,mashabiki wa Simba atunaga njaa,atuna strees za maisha,kipindi cha mvua atusombwi na mafuriko.
 
anayejua kikosi cha leo tafadhali..! chama la wana SIMBA.
NAPENDEKEZA MWALIMU ATUMIE MFUMO WA 4 2 3 1

4 defenders
KAPOMBE
M.HUSSEIN
WAWA
ONYANGO

2 Defending midfilders
MZAMIRU
TADEO LWANGA

2 Central midfilders + 1 attacking midfilder

BWALYA
MIQWISSONE
CHAMA

1 Striker
KAGERE/MGALU/BOCCO

Mwarabu atapata taabu sanaaa
 
NAPENDEKEZA MWALIMU ATUMIE MFUMO WA 4 2 3 1

4 defenders
KAPOMBE
M.HUSSEIN
WAWA
ONYANGO

2 Defending midfilders
MZAMIRU
TADEO LWANGA

2 Central midfilders + 1 attacking midfilder

BWALYA
MIQWISSONE
CHAMA

1 Striker
KAGERE/MGALU/BOCCO



Mwarabu atapata taabu sanaaa
Umepita mulemule nilifyofikiria mimi,ila kwenye stricker aanze Muga,ana uwezo wa kukaa na mipira miguuni.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom