Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hao tunawamuduRefa wa pambano keshajulikana, anatoka Cameroon ni Sidi Aliom.
Ndiye aliyechezesha fainali ya (AFCON) mwaka 2019kati ya Algeria na Senegal
Mwaka 2014 alichezesha fainali za kombe la dunia lililofanyika Brazil na kuweka rekodi ya kuwa refa mdogo zaidi katika mashindano ya mwaka huo. Pia amewahi kuchezesha kombe la duniaa la vijana chini ya umri wa miaka20 na piaa kombe la dunia la vijana chini ya miaka 17 atasaidiwa wasaidizi 2 na refa wa akiba ambao wote watatoka Cameroon.
Kamishina wa Mchezo atatoka Kenya.
Msimamizi mkuu atatoka Sudan wakati mtathimini wa kiufundi wa masuala ya luninga atatoka Tunisiawakato ofisa wa masuala ya vipimo vya covid 19 atatoka Tanzania.
CAF imeona ukubwa wa pambano hadi ikachagua refa makini kuchezesha hili pambano.
Wengine wanahudhuria mazoezi kuhakikisha wachezaj wanajiandaa vizuri kwa mchezo wengine wanaita waandishi wa habari kuwaambia wanasusia ligi. 😂😂Jambo TANZANIA na Duniani Kote..!
Naaaam..!
Jumanne ya February 23, 2021 muda wa saa 10:00 Alasiri, kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, kutakuwa mchezo wa kundi A' wa Klabu Bingwa Barani Afrika ambapo Mnyama Mkali Kuliko Wote Mwituni Simba SC, anakwaruzana na Mabingwa Watetezi Al Ahly SC kutoka nchini Misri.
Patashika hii ya aina yake inatarajiwa kuwa kali mno, na ya kusisimua kwa wote wa muda wote dakika 90 kwa kila timu kuhitaji ushindi na kujikusanyia alama tatu muhimu.
Timu zote mbili katika michezo yao ya kwanza waliweza kushinda, ambapo Simba SC waliweza kuibuka na ushindi ugenini wa bao 1-0 dhidi ya AS Vita Club na Al Ahly SC wakiwachapa Al Merrikh kwa mabao 3-0 nchini Misri.
Kutoka Simba SC "Ni jukumu la kuteta heshima ya soka TANZANIA na Afrika Mashariki lipo kwetu hivyo maandalizi ya kuleta heshima tutakapowakabili Mabingwa namba tatu wa dunia inaendelea.
Mechi ya Kibabe, mechi ya wanaume wa shoka, wababe wa soka Afrika, siyo ya kukosa, vita ndani ya uwanja kuhakikisha tunabeba alama zote tatu za mchezo" taarifa ya Simba SC imeeleza.
Jambo kubwa kwetu kama Watanzania, Wanachama na Mashabiki wa Simba SC pamoja na Wadau wa soka ni kuwaombea dua wanajeshi wetu.
Si mchezo mwepesi lakini kuna jambo tunakwenda kulifanya kuelekea mchezo huo, hivi ni vita zaidi ya vita vya Kimbari, hivyo kunahitaji jitihada na nguvu ya pamoja kuweza kushinda vita. Hivyo tujipange na tuweze kushinda na kuipeperusha vema bendera yetu..Mungu Ibariki Simba, Mungu Ibariki TANZANIA.
Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
Utapata yanayojiri kuanzia leo mpaka siku ya mchezo kutoka kwa Jopo la WanaJF sembo, OKW BOBAN SUNZU, Shunie, NAWATAFUNA, Mwifwa, Dam55, mjingamimi, Root, rodrick alexander, mmteule, Payrol Saint Ivuga, King Ngwaba, Scars na wengine chini ya Nahodha...Ghazwat View attachment 1708072View attachment 1708073
Update;
Wachezaji wa Simba SC wamefanya mazoezi leo jioni ya February 21 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa
Tayari kabisa kuwakabili Al AhlyView attachment 1708571
Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba SC na Mwenyekiti Murtaza Mangugu pamoja na Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez, wamehudhuria mazoezi leo kuona namna timu inavyojiandaa kuwakabili Al Ahly.
Kocha Msaidizi Suleiman Matola
"Si rahisi ni mechi ngumu ikichukulia kwamba tulipata matokeo katika mchezo uliopita, na ukiangalia ligi ya mabingwa Afrika hakuna mtu rahisi.
Lakini tumejipanga pamoja kwa kwamba tunakutana timu ambayo iko nzuri na bora zaidi, lakini lazima tuhakikishe tunapata matokeo katika mchezo wetu wa nyumbani".
Kocha wa Al Ahly Pitso Mosimane
"Tupo tayari kwa mchezo hakuna la kuhofia na muda wa mechi sio sababu ya kubadili kikosi, tupo tayari kwa mapambano.
Simba ilicheza Kinshasa na kushinda dhidi ya As Vita na hicho ndo kitu ambacho kinatufanya tuwe makini zaidi dhidi ya Simba.
Walicheza vizuri sana hiyo inaashiria benchi la ufundi linafanya kasi nzuri.
Ina wachezaji wazuri wa kigeni, Luis ni mchezaji mzuri nilimsajili kutoka Msumbiji wakati nikiwa Mamelodi na tukamtoa kwa mkopo kuja Simba, ni mchezaji muhimu
Claotus ni mchezaji anayependa kucheza mpira, tulikutana naye wakati anachezea Zesco, ni mchezaji mzuri
Washambuliaji ni wazuri, mchezaji namba 7 [Mugalu] halafu wana mchezaji mkongwe namba 14 [Kagere] ni top player na kuna kiungo mwingine wa Zambia [Bwalya]".
Ndo tofauti ya Timu Bora na Kubwa Barani Afrika (Mnyama) na Timu Kongwe! Uto[emoji12]Wengine wanahudhuria mazoezi kuhakikisha wachezaj wanajiandaa vizuri kwa mchezo wengine wanaita waandishi wa habari kuwaambia wanasusia ligi. [emoji23][emoji23]
Huyu ndo kazi ambayo amebaki nayo ni ya kudanga na shobo tu..TFF ipo haja ya kumpiga Komeo.Mwamba Senzo vs Pisto
[emoji16][emoji16][emoji16] Kamati ya roho mbaya View attachment 1709592
Mwamba Senzo Msingisa
Faida zingine za kuipenda Simba ni pamoja na:
1)Unaongeza uwezo wa mapafu kuwa na oksijen ya kutosha,tatizo la upumuaji litakua historia kwako.
2)Kuongeza vitamin mwilini.
3)Thinking capacity inaongezeka siku baada ya siku.
4)Kiwango cha kipato chako kuimarika,mashabiki wa Simba atunaga njaa,atuna strees za maisha,kipindi cha mvua atusombwi na mafuriko.
NAPENDEKEZA MWALIMU ATUMIE MFUMO WA 4 2 3 1anayejua kikosi cha leo tafadhali..! chama la wana SIMBA.
[emoji23][emoji23]Utajiri wa mwamedi mnaona ni wa baba zenu
Umepita mulemule nilifyofikiria mimi,ila kwenye stricker aanze Muga,ana uwezo wa kukaa na mipira miguuni.NAPENDEKEZA MWALIMU ATUMIE MFUMO WA 4 2 3 1
4 defenders
KAPOMBE
M.HUSSEIN
WAWA
ONYANGO
2 Defending midfilders
MZAMIRU
TADEO LWANGA
2 Central midfilders + 1 attacking midfilder
BWALYA
MIQWISSONE
CHAMA
1 Striker
KAGERE/MGALU/BOCCO
Mwarabu atapata taabu sanaaa