Kuelekea kuadhimisha miaka 10 ya ndoa

Wazee wa kataa ndoa wako wapi leo??
 
Ndoa ni jambo jema na ndoa si msahafu na kuilinganisha ndoa na gereza ni kugenerelize mambo.Furaha na huzuni kwenye ndoa inatokana na jinsi gani nyie mnaendesha ndoa yenu, kama imekua ngumu kuishi pamoja kwanini mlazimishe kuendelea kuishi pamoja.Kama Kiungo cha mwili kikihatarisha afya ya mwili unakikata kwanini ishindikane kuachana na ndoa korofi.
 
Hongera mkuu, inaonekana mda wa uchumba uliutumia vizuri katika kuchunguzana.

Mwaka ujao,natimiza miaka 10 ya ndoa,ndoa ni nzuri,familia ni nzuri,kila napoamka asubuhi nawaona watoto wangu wanavyonifurahia,naporudi nyumbani wanavyonikimbilia na kunikumbatia,nahisi faraja,Upendo,amani najawa na tumaini katika maishaπŸ™
Hapo Kuna mwamba anatimiza miaka 7 na mtoto mmoja Ni wake
 
Kwa niaba ya Moderators naomba nikupongeze. Hongera sana Mkuu.
 
Kwahiyo unataka kusema mababu na mabibi zetu waliodumu kwenye ndoa zaidi ya miaka 80 hawakuwa na akili timamu? Asiye na akili ndio anaikimbia ndoa, we umeona wapi kichaa akaoa? Na ndio maana moja ya vigezo vya mtu kuoa awe na akili timamu.
Nimeleta kama swali,sijaleta kama hoja. Pia jitahidi kusoma key point za swali husika kabla haujaandika unachowaza!!
 
Kwani kuna tofauti kati ya ndoa na kuishi na mwanamke?

Mimi naishi na mwanamke na tunalea watoto wetu, je nina tofauti gani na wewe?
 
Kwahiyo unataka kusema mababu na mabibi zetu waliodumu kwenye ndoa zaidi ya miaka 80 hawakuwa na akili timamu? Asiye na akili ndio anaikimbia ndoa, we umeona wapi kichaa akaoa? Na ndio maana moja ya vigezo vya mtu kuoa awe na akili timamu.
Kuna thinking and reasoning reasoning capacity fulani ukiwa nayo mahusiano yanakuwa mtihani Mkubwa sana, hasa nature ya malezi na imani za jamii zetu.
 
Kwani kuna tofauti kati ya ndoa na kuishi na mwanamke?

Mimi naishi na mwanamke na tunalea watoto wetu, je nina tofauti gani na wewe?
Huyo mwanamke iko siku utamtimua endapo mtatofautiana na kibaya zaidi hapo alipo hana haki wala wajibu ni kama unamtumikisha na siku ukimtimua popote atakapokwenda hawezi kupata msaada wa kisheria kwa sababu itaonekana mlikuwa mnaishi na hamna ndoa. Hivyo kigezo hicho ndio kama ushindi kwako.
 
Kumbe kufunga ndoa ni kwa ajili ya kujihami.

Nilidhani ukifunga ndoa upendo unaongezeka na kuwa na familia yenye furaha, kumbe siyo.

Mimi nitaendelea hivi hivi ili tuendelee kuheshimiana.
 
Sio kila mtu anatamani ndoa mkuu badili hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…