Kuelekea kupanga mishahara upya; Mishahara ilingane kwa kada zote

Mtarban

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2015
Posts
3,858
Reaction score
5,101
Habari wanandugu,

Nianze kwa kusema kuwa niipongeze serikali kwa nia nzuri iliyonayo ya kupitia na kupanga upya viwango vya mishahara kwa wafanyakazi wa kada zote.

Kwa muda mwingi tumeshuhudia kutofautiana kwa viwango vya mishahara kutoka fani mmoja kwenda fani nyingine, mfano ualimu, afya, sheria, uhandisi n.k ambapo baadhi ya Kada wamekuwa wakilipwa mishahara mikubwa kuliko wengine ingawa ukiangalia majukumu na mazingira yao ya kufanyia kazi hayatofauti sana.

Kutofautiana huku kwa mishahara kunapelekea baadhi ya wafanya wa Kada Fulani kuwadharau wafanyakazi wa kada nyingine, lakini pia no uharibifu wa pesa kwani kama MTU yule yule (mwalimu) analipwa 20000 na naweza kuishi basi hata huyu mwingine (daktari) akilipwa 20000 ataweza kuishi na kutimiza mahitaji yake. sula hili siyo zuri

katika kuelekea kupanga mishahara upya serikali ifanye utaratibu wa kulinganisha mishahara kwa wafanyakazi wote kwa kutegemeana na viwango vyao vya elimu yaani wenye elimu ngazi ya shahada mshshahara wao ulingane, hali kadhalika ngazi ya diploma na cheti.

By mkulima wa nyanya
 
kama ni kweli wamefikia hatua ya kupanga mishahara basi ushauri wako ni mzuri sana!
 
jamani vitu vingine tuwe tuna uliza wenyeji mwalimu wa ngazi ipi Tanzania analipwa mshahara wa laki mbili mbona mnapenda kuona kama walimu ndio watumishi hohe hahe kwa kila kitu

Hivi mnajua Kuna walimu wanachukua mshahara milioni moja yani hiyo milioni ni yake hapo makato yote yamefanyika

Hivi mnajua katika watumishi wa umma ukiweza tatu bora mwalimu hawezi kukosa kuwa na mshahara mzuri ukitofautisha na idara nyingine

Tatizo walimu wamejaa uchoyo na unafiki ndio maaana wanaoneka hawana kipato wanaogopa kusema wapo vizuri kiuchumi kwakujua wataobwa au kukopwa
 

Mimi nimetoa mfano, sijasema kuwa mwalimu analipwa laki mbili
 
Unadhani inawezekana hivi changamoto za idara ya afya unaifananisha na idara ya elimu?

Ufananisho huu unatumia hoja ipi Mkuuu

unaongea usivyovijuwa, kila idara INA changamoto zake na huwezi kusema kuwa idara ya afya ina changamoto nyingi kuliko zilizoko idara ya elimu, hauko siliazi
 
unaongea usivyovijuwa, kila idara INA changamoto zake na huwezi kusema kuwa idara ya afya ina changamoto nyingi kuliko zilizoko idara ya elimu, hauko siliazi
Nipokwambia unielezee nilihitaji hoja wala sio mipasho

Hivi unajua kwanini madaktari walihitaji chanjo hepatitis?

Huu ni mfano Mdogo tuuu
 
unaongea usivyovijuwa, kila idara INA changamoto zake na huwezi kusema kuwa idara ya afya ina changamoto nyingi kuliko zilizoko idara ya elimu, hauko siliazi
Kuna vitu vingine vinachekesha kweli dunia mzima haupo huo utaratibu mtu na MMED yake ya neurology anachambua ubongo kama mchele amekaa darasani miaka 9 eti alipwe sawa na mwalimu wa civics form one, NONSENSE.
Ukiona sehemu wanalipa vizuri hamia huko.
 
Ndio maana nauliza hapa maana kuwa daktari kunahitaji usome kwa miaka sita mitano chuoni

Unalinganisha na degree ya miaka mitatu
 

ukiona mshahara haukutoshi kwa kuwa eti unafanya kazi ya kuchambua ubongo, kaa nyumbani usubiri kuchambua ubongo Wa wanafamilia yako
 
Lakini hapa Kuna kitu umesahau, mazingira ya kazi. Mfano daktari si sawa na mhandisi, sijui hapo unaelewa..!!? Mazingira ya kazi ndo yanayoleta mshahara. Kwa mfano kazi za utabibu ni hatarishi "risk", tumeshuhudia wengine kuambukizwa magonjwa kama ukimwi, halafu wengine wanavuta sumu kutoka kwenye zile dawa,
Kuna mashirika ya serikali yanayofanya kazi na watu wa mataifa mbali mbali, mfano viwanja vya ndege, bandari, hawa wanafata sheria za kimataifa kama IMO na zingine (tena sheria hizi huwataka watu walipwe kwa hela za kigeni). Kuna sehemu kazi zinafanyika saa ishirini na nne wakati sehemu zingine kazi ni nusu siku. Sasa hapo wanalipwaje? Tujaribu kuangalia nchi za jirani, mimi naomba tuwe tunajifunza kwa wenzetu (benchmarking). Tusilete siasa kwenye kazi au kufanya kazi kwa mihemko. Naomba uliyeleta uzi huu, urudi nyuma kisha ufanye tafiti Kisha utuletee mrejesho.
 
angalia mwalimu anafanya kazi masaa mangapi kwa wiki linganisha na daktari af urudi utuambie vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…