Kuelekea kupanga mishahara upya; Mishahara ilingane kwa kada zote

Kuelekea kupanga mishahara upya; Mishahara ilingane kwa kada zote

Bora wafanye hivo maana kuna vitaasisi vinajipangia mishahara wakati kazi hata hakuna kazi wanayofanya ambayo ni kubwa kuzidi wengine, pia itaondoa jeuri
 
Kila MTU atalipwa anachostahili,,ukitaka mshahara wa daktari au injinia rudi shule kasomee uinjinia uone ugumu wake then ndo uje ulipwe,tukifanya kama unavyotaka nchi hii haitakuwa na wataalamu,wote watajazana ualimu sababu yann kujitesa kusoma misomo migumu ilhali nakuja kulipwa sawa na mwalimu
 
toa mfano unaoeleweka sasa alafu unajua Kuna kitu miye huwa nashangaa sana watu wote waodharau walimu ambao wapo secta tofauti na uwalimu wengi wao wazazi wao ni walimu

Yani huu ni utafiti ulio wazi hakuna secta ya utumishi wa umma au nje ya utumishi wa umma ambayo watumishi wake wanaojitahidi na kuhakikisha watoto wao watapata elimu bora kama walimu

Walimu ndio wanaongoza kuwa na watoto madaktari , injinia, wahasibu, mahakimu nk ila ajabu hawa watu wanadharau walimu sasa unajiuliza hivi hiyo kazi ingekuwa ina tatizo mzazi wako aliwezaje kukosomesha

Ukibisha wewe ingia tasisi yoyote sema jamani wale watumishi ambao wazazi wao ni walimu wandike majina hapa Kuna offers ya inakuja utaona asilimia tatu watakuwa watoto wa walimu

Tusidharau walimu jamani wapo vizuri sema wengi wao hawatambui hilo
Hakuna aliyedharau mwalimu sema wenyewe wanajidhalilisha,wanaonesha wazi kuwa kichwani hamna kitu na ndio mana wanasiasa wanawatumia sana hadi kuwadekisha madarasa
 
Bora wafanye hivo maana kuna vitaasisi vinajipangia mishahara wakati kazi hata hakuna kazi wanayofanya ambayo ni kubwa kuzidi wengine, pia itaondoa jeuri
Uzembe wa walimu unaanzia tangu shuleni,wakati wenzenu wanapambana kusoma kwa bidii wawe ma injinia au madaktari au wahasibu nyie mnacheza,,halafu mnataka mje kulipwa sawa,haiwezekani hiyo kitu
 
Haha et mwalimu alipwe sawa na Polisi acheni mambo ya kitoto....
 
unaongea usivyovijuwa, kila idara INA changamoto zake na huwezi kusema kuwa idara ya afya ina changamoto nyingi kuliko zilizoko idara ya elimu, hauko siliazi
pamoja na hayo, Mimi nipate Div one ya pcb, nilikuwa nakesha nasoma wewe na HKL yako miguu juu umelala bwenini, nije chuo kikuu nisome 6yrs na msuri mnene, kupasua maiti na kadhia zote ndo Napata registration ya udactari, wewe miguu juu unasoma 3yrs ushapada degree yako ya ualimu, tena ya discussion tu kwenye vimbweta.
bado kazini niitwe hata usku wa manane kuwahudumia watu,sina sikukuu wala jumapili, wewe saa 9 alasiri ushafunga ofisi mpaka kesho na ni weekdays tu.

Alaf tuajiliwe na kulipwa mshahara sawa???? hell no. tinaenda private kama noma na iwe noma.

dactari lazima alipwe mshahara zaidi ya mwalimu, tusipofanya hivi tutawakosa madactari maana kutakuwa hakuna haja kuumia na masomo miaka yote hiyo alaf tulingane mshahara na mwalimu aliyesoma bila kuumia sana. wote tuwe waalimu tu.. alaaah.
 
Kuna vitu vingine vinachekesha kweli dunia mzima haupo huo utaratibu mtu na MMED yake ya neurology anachambua ubongo kama mchele amekaa darasani miaka 9 eti alipwe sawa na mwalimu wa civics form one, NONSENSE.
Ukiona sehemu wanalipa vizuri hamia huko.
we hujui taifa bila walimu hakuna cha kuwepo daktari wala nani we ki la za
 
mwalimu sa 2 asubuh had sa 8 mchana masaa 6
6x5 (j3 mpk ijumaa) =30 hrz per week
ana likizo nne kwa mwaka midterm 2 terminal 2
daktari: saa 2 hadi saa10 masaa 8 8x7 (j3 hadi j3) =56 hrz per week likizo moja tu kwa mwaka mwez m1 ,bado night calls
mwalimu ataongea na wanafunzi wake 100 kwa mara moja wote anawafundisha kitu kimoja atondoka, daktari ataongea na watu 100 mmojammoja kila mtu akiwa na tatizo lake

kama kuna kingine uliza

1. Nani kakwambia likizo za wanafunzi pia ni za walimu?

2. Nani kakwambi walimu wanaingia saa mbili asubuhi na kutoka saa nane mchana?

3. Hivi wewe umesoma shule gani ya ajabu namna hiyo?

NB; Mimi nilisoma shule ambayo Mwl wa Math na Phy ni mmoja tu, na anafundisha shule nzima na bado ni mkuu wa shule!!

ONYO KALI: Usilete mifano ya walimu wa ST.Merry, ST Francis, FEZA nk!!
 
mwalimu aliyepata div 3 au 4 akaungaunga na kupata degree alingane na pharmacist au ddaktari aliyepata div 1 six..kisa tu wote eti wana degree! ridiculous!
halafu hiyo one ya huyo daktari imetoka kwa haohao unao waita wameunga unga elimu yao this is something to lough at.
 
Waipange upya ila isilingane kabisa kuwe na katofauti kadogo hata ka elf 60 kuna watu wanakofanya kazi Mungu awasaidie tu japo kwa sasa tofauti ni kubwa
 
kwa nini mkuu? harafu mi sijajiegemeza sana kwenye mishahara ya madaktari maana mishahara yao haitofautiani sana na ya walimu labda kwa wewe unayeisikiliza vijiweni
Nani kasema haitofautiani sana, acha kujipa moyo wewe, DAKTARI MWENYE DIPLOMA TU ANAKULA PESA NDEFU KULIKO MWALIMU MWENYE DEGREE
 
mwalimu aliyepata div 3 au 4 akaungaunga na kupata degree alingane na pharmacist au ddaktari aliyepata div 1 six..kisa tu wote eti wana degree! ridiculous!
Acha ushamba kwani hakuna walimu wenye div1? Usiropoke vitu usivokuwa na maarifa navyo nikweli mwalim halingan na dactar lkn div sio kigezo hii ni dalili ya ulimbukeni
 
Bora wafanye hivo maana kuna vitaasisi vinajipangia mishahara wakati kazi hata hakuna kazi wanayofanya ambayo ni kubwa kuzidi wengine, pia itaondoa jeuri
Jipeni Moyo mishahara ya MUHIMBILI ifanane na mishahara ya majani ya chai sekondari
 
Naona watu wengi mnachangia kwa mihemko na kishabiki zaidi huku kila mmoja akidharau idara ya mwenzake.....ni kweli huwezi linganisha changamoto za idara ya afya na elimu,zinatofautiana sana ila sasa jiulize watu wote wakiwa madaktari nani atakuwa mwalimu?and vise versa
 
Naona watu wengi mnachangia kwa mihemko na kishabiki zaidi huku kila mmoja akidharau idara ya mwenzake.....ni kweli huwezi linganisha changamoto za idara ya afya na elimu,zinatofautiana sana ila sasa jiulize watu wote wakiwa madaktari nani atakuwa mwalimu?and vise versa
Sasa kama wapo waliokubali kuwa walimu kwa nini watake kulipwa sawa na madaktari?
 
Siasa ya ujamaa inayoongelea usawa inasema kuwa kila mtu anatakiwa kulipwa kwa kadri ya jasho au kazi yake.Malipo hayatakiwi kulipwa sawa kwa sifa za makaratasi tu walizonazo wafanyakazi bali kwa kazi wanayofanya.

Tuanze kwa mfano mdogo
1.Afisa masoko aliyemaliza digrii UDOM na mwingine kamaliza digrii UDSM.Wamesoma na kumaliza siku moja mmoja anapelekwa Shirika la ndege la ATCL mwingine anapelekwa TANAPA.Yule wa ATCL analala tu anakoroma ofisini hahangaiki kutafuta wateja ndege inaondoka bila abiria na shirika linapata hasara mfulululizo sababu ya uzembe wa kutochapa kazi kwake na kusababisha Serikali kutoa ruzuku.Huyo aliyepelekwa TANAPA anachapa kazi idadi ya watalii inaongezeka shirika linapata faida kubwa hadi kulipa gawio kwa serikali kutokana na juhudi zake.

Hao watu wawili ukiwalipa kwa sifa tu za vidigriii unalea uzembe na uvivu.

2.Chukulia pia mhasibu wa benki.Toka asubuhi akiamka yeye ni kupokea na kulipa mabilioni ya pesa mfululizo hadi anapoenda kulala huwezi mlinganisha na mhasibu wa shule ya sekondari ambaye kwa mwezi aweza tu kuwa anakoroma ofisini kwa kuwa hana hela ya kupokea wala kulipa

MISHAHARA hata kwenye siasa za ujamaa hailingani kwa sifa za digrii au vyeti ni HAPA KAZI TU


Mishahara duniani kote watu wafuatao hulipwa pesa nyingi mno

Mapato ndio kila kitu iwe kwenye nchi au taasisi au kampuni binafsi.Watu walio sehemu za kusaka wateja na kuumiza vichwa kuingiza mapato MAKUBWA wawe kampuni mfano vodacom,tigo,bandari,TRA,TANAPA nk hulipwa sana.Sababu ndio injini ya ncchi kwenda.Wasipochacharika barabara nchi ikakosa mapato Wanajeshi ,Polisi hawatalipwa,walimu hawatalipwa,madaktari hawatalipwa,wabunge hawatalipwa,sekta yote ya serikali haitalipwa na nchi inaweza hata kupinduliwa kwa hilo na hata shirika laweza kufa.

Sababu iliyoua hata mashirika ya umma ilikuwa mojawapo tatizo la mishahara midogo kwa wafanyakazi wa hayo mashirika ya umma ambayo serikali iliyaweka ili yazalishe faida yaipe serikali gawio iendeshe mambo yake.Umakini mkubwa unatakiwa hasa kwenye INCOME GENERATING INSTITUTIONS ambazo huendeshwa kwa faida kubwa na kuipa gawio serikalini.Mishaghara ikichezewa huko ni hatari kwa nchi.

Chukulia kampuni kama BREWERIES ilikuwa chini ya waswahili wenye digrii kibao lakini waliokuwa wakilipwa kidogo ikaenda hadi kufikia kufa.Ilipouzwa kwa makaburu wao wakaleta wazungu watatu tu wakabaki na waswahili wale wale ila wakawapandisha sana mishahara sasa hivi breweries iliyokuwa inakufa ni mlipa kodi mkubwa wa kodi na gawio kwa serikali!! Kwa hiyo eneo la Income generating institutions KWATAKA umakini mkubwa .Kukiborongwa au kuua morali wa wafanyakazi iwe kwa kutumia kigezo cha mishahara nk ni hatari
 
Back
Top Bottom