Kuelekea kupanga mishahara upya; Mishahara ilingane kwa kada zote

Kuelekea kupanga mishahara upya; Mishahara ilingane kwa kada zote

Mimi nimetoa mfano, sijasema kuwa mwalimu analipwa laki mbili

Haina haja ya kuweka debate kuhusu mshahara wa mwalimu
Ipo wazi kwamba walimu wanalipwa pungufu ukilinganisha na sekta nyingne

Au tunataka had TWAWEZA waje ku confirm
 
Kipaumbele
1.Afya
2.Elimu
Kada nyingine entry level hiwe niwa Dip au Degree mshahara uwe sawa na treatment hiwe sawa hii itaondoa watu kukimbikia TRA au Mashirika ya umma kwa sababu itaondoa ubagizi.Only in Tanzania Diploma holder yupo TRA anamzidi mshahara Mwalimu mwenye degree anayefundisha secondary kuandaa kizazi cha sasa na baadae.Solution nikuwa na tume moja ya mshahara kwa kwa wafanyakazi wa umma na mashirika ya umma.
 
ukiona mshahara haukutoshi kwa kuwa eti unafanya kazi ya kuchambua ubongo, kaa nyumbani usubiri kuchambua ubongo Wa wanafamilia yako
Nani kasema haunitoshi na hata usiponitosha kuna overtime, night, calls, procedures, bima, part time hapo sijazungumzia clinic, unajua MMED anakula ngapi serikalini?.... ni mishahara ya miezi 5 ya mwalimu mwenye degree, intern doctor tu wanakula 1. 2M yaani katoka tu MD 5 hata leseni hana, halafu ninyi muliofeli na kushindwa kusoma udaktari na pharmacy wengi wenu ndio walimu, munakuja kutusumbua na visredi vyenu vya kipuuzi, nani alikukataza kugonga one six ukachue jiwe lako la MD pale MUHAS pengine ungekuwa una superspeciality in hepatogastroentelogy sasa unakula zaidi ya 5M/months.
Una hoja za kitoto ulipaswa kutoa huo ulinganifu wa changamoto wa hizi kada

Huwezi kufananisha changamoto idara ya afya na idara ya elimu
 
Akili za mwendokasi hizi. Mbona hujiulizi kwanini bei ya vitabu vya Biology na Physics au zaidi vitabu vya medicines ni tofauti? Je tuition fee ya shahada za udaktari sawa na zile za History? Na mbona hupendekezi wote wasome miaka 3 undergrts kama BA kiswahili?
 
Nani kasema haunitoshi na hata usiponitosha kuna overtime, night, calls, procedures, bima, part time hapo sijazungumzia clinic, unajua MMED anakula ngapi serikalini?.... ni mishahara ya miezi 5 ya mwalimu mwenye degree, intern doctor tu wanakula 1. 2M, halafu ninyi muliofeli na kushindwa kusoma udaktari na paharmacy wengi wenu ndio walimu poor you

hoja yako ya kipuuzi, kwani kwenye afya hakuna wanaoungaunga mpaka ngazi ya degree au masters?
 
angalia mwalimu anafanya kazi masaa mangapi kwa wiki linganisha na daktari af urudi utuambie vizuri

katika watu wanaofanya kazi kwa muda Mdogo ni hao unaowasemea. kazi zao ziko kwa zamu, anaweza kwenda SAA sita mchana akatoka SAA kumi na mbili/ SAA mbili usiku. sasa hayo Massa unayoyasemea no yapi?
 
Mimi nimetoa mfano, sijasema kuwa mwalimu analipwa laki mbili
toa mfano unaoeleweka sasa alafu unajua Kuna kitu miye huwa nashangaa sana watu wote waodharau walimu ambao wapo secta tofauti na uwalimu wengi wao wazazi wao ni walimu

Yani huu ni utafiti ulio wazi hakuna secta ya utumishi wa umma au nje ya utumishi wa umma ambayo watumishi wake wanaojitahidi na kuhakikisha watoto wao watapata elimu bora kama walimu

Walimu ndio wanaongoza kuwa na watoto madaktari , injinia, wahasibu, mahakimu nk ila ajabu hawa watu wanadharau walimu sasa unajiuliza hivi hiyo kazi ingekuwa ina tatizo mzazi wako aliwezaje kukosomesha

Ukibisha wewe ingia tasisi yoyote sema jamani wale watumishi ambao wazazi wao ni walimu wandike majina hapa Kuna offers ya inakuja utaona asilimia tatu watakuwa watoto wa walimu

Tusidharau walimu jamani wapo vizuri sema wengi wao hawatambui hilo
 
Akili za mwendokasi hizi. Mbona hujiulizi kwanini bei ya vitabu vya Biology na Physics au zaidi vitabu vya medicines ni tofauti? Je tuition fee ya shahada za udaktari sawa na zile za History? Na mbona hupendekezi wote wasome miaka 3 undergrts kama BA kiswahili?

kwa hiyo wewe kwa ushauri wako aliyesoma kwa miaka mingi basi alipwe mshahara mkubwa
 
habari wanandugu!

Nianze kwa kusema kuwa niipongeze serikali kwa nia nzuri iliyonayo ya kupitia na kupanga upya viwango vya mishahara kwa wafanyakazi wa kada zote.

kwa muda mwingi tumeshuhudia kutofautiana kwa viwango vya mishahara kutoka fani Moja kwenda fani nyingine, mfano ualimu, afya, sheria, uhandisi n.k ambapo baadhi ya Kada wamekuwa wakilipwa mishahara mikubwa kuliko wengine ingawa ukiangalia majukumu na mazingira yao ya kufanyia kazi hayatofauti sana.

kutofautiana huku kwa mishahara kunapelekea baadhi ya wafanya Wa Kada Fulani kuwadharau wafanyakazi Wa kada nyingine, lakini pia no uharibifu Wa pesa kwani kama MTU yule yule (mwalimu) analipwa 20000 na naweza kuishi basi hata huyu mwingine (daktari) akilipwa 20000 ataweza kuishi na kutimiza mahitaji yake. sula hili siyo zuri

katika kuelekea kupanga mishahara upya serikali ifanye utaratibu Wa kulinganisha mishahara kwa wafanyakazi wote kwa kutegemeana na viwango vyao vya elimu. yaani wenye elimu ngazi ya shahada mshshahara wao ulingane, hali kadhalika ngazi ya diploma na cheti

by mkulima Wa nyanya
Acha kufananisha DOCTOR OF MEDICINE na vitu vya kipuuzi, kwa taarifa yako tu ada ya kusoma MD pale KCMC kwa mwaka mmoja tu unasoma degree ya ualimu chuo chochote hapa TZ hadi unamaliza na chenji inabaki......... halafu eti mtu huyo aje alipwe sawa na mwalimu, SERIOUS?
"The high the investment the higher the return"
 
Haina haja ya kuweka debate kuhusu mshahara wa mwalimu
Ipo wazi kwamba walimu wanalipwa pungufu ukilinganisha na sekta nyingne

Au tunataka had TWAWEZA waje ku confirm
Sana sana Twaweza watausifia huo mshahara wa Mwalimu.Sisi tunaokaa nao ndio tunajua maisha yao,Mwalimu hana overtime,hana house allowance,hana transport na airtime allowance,hila mshara wake unakatwa PAYE, Pension,NHIF,CWT, sasa huko pension inakopelekwa kwenye hayo mashirika unayoyajua wafanyakazi wanajilipa mishahara minono na mikopo juu kutokana na pension za wafanyakazi ifike mahala tuwaonee huruma walimu wanaojitolea kufundisha katika mazingira magumu sana huku wakistaafu na kuangaikia mafao.
 
katika watu wanaofanya kazi kwa muda Mdogo ni hao unaowasemea. kazi zao ziko kwa zamu, anaweza kwenda SAA sita mchana akatoka SAA kumi na mbili/ SAA mbili usiku. sasa hayo Massa unayoyasemea no yapi?
mwalimu sa 2 asubuh had sa 8 mchana masaa 6
6x5 (j3 mpk ijumaa) =30 hrz per week
ana likizo nne kwa mwaka midterm 2 terminal 2
daktari: saa 2 hadi saa10 masaa 8 8x7 (j3 hadi j3) =56 hrz per week likizo moja tu kwa mwaka mwez m1 ,bado night calls
mwalimu ataongea na wanafunzi wake 100 kwa mara moja wote anawafundisha kitu kimoja atondoka, daktari ataongea na watu 100 mmojammoja kila mtu akiwa na tatizo lake

kama kuna kingine uliza
 
Kweli wewe ni major and complex cranial nerve

Tisha sana mkulu
 
Nipokwambia unielezee nilihitaji hoja wala sio mipasho

Hivi unajua kwanini madaktari walihitaji chanjo hepatitis?

Huu ni mfano Mdogo tuuu
Mkuu naona kama unajichanganya mwenyewe! Kwani ukimpa Daktari mshahara mkubwa ndo hataweza kuambukizwa hiyo Hepatitis? Pia mleta uzi kaelezea simpo tu tena kwa mfano kuwa kama mshahara wa mwl akipewa daktari hataweza kuishi?

Tatizo watu wanaingia deep sana kwenye suala dogo!!
 
Kuna vitu vingine vinachekesha kweli dunia mzima haupo huo utaratibu mtu na MMED yake ya neurology anachambua ubongo kama mchele amekaa darasani miaka 9 eti alipwe sawa na mwalimu wa civics form one, NONSENSE.
Ukiona sehemu wanalipa vizuri hamia huko.
Mbona kama hivyo fani nyingine zitakosa watu hv Mwl mwenye Masters ya Mwaka mmoja kwa ada ya Milioni 2 akalipwe Sawa na Daktari anaye toil kupata masters kwa miaka mitatu na ada ya Million 10 kila mwaka na pesa yenyewe kajilipia thru mikopo si afadhali kila mtu awe mwl!
 
Mkuu naona kama unajichanganya mwenyewe! Kwani ukimpa Daktari mshahara mkubwa ndo hataweza kuambukizwa hiyo Hepatitis? Pia mleta uzi kaelezea simpo tu tena kwa mfano kuwa kama mshahara wa mwl akipewa daktari hataweza kuishi?

Tatizo watu wanaingia deep sana kwenye suala dogo!!
Kuna mahali pamesemwa

Changamoto kazini kwamba zinafanana

Nimekataa Hakuna mfanano wa changamoto kati ya idara ya afya na idara ya elimu
Idara ya afya yenyewe tuuu ni changamoto achana na hizi za eneo la kazi
 
kwa hiyo wewe kwa ushauri wako aliyesoma kwa miaka mingi basi alipwe mshahara mkubwa
Sijasema wala kushauri hivyo, nilikuwa namsaidia mtoa mada aendelee kujenga "homogeneity" societies kama enzi za usoshalist.
 
Mbona kama hivyo fani nyingine zitakosa watu hv Mwl mwenye Masters ya Mwaka mmoja kwa ada ya Milioni 2 akalipwe Sawa na Daktari anaye toil kupata masters kwa miaka mitatu na ada ya Million 10 kila mwaka na pesa yenyewe kajilipia thru mikopo si afadhali kila mtu awe mwl!
Mtoa mada kavulugwa aisee,wenzake wanabadilisha fani kimya kimya huwa hawaongei
 
Back
Top Bottom