Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Kupitia uzi huu na mimi niandike pia msimamo wangu kuhusu suala hili,,

takribani mwaka sasa tangu nimejiandikisha NIDA na kupiga picha pia,,

lakini tangu nimeanza kufuatilia kitambulisho changu sijaambulia chochote zaidi ya mateso ya nenda rudi nenda rudi kila siku,, uzembe wa nani,,!?

ndipo nilipoamua kuomba angalau basi nipewe hata namba (NIN) ili angalau niweze kusajiri SIM card zangu,, Ajabu wananiambia taarifa zangu hazipo,,

Msimamo wangu ni huu,,
binafsi nimeshatimiza wajibu wangu nimejitokeza kujiandikisha kwa kufuata taratibu zote,, nina uhakika sijakosea mahali popote,,

hivyo basi naomba pia NIDA watimize wajibu wao kunisajiri kama ambavyo mimi nilivyotimiza wajibu wangu kujiandikisha,,

na siko tayari kurudia upya kama wanavyotaka wao maana ni dharau na matumizi mabaya ya muda,, nawataka wazitafute taarifa zangu hadi zipatikane walipozitupa,,


vinginevyo Selikari iwawajibishe kwa kushindwa kutimiza majukumu yao na kutusababishia usumbufu wengine,,
 
serikali hii ya wanyonge haishindwi kuzima kweli mana kama ilifungia viroba na kukubali wafanya biashara kupata hasara basi hata hapa kwenye line haigopi kupoteza kodi
 
Kupitia hekima zake mkuu wa nchi, ana uwezo wa kuongeza muda tena ata wiki tatu ili kukamilisha zoezi kwa waliosalia na hakuna wa kupinga.Sidhani kama Mh.Rais anaweza kudiriki kuwanyima wananchi wake mawasiliano huku akiziona tabu zao kwenye kuhakikisha wanajisajili mwitikio ni mzuri tu muda na changamoto nyingine ndio kikwazo kama kupotea kwa mtandao au jam.
 
Hali ipoje mtaani kwako? Je wewe unayesoma umekalimisha usajili?

Umekumbana na usumbufua/kero gani wakati wa zoezi hili?

Nani alaumiwe endapo laini nyingi zikifungiwa?

Tutegemee njia mbadala tutakayopewa baada ya laini kufungiwa? Au ndio kudandia simu ya jirani ili upate kuwasiliana?

Au tutegemee muda wa rehema kuongezwa tena?

Funguka.......
 
Hivi Wanyonge hasa ni kina nani ,ili uwe mnyonge unatakiwa uwe na vigezo gani?
 
Najiuliza sana ule msemo walio sema kwamba ukimsajiria rain mtu kwa kutumia namba yako ya nida unalipa fain milion 5 inamaa haturuhusiwi ata kusajiri rain nyingine kwaajiri ya sim ya mezan nyumban ambayo itatumika na mfanyakazi au watoto nyumban kwaajir ya taharifa binafsi endapo mzazi ana kua mbali na familia yake

Ili jambo riwekwe kiuwaz kidogo ili liwe na wepesi kidogo

Maana maisha nikidore???


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muda mwingine Wabongo hatupo makini kabisa tunawalaumu NIDA bure, hili zoezi toka limetangazwa watu walikuwa hawana muda nalo kabisa ukifika ofisi za NIDA unakuta watumishi wa NIDA wanapiga tu stori hakuna kazi ila deadline inapokaribia kila mtu yupo bize kuhangaikia na NIDA na malalamiko juu.

Mchakato wa kupata kitambulisho cha taifa umeanza zaidi ya miaka minne nyuma, Mlikuwa wapi siku zote.
Utaacha kazi watoto wale mawe,alafu huyo Bosi unaanzaje kumuaga unaenda kusajili line, wakati unaenda NIDA kwa ruhusa bahati kama siyo yako unakutana na foleni hadi unaamua kurudi kazini,Je wale wa vijijini amabako hamna hata wakala unafikiria wana pesa za kwenda Center au Wilayani kwa haraka kisa laini ya simu.
"Zoezi Endelevu"
Deadline ni leo 20/01/2020 saa 23:59 usiku kama utaratibu wa siku na saa itaheshimiwa ili wale wajamaa wetu wa tija kwa mteja wasiende mahakamani kudai tumeonewa..
"Tuko Vizuri" mabeberu wanasubiri line zifungwe walete vikwazo vya uwekezaji.
 
Back
Top Bottom