Kupitia uzi huu na mimi niandike pia msimamo wangu kuhusu suala hili,,
takribani mwaka sasa tangu nimejiandikisha NIDA na kupiga picha pia,,
lakini tangu nimeanza kufuatilia kitambulisho changu sijaambulia chochote zaidi ya mateso ya nenda rudi nenda rudi kila siku,, uzembe wa nani,,!?
ndipo nilipoamua kuomba angalau basi nipewe hata namba (NIN) ili angalau niweze kusajiri SIM card zangu,, Ajabu wananiambia taarifa zangu hazipo,,
Msimamo wangu ni huu,,
binafsi nimeshatimiza wajibu wangu nimejitokeza kujiandikisha kwa kufuata taratibu zote,, nina uhakika sijakosea mahali popote,,
hivyo basi naomba pia NIDA watimize wajibu wao kunisajiri kama ambavyo mimi nilivyotimiza wajibu wangu kujiandikisha,,
na siko tayari kurudia upya kama wanavyotaka wao maana ni dharau na matumizi mabaya ya muda,, nawataka wazitafute taarifa zangu hadi zipatikane walipozitupa,,
vinginevyo Selikari iwawajibishe kwa kushindwa kutimiza majukumu yao na kutusababishia usumbufu wengine,,