Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Habari: Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu Cha Sokoine Dkt. Silvery Ishuza ameshauri serikali kusitisha zoezi la kufunga namba za Simu ambazo hazijasajiliwa kwa kutumia alama za vidole ili kuepusha mdororo wa uchumi unaoweza kujitokeza.



MIMI PIA NAUNGA MKONO KAULI HII YA PROFESSOR.

Source: ITV

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
 
 
Kama Mtanzania ninapenda kujua, vipi kama nitaibiwa simu na line yangu kutumika kufanya uhalifu?

Vipi nitakuwa na kesi ya kujibu au?

Hakuna uwezakano kwamba line zetu zitakua potential target kwa majambazi?
Utaitwa police kisha utawaeleza watawakamata through gps
 
Serikali ilishasema haishauriki, ila ukiona watu kila kukicha wanazidi kutoa ushauri sambamba na kukosoa yale matendo maovu bila kujali usalama wa maisha yao basi ni kwamba watu wana nia NJEMA na taifa lao


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni muhimu kutoa taarifa polisi haraka sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Umengoa kirahisi sana...bila shaka hujakutana na changamoto ya kupotelewa na line au simu

Wengi hatuna utaratibu kwamba ukipotelewa na vitu kama hivyo unaenda polisi ghafla...Wengi wanaenda badae sana kwa lengo la ku-renew line tu
 
Naomba kujua, ni faida zipi zitakazopatikana kwa kufungia laini za watanzania milioni ishirini kwa sababu zisizo na mashiko?

Kuna watu wanaishi kwa miamala ya simu.

Kuna watu wanaishi kwa kutumia internet.

Miamala ya benki na biashara yote inahitaji simu!

Kadi za NIDA hakuna. Na simu zinazimwa!

Vitambulisho vya kura na leseni hawataki. Wanataka NIDA. Bila NIDA hakuna kusajili.

Hakuna guarantee kwamba NIDA watatoa namba upesi baada ya laini kufungwa.

Kwahiyo watu wataishi bila mawasiliano kwa muda usiojulikana mpaka pale NIDA watakapojisikia kutoa kadi na namba!

Haya yote yanafanywa kwa ajili ya nani? Kuna motive gani nyuma ya huu uovu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu watasajili tu na utashangaa kila mtu soon atakuwa na laini iliyosajiliwa. Hata mfumo wa analojia watu walipinga sana kuwa watu hawana uwezo wa kununua vingamuzi mara sijui nini lkn mfumo ulizimwa na hadi leo maisha yanaendelea. Mabadiliko ni threats kwa watu wengi lkn baada ya muda mchache wanazoea na maisha yataendelea kama kawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…