Leo ni siku yetu ya uhuru na ukombozi dhidi ya utumwa wa airtime na mabando. Tumeyazoea hadi yamekuwa uraibu yanatumalizia pesa vibaya. Kuna familia inatumia hadi laki mbili kwa mwezi ukijumlisha pesa zote ambazo wanafamilia hao wamenunulia mabando ya kuperuzi watsapp na youtube. Lakini kwa bahati nzuri sana, asilimia kubwa ya simu hizi hazijasajiliwa. Leo wote hawa watapata ukombozi wa kuondokana na adha hii.
Hatua hii ya kuzima simu naifananisha na kupeleka mateja sober house. Siku ya kwanza wataona shida lakini baadaye watakuja kuzoea, na wakikumbuka kiasi cha pesa walichotumia kutumikia uraibu, wanajilaumu kwanini hawakuacha mapema.
Asanteni TCRA, tupelekeni sober house kwa kutuzimia hizi simu tupone uraibu.
Kwaheri sms. Kwaheri bando. Kwaheri youtube. Kwaheri data.
Kama kupiga simu tutapiga tu, zile za lazima sana na tutatumia muda mfupi. Mbona kabla ya hizi smart phone na mobiles tuliwasiliana vizuri tu.
Miamala tutatumia wakala na fahari huduma. Na soon tutagundua hasara za kuwa na m-pesa.
Mabenki leteni kadi tuwe tunalipa kwa kadi kila mahali kama ulaya. Hizi masimu ni hasara tu.