Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Hivi hawa NIDA wangetoa vitambulisho muda unaofaa yote haya yasingetokea leo unawatwisha Watanzania mzigo si wao kwani wangesajili kwa kitambulisho cha mpiga kura kungekuwa na tatizo gani?Serikali imeweka mashariti lazima uwe na nida wakati imeshindwa kutosheleza vitambulisho mbona serikali inamwonea raia
 
Leo ni siku yetu ya uhuru na ukombozi dhidi ya utumwa wa airtime na mabando. Tumeyazoea hadi yamekuwa uraibu yanatumalizia pesa vibaya. Kuna familia inatumia hadi laki mbili kwa mwezi ukijumlisha pesa zote ambazo wanafamilia hao wamenunulia mabando ya kuperuzi watsapp na youtube. Lakini kwa bahati nzuri sana, asilimia kubwa ya simu hizi hazijasajiliwa. Leo wote hawa watapata ukombozi wa kuondokana na adha hii.

Hatua hii ya kuzima simu naifananisha na kupeleka mateja sober house. Siku ya kwanza wataona shida lakini baadaye watakuja kuzoea, na wakikumbuka kiasi cha pesa walichotumia kutumikia uraibu, wanajilaumu kwanini hawakuacha mapema.

Asanteni TCRA, tupelekeni sober house kwa kutuzimia hizi simu tupone uraibu.

Kwaheri sms. Kwaheri bando. Kwaheri youtube. Kwaheri data.

Kama kupiga simu tutapiga tu, zile za lazima sana na tutatumia muda mfupi. Mbona kabla ya hizi smart phone na mobiles tuliwasiliana vizuri tu.

Miamala tutatumia wakala na fahari huduma. Na soon tutagundua hasara za kuwa na m-pesa.
Mabenki leteni kadi tuwe tunalipa kwa kadi kila mahali kama ulaya. Hizi masimu ni hasara tu.
 
Pole. wajulishe ndugu zako kuwa huna simu kuanzia kesho. Rekodi namba zao. Ukiwamisi unaenda kwenye call box au unaazima ya jirani.

Hii itakupa nidhamu ya matumizi, utagundua matumizi yako kwa ujumla yatapungua sana. Ulishafikiria simu yako inamaliza pesa zako kiasi gani?

Shukuru Mungu kwa hii fursa ya kubana matumizi
 
Wananchi katika mikoa mbalimbali ikiwemo Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga na DSM wamemuomba Rais Magufuli awaongezee muda wa kusajili line za simu kwa njia ya vidole.

Wananchi hao wamedai kwa kiasi kikubwa NIDA ndio kikwazo cha wao kuchelewa kwani wengine wanafuatilia vitambulisho kuanzia mwezi June mwaka jana.

Source ITV habari!

My take; Serikali ya awamu ya 5 ni sikivu!
 
Website yenyewe haifunguki boss!
Juzi ilikuwa inafunguka na niliwasaidia ndugu zangu kijijini huko kupata namba zao.
Nikweli leo nimejaribu haufunguki, ila namba zinatoka.
 
We labda una mjomba wako pale NIDA. Watu tangu 2016 hawana vitambulisho wala namba, ww unasema wiki 2?
Hainaga undugu hiyo.
Ukiona wiki mbili zimepita haujapata namba yako ujue taarifa zako hazijawa submitted.
Ila wakizi submit wiki mbili ni nyingi, wiki tuu.
Watu wamejiandikisha mwezi huu wa 12 na namba zao zimetoka. Hamna undugu wala.
 
Mapato ya kutokana na matumizi ya simu ni zaidi ya tunavyofikiri...everybody (watu walau kuanzia miaka 15) has a gadget and its transacting

Nlisoma sehemu kando ya Sekta ya Madini
Telecom Industry inafuatia kwa mapato nchini

Mfano mdogo tu kila vocha kuna VAT
Hawawezi kuzima
TCRA wanaweza kuzima kwa kuwa wao hawajui mambo ya VAT Mambo ya VAT wahusika ni TRA
 
Back
Top Bottom