Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Tuko sawa
 
Watu kama nyie mmeshasajili kitamboo ila mnausoma upepo tu.

Kuna wadau shuleni ukisemaga "kusoma kuelewa kukesha mbwbwe wao wanasapoti huo msemo kumbe wanapiga msuli home wa kukesha
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninasikitika TCRA mnatoka mlikolala na kudai eti mtu akitumia kitambulisho chake kusajilia line ya mtu mwingine eti adhabu ni jela.

Hivi mnajua ujanja waliokuwa wanautumia wasajili kutumia taarifa za mtu bila ridhaa yake. Haki tena acheni kukurupuka.

Kama mngekuwa serious tangu mwanzo mngekuwa makini.
 
Haituumi kutokuwa na kitambulisho ila kufungiwa laini za simu!, Na si hivyo tu mwiba mwengine ni kuwa watakaotusajilia watawekwa jela.

Sipendi zoezi hili hasa la NIDA maana linavikwazo utadhani nchi tumekodi. Hakuna viongozi wanaotutetea! Watu wanalalamika humu uhamiaji rushwa NIDA rushwa sijui mnataka iweje!!

Haka kataifa sijui kanapelekwaje napinga na nakaidi kwa ukali wanaokwamisha zoezi la usajili kwa alama za vidole ila sipendezwi na namna Mambo yalivyo!!
 
Wale wenzagu na mimi magwiji na makonki wa kufanya tukio siku ya deadline!
Tunasikitika sana tangu jana jioni na leo jumamosi, na kesho jumapili mtandao wa kusajili simkad kwa alama ya vidole hautapatikana!

Ni rai yangu tutaongezewa muda simu zetu hazitazimwa.
Imetolewa na mwenyekiti wa!

WASUBIRI DEADLINE!!!
 

Akili ndogo mpaka lini??, Hili nalo mpaka tuambiwe kuwa ni kosa??, acheni kutupotezea mda
 
Sio tarehe 20 January tu, mpaka huu mwaka unaisha hakuna SIM card itafungiwa kisa haijasajiliwa kwa mfumo huo wa alama za vidole.

Nchi yangu naijua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…