Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Mtu unawekwa jela kivipi kwa kumsajilia mtu.
Watajuaje?

Kama nimemsajilia mtu akaenda kufanya uhalifu hapo yakinikuta ya kunikuta ndio halali.
 
Watanzania Tunanyanyaswa sana,. Machungu yako Ukiyapeleka kwenye Box la kura 2020 Napo Yanachakachuliwa.
 
Haituumi kutokuwa na kitambulisho ila kufungiwa laini za simu!, Na si hivyo tu mwiba mwengine ni kuwa watakaotusajilia watawekwa jela!!😭
Sipendi zoezi hili hasa la NIDA maana linavikwazo utadhani nchi tumekodi!! Hakuna viongozi wanaotutetea! Watu wanalalamika humu uhamiaji rushwa NIDA rushwa.. sijui mnataka iweje!!

Haka kataifa sijui kanapelekwaje!! Napinga na nakaidi kwa ukali wanaokwamisha zoezi la usajili kwa alama za vidole ila sipendezwi na namna Mambo yalivyo!!
Na nyie kijani hua mnalalamika?ni mwiko kulalamika we lumumba,endelea kusifu na kuabudu atakuja jiwe kukutetea
 
Akili za mliotangulia kucomment kabla ya hii yangu poleni. Katika zoezi la uandikishaji wa dole gumba kuna manuva mengi yamefanyika na line nyingi zimesajiliwa kwa vitambulisho vya watu bila wamiliki wa vitambulisho kujua. Bahati mbaya sijui namna ya kuattach uzi wangu uliopita ila nilishawahi kutahadharisha.

Kwa mfano wewe ulipoenda kusajili ulipoweka dole gumba ukaambiwa rudia mtandao umeyumba kumbe sio kweli bali line ingine ishasajiliwa na itauzwa kwa mtu asiye na Id ya NIDA.

Wewe bila kujua unarudia na unakamirisha usajili wako kumbe kwenye zoezi la kuambiwa rudia tena kuweka kidole kuna namba zingine mbili line zimesajiliwa na msajili anaziweka reserve baadae anauza zile line.
 
Kisaikolojia fanya haya. Kama una smartphone utaendelea na internet kwa wi fi ya mtu mwingine karib. Utaacha aina zote za mikopo ya mitandaon. Utafanya mawasiliano ya kupiga kwa internet tu bila line kwenye whasapp, viber etc. Utarudia mifumo ya kibenk kuhusu pesa hasa huduma ya cardless. Mwisho wa yote utaambulia usumbuf kias lakin kampun zitapoteza makato meng yanayokuhusu na serkali itapoteza mapato ya kodi.
...Asante kwa Kujitahidi Kuniandaa Kisaikolojia, Mkuu Rwazi1...[emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaonekana unadaiwa [emoji23][emoji23][emoji23]
Maana lazima wakutafute.
Mi nimejikuta nimesajili laini zangu zote nne, lakini nilikuwa nimepanga kususa wanifungie tu ili watu waanze kunitafuta mithili ya mtu anayetafuta ng'ombe wake aliyepotea, atatembea kuulizia kila mahali..

rombo punguzeni pombe
 
Back
Top Bottom