Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

.
3bdd2881c1c242ca900350dfd0339937.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni mtizamo wangu ambao nauleta kama tahadhari kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) juu tukio la kionevu ambalo Watanzania wanalipigia kelele lakini mamlaka zinatumia ubabe kulitekeleza.

Kwa mujibu wa TCRA, kesho kutwa ndio hatma ya line takribani milioni 20 za Watanzania kuwa hewani kwa kile kinachodaiwa kutokuwa na usajili wa alama za vidole.

Kwa mujibu wa TCRA mpaka juzi ni 53% tu ya line za simu kati ya line zote ndizo zilizosajiliwa kwa alama za vidole hivyo kitakwimu ni kama nusu ya watumiaji wa simu line zao zitafungwa mpaka watakapokamilisha taratibu.

Ningependa niwakumbushe chama changu pendwa CCM kwamba idadi ya watu ambao haijasajili line za simu kama wataamua kulipiza kisasi kwenye uchaguzi ujao kwa uonevu wakuzifunga line zao ni dhahiri uchaguzi utakuwa mgumu.

Nawakumbusha uchaguzi mkuu 2015 idadi ya watu waliojiandikisha kupiga kura ni 23,253,982 na idadi ya waliojitokeza kupiga kura kote bara na visiwani ni watu milioni 15.6.

Watu watakaofungiwa line za simu kwa makadirio ni takribani watu milioni 20, hivi hamuoni kwamba hili ni hatari hasa kwa mwaka wa uchaguzi kama huu?

CCM tambueni hili zoezi Watanzania mnaowatetea (wanyonge) ambao ndio wapiga kura ndio wahanga wakubwa kwani wengi wapo vijijini ambapo hizi huduma hazipo.

Watu wamepoteza muda wao tangu awali zoezi hili lilipoasisiwa mwaka 2014 wamehangaika na vitambulisho hivi pasipo mafanikio, wapo ambao wamediriki hata kuuza mifugo kama kuku ili kupata nauli za kwenda wilayani (NIDA) ili tu walau kupata hizo namba za NIDA lakini mpaka leo hawajazipata.

Hii dhana kwamba wananchi walipuuza hili zoezi mwanzoni sio kweli kwani sisi ndio wananchi, wapo wengi wamejitokeza mwanzoni kabisa 2014 lakini hawajapata vitambulisho, watu wamerudia tena na tena lakini hawa NIDA ni tatizo.

Tusijiamini eti tu kwasababu ya miradi kama Stiglers, ununuzi wa ndege. Hii idadi ya watu wanaoenda kuonewa tarehe 20 kwa uzembe wa NIDA inaweza kabisa ikawa tatizo uchaguzi ujao.

Watanzania hawakatai kujisajili ila ni vema wakawekewa mazingira wezeshi ili wajisajili.

SMS sent & delivered
 
Huyo Jiwe anajidanganya sana......

Kwa kuwa anaamini Tume ya uchaguzi ni mali yake.............

Anaamini pia vyombo vyote vya dola, vikiwemo Jeshi la Polisi na TISS vyote anavimiliki yeye, kwa hiyo haoni namna gani kura ya mwananchi, kupitia sanduku la kura, namna litakavyogeuza matokeo hayo
 
Nani amekuambia kuna uchaguzi huru na haki? . haupo ndiyo maana serikali inafanya inachotaka
. demokrasia imesharudi kwa mabeberu walioileta nao hawana mpango kuingilia mambo yetu ilimradi mirija haijaathirika
Tupambane na hali zetu. Chama tawala kinwwza amua wabaki na viti vinne vya machokoani mambo knisha. JK aliwapa Uhuru mkasema ni rais dhaifu naye akasema nawaletea jembe tingatinga. Tutulie miaka isonge kama MUNGU ataturudishia mstaarabu tusimdhihaki kama JK tulivyomtukana. Tumeuona upande Wa Pili Wa asiye dhaifu nchi ianavyokwenda .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zoezi linaenda holela sana mpaka vichochoroni wanasajili, usalama wa usajili ni mdogo sana kwa kweli na ukizingatia watu wana njaa Kali sana
 
Kifurushi cha data nina cha mwezi sijuwi ni fanyeje nikimalize maana kwa siku mbili walizo niambia zimebaki wafunge laini Yao siwezi kumaliza kifurushi changu! Haiwezi kuwa kesi ya uhujum uchumi!
 
Nani amekuambia kuna uchaguzi huru na haki? . haupo ndiyo maana serikali inafanya inachotaka
. demokrasia imesharudi kwa mabeberu walioileta nao hawana mpango kuingilia mambo yetu ilimradi mirija yaohaijaathirika
Tupambane na hali zetu. Chama tawala kinaweza amua wapinzani wabaki na viti vinne vya machokoani mambo kwisha. JK aliwapa Uhuru mkasema ni rais dhaifu naye akasema nawaletea jembe tingatinga. Tutulie miaka isonge kama MUNGU ataturudishia mstaarabu tusimdhihaki kama JK tulivyomtukana. Tumeuona upande Wa Pili Wa asiye dhaifu nchi inavyokwenda .

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Mtaani wanapita vijana wamachinga na maspika yao, wanatangaza "tunasajili laini kwa alama za vidole". Wanachomoa vimtambo vyao, wanakuomba kitambulisho wanakusajili. Ni nani anaweza kupreserve integrity ya zoezi?

Hivi watu wenye ajenda zao wakiwapa hawa vijana pesa na wakisajili kwa fingerprints za watu wengine zoezi hili umakini wake utakuwaje?

2. Mtandao mmoja mtu anaweza kuwa na laini hadi 5

Je mtu mmoja mwenye kitambulisho akisajili laini kadhaa na kugawa nyingine kwa ndugu, jamaa na marafiki itakuwaje?

3. Huko vijijini ndani ndani kabisa hao wanaosajili kwa alama za vidole capacity yao ya kufika huko ndanindani ikoje?

MY TAKE:
Hii nchi ni nchi ya watu masikini sana, kinachosikitisha ni kwamba pale kunapoanza kutokea mwangaza fulani hivi wa sekta fulani kuanza kuchomoza na kushine ili baadae iwe nguzo muhimu ya kiuchumi na kijamii, huwa zinatokea forces fulani kutoka kwa serikali ileile kuanza kuweka regulation ngumungumu zinazorudisha mafanikio ya wananchi nyuma. Kwa mfano:

a) Wananchi walikuwa wameshapiga hatua kubwa kweli kwenye kumiliki TV, kiufupi nyumba za wananchi wengi vijijini na mijini walishaanza kuona TV kama sehemu ya utamaduni wao. Cha ajabu serikali ikaja na mambo ya kuhama Kutoka Analojia kuja Dijitali, na kusababisha kuleta watu wa ving'amuzi kitu kilichopekekea gharama za kumiliki TV kuwa juu, na matokeo yake nyumba nyingi nchini leo hii TV ni anasa!. Watu leo hii imefikia hafua kuangalia Taarifa za habari Bar, au kuangalia mpira wa ligi yao wenyewe kwenye mabanda ya mpira!
Kiufupi base ya wananchi wamiliki TV, imeshrink mno

b) Leo tena baada ya mafanikio ya wananchi mamilioni kwa mamilioni kumiliki laini za simu, serikali ile ile yenye kawaida ya kuvuruga baada ya mambo kuanza kuonekana kukaa kwenye msitari inakuja na reguation juu ya regulation, leo inataka watu wajisajili kwa vitambulisho vya NIDA plus fingerprints, wakati inajua ipasavyo kuwa capacity ya kuprovide vitambulisho hivyo kwa kasi ni ndogo lakini pia uwezo wa kusajili hizo alama za vidole kwa kasi ya kutosha hadi kucover huko vijijini ni mdogo!
Matokeo ya hili zoezi la usajili wa laini ni ama watu wengi watacheat kwa kutokuwa na usajili sahihi au kupelekea upunguaji wa umiliki wa laini za simu, matokeo yake wamiliki simu watapungua kama ilivyotokea kwenye zoezi la TV
Mara simu fake sijui iliishia wapi, tukapata hasara, ivi kweli raia mimi ntajuaje hii ni fake au sio, kwanini Serikali kupitia TBS isizuie zisiingie, kiukweli Serikali ndo inarudisha nyuma Maendeleo ya wananchi
 
Kesho watasajili kwa kupima damu sio fingerprint tena,viongozi wenye mawazo ya ujamaa ndivo walivo kwao salama kuwatawala future less people wanaitwa wanyonge kwa kuwatengenezea umasikini ili watawaliwe kirahisi.Shida ipo tunapokosea kuchagua viongozi.
Zoezi la usajili limetumiwa na wengine wamejiongeza kutengeneza pesa kupitia changamoto za zoezi hilo.Kama wawezapata line iliyosajiliwa bila kupanga foleni hilo zoezi lina maana gani
 
Huwezi elewa we subiria hiyo tar20 watufungie cheap zetu ndio utaelewa humu jf kwenyewe wengi tutashindwa kuingia achilia mbali maswala ya kupiga simu kijijini tutarudi enzi za kusikiliza taarifa ya habari kwa m/kiti wa kijiji.
Kakudanganya nani,jf na social media zote namba za,Simu ni hiari yako.Mbona unajisajili bila hata Simu walla namba.Kumbuka hatumiliki server za hizi social media hata aliye nje ya nchi anajusajilia tu.Wakifungia tutatumia line za nje hata Kenya kutuma pesa
 
Ni vema ukajiridhisha mwenyewe kama umesajiliwa ili usije kupata mshtuko siku hiyo ya tarehe 20/01/2020.

Hivyo piga *106# kisha chagua 1 utapata uthibitisho.

Maendeleo hayana vyama!
 
Tanzania tuna tatizo la kutokuwa na sera za taifa. huduma, elimu, uchumi afya na usalama zinatakiwa kuwa sera za taifa hata aje kichaa gani angebanwa na katiba na sheria lakini aya mambo ya kufata matakwa ya mtu mmoja ndio yanatughalimu kama nchi.

Unamwambia babu wa miaka 70 akajipange foleni nida kujaza form ya kusajili line seriously? mzee atoke kijijini kwenda wilayani kutafuta namba? unakuta mtu anatembea km 50 kwa baiskeli nenda rudi nenda rudi bila mafanikio. huduma ni haki ya kila mtu kuwafungia watu lain kwanza ni uvunjifu wa katiba.
Wao ndo watakosa mapato.mawasiliano zikiwepo hata Simu mbili kijijini zinatosha wataaazimana kuwasiliana tutatumia wasap,tango,nk
 
Yaani sisi dah! Kuna kitu kweli tunaweza kukifanya kwa weledi kabisa kabisa kikaenda kitaalamu bila figisu figisu? Kwa nini inakuwa hivi lakini?

Hapa utakuta watu wameiba mpaka basi. Watu weusi sisi tuna matatizo sana wallahi.
Shida na changamoto plus njaa ya wasimamia zoezi upelekea mambo ya shortcut.Kumbuka technology haiwezi shindana na akili ya mwanadamu
 
Hili zoezi ni la kipumbavu haijawahi tokea,wataweka vipi dead line wakati si wananchi wote wana vitambulisho vya Nida?Kupata Kitambulisho chenyewe unaweza hata zimia kwenye foleni.Kwanza sidhani kama kuandikisha line ndo kitu mtanzania anahitaji ili aishi.Mtanzania anahitaji Maji safi na salama,Kazi,huduma bora za jamii kwa ujumla.
Hivi Ni sheria namba ngapi inayotamka mwisho wa kusajili Ni tar 20? Je Ni sheria ipi inayotamka kumiliki simu bila kitambulisho Cha taifa Ni kosa kisheria? Nasikia sijui Kuna kifungo Cha jela kwa kosa lipi?
 
kwa nijuavyo Mimi...... ukiangalia kwa Kina mambo matatu
  1. Kuzima simu kwa wasiosajiliwa kwa Alama za vidole kutaliingizaTaifa hasara ya mapato yatokanayo na kodi za huduma za simu
  2. Makampuni ya Simu yatapoteza Wateja na mapato pia
  3. Wale watakao shindwa kusajili kuna uwezekano mkubwa wakatumia line zilizosajiliwa na ndugu, Rafiki au watu wengine
  4. Ni zoezi Zuri kwa ustawi wa Nchi hasa kwenye mambo ya Usalama lakini limegubikwa na Changamoto kutoka NIDA....
Yote kwa yote TCRA busara itumike juu ya Jambo hili ikiwezekana uongezwe muda wa usajili.....
 
Back
Top Bottom