Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Vipi ulitabiri simu za kichina kufungwa? Vipi zilifungwa hazikufungwa? Je, ulitabiri kuzimwa kwa analog kupisha digital? Je analog ilizimwa haikuzimwa? Haya ndo mabadiliko yenyewe sasa hatuwezi kurudi nyuma, hatuwezi kuishi kizamani lazima mfumo ubadilike hata kama tumechelewa kufanya maamuzi.
Kufanya maamuzi sio kuumiza watu. Bali ni kuwaandaa kwa mipango thabiti.
Acheni kujificha kwenye kichaka cha maendeleo wakati mnarudisha watu nyuma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kesho ndo cku ya mwisho means next day ndo zinafungwa

mwanabhonga
 
Pamoja kwa 100%
Utawala huu wa Magufuli ni rahisi sana kutabiri kitu na kikatokea.
Nilitabiri Babu Seya atatoka ile December 9 2017 ikawa, nilitabiri 2019/2020 watumishi wa umma hawataongezewa hata senti ikawa. Leo narudia tena kutabiri utabiri huu mgumu kuwa line za simu zisizosajiliwa kwa namba ya NIDA kesho tarehe 20 kuelekea tar 21 hazitafungwa.
Kama unabisha tuwekeane dau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa uelewa wangu mdogo Mh Rais alisema zoezi la kusajili laini kwa alama za vidole mwisho tarehe 20, hivo bas kufungwa kwa lain ambazo hazijasajiliwa zitafungwa tarehe January 21, 2020 saa 00:00 EAT.
 
Wadau,Niko hapa maeneo ya mbagala mwanamtoti natoka kwenye pilika zangu,mpaka saa hizi naandika huu uzi ,saa moja na dakika hamsini na sita,Bado Kuna watu wamejazana katika vituo vya kusajilia laini za simu.

Mida mchache ujao tutasikiliza taarifa ya habari sijui,E-1 ataongeza muda Tena au ndo imetoka.

Hebu tuendelee kula mtori ,nyama tutazikuta chini.
Wenye updates za usajili watuletee kuitia uzi huu.

Cc,ziro iq.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa usalama wa nchi na changamoto za mtandao acha wafunge naunga hoja maaana watanzania wengi wanapenda mizaha sana ....sasa yamewakuta wanaanza lawana

Tujifunze kutii....sio ulalalmika ovyo ...
Nida gumezunguka kila kijiji /mtaa kitongoji ...lkn watu wanaoita tu wanaendelea na shughuli zao

Sasa ...meli imezama wanaaanza lawama za kijinga kwanza Tanzania tumechelewa sana ....kufanya mabadiliko haya

sent from toyota Allex
Pumbafu kweli Wewe Jamaa! Je unajuwa Mkoa wa Kigoma Wananchi walisajiliwa na NIDA Mwaka Jana mpaka leo hawajapewa hata namba za vitambulisho! Sio unafurahia na kukashifu kwasababu Mkoa unaoishi wengi mlisha pewa vitambulisho na baadhi yenu mkazembea kusajili line zenu, ukadhani Nchi nzima wamepewa hizo namba za NIDA .
 
Naibu Waziri wa wizara ya mawasiliano na uchukuzi amenukuliwa mjini Kigoma akisema kuwa watu watakao zimiwa laini za simu ni wale ambao hawajajaza fomu za NIDA kabisa lakini Kwa wale walio jaza fomu za NIDA serikali itatumia hekima katika kudili na suala Lao.
 
Kesho ni mwisho ndio muache dharau kujiandikisha NIDA ilianza tokea enzi ya Jk
 
Habari zenu wakuu
Kabla laini hazijafungiwa siku ya tarehe 20.01.2020
Ni vyema ukatoa pesa na kuhakikisha salio halibaki katika laini hiyo. Pia unaweza kuhamisha pesa katika laini ambayo ni rahisi kufanyia mihamala yako .

tufanye hivi kupunguza lawama wakuu
 
Pumbafu kweli Wewe Jamaa! Je unajuwa Mkoa wa Kigoma Wananchi walisajiliwa na NIDA Mwaka Jana mpaka leo hawajapewa hata namba za vitambulisho! Sio unafurahia na kukashifu kwasababu Mkoa unaoishi wengi mlisha pewa vitambulisho na baadhi yenu mkazembea kusajili line zenu, ukadhani Nchi nzima wamepewa hizo namba za NIDA .
Unafikiri NIDA wanatoa vitambulisho kama unagawa karanga?
 
Back
Top Bottom