Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Kuelekea laini za simu zisizosajiliwa kuzimwa; Ushauri wa namna bora ya kufanya ili kutovunja sheria za nchi

Hakuna mantiki ya kutekeleza hili la kufungia lines kwa haraka hivi. Kwanini asiwape deadline NIDA na kuwaongezea nguvu kazi & vitendea kazi ili wafanye kazi kwa weredi? Kwanini watu wasiruhusiwe kusajiri line kwa kutumia pasipoti au driving licence? Kuna madhara gani kijamii, kiuchumi, kisiasa na kiintelijensia kusogeza deadline mpaka Sepr 2025?

Sababu ni uchaguzi sio usalama
 
Ni bahati mbaya kuwa zoezi la vitambulisho vya taifa limegeuzwa kuwa ni muhimu zaidi kwa usajili wa namba za simu kuliko maana yake halisi kuwa ni Kitambulisho cha Mtanzania.

Na hii inatokana na tabia zetu za kutaka kila jambo lazima kuchomekea siasa. Kulikuwa na sababu gani kwa Rais kuliingilia kati kwa matamko kibao tena yanayopingana yenyewe wakati jambo hili wangeachiwa wataalamu wahusika mfano NIDA, TCRA na mitandao husika na lazima wangepata ufumbuzi usio na shida?

Vitambulisho vya NIDA ni muhimu kitaifa kwa usalama watu lakini kwa mtindo huu wa kusajili kwa shinikizo ili kuwahi deadline ya simu kutakuwa na uhakiki wa kweli kuwa nani anapewa udhibitisho huo wa uraia? Au wanataka baada ya miaka miwili mitatu tutumie mabilioni mengine kurudia zoezi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fact
Umewaza kama nilivyowaza mimi
Maana nzima ya uraia haipo tena bali ID ya kusajilia laini. Siasa imeingizwa pasipotakiwa siasa.

GOD is GOOD
 
Chakaza,
Tena wamezalisha tatizo lingine kubwa zaidi, kwa wananchi kutumia vitambulisho vya wengine, ili mradi tu wawahi ile "deadline" ya tarehe 20/01/2020 ya kuzizima simu zote

Tatizo linajulikana wazi kuwa lipo NIDA kutokana na kutowwza kumudu idadi ya watu wanaojitokeza sasa kwa ajili ya kuwahi kusajili simu, sasa iweje adhabu ya kufungia simu aibebe mwananchi wa kawaida?

Ngoja wazime hizo simu, halafu waone hiyo "impact" yake kwa serikali kukosa mabilioni ya pesa kila siku, kutokana na "transactions" nyiingi za pesa zinazofanyika kwenye mitandao ya simu
 
Kama umesajili line yako na bado unasubiri taarifa confirmation au bado hujasajili naona baadhi yetu tumeanza kuonja joto la kuzimiwa mtandao.

Si mimi hata jamaa yangu hapo Dar hapatikani, nimetumia njia mbadala kwa kupitia jamaa wa ofisini kwake ndipo akaniambia yupo ofisini.

Sijaelewa kama ndiyo wamefanya yao au wanatest mitambo, mdau huko ulipo vipi upo hewani?
 
Hakuna kitakacho fungiwa ondoeni hofu waTanzani
 
Back
Top Bottom