Pre GE2025 Kuelekea Machi 8 , Wanawake wasipewe nafasi za Uongozi/Kiutendaji Kwa sababu ya Jinsia yao!!

Pre GE2025 Kuelekea Machi 8 , Wanawake wasipewe nafasi za Uongozi/Kiutendaji Kwa sababu ya Jinsia yao!!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2017
Posts
25,725
Reaction score
78,589
Ndio unaweza niita Mkoloni au Mfuasi wa Mfumo Dume , Vyovyote vile iwavyo, ukweli ni kwamba, Kuna Nafasi za Kiuongozi na Kiutendaji hazitakiwi kupewa Wanawake Kwa sababu tu ni Wanawake !!.

Badala yake ni Lazima Wanawake wao wenyewe kuonyesha Uwezo na uthubutu wao Kila sehem waliyopo ili waonekane , Ukifanya kazi yakutukuka unaonekana tu .

Kwa mfano, Waziri Dkt Gwajima D, Mama yetu huyu aliibuliwa rasimi na Hayati Dokta Magufuli , si Kwa sababu ya Jinsia yake Bali uchapaji wake wa kazi akiwa kama Daktari.

Tunahitaji akina Dkt Gwajima , RC Sendinga , Mbunge Msambatavangu , Catherine the great , Condeleeza Rice, Cleopatra , Indra Gandhi, Angel Merkel n.k

Wakati fulan jaribio la kuuwawa Kwa Trump, yule Mwanamama Mkurugenzi wa SS , akihojiwa mbele ya Bunge , mule Ndani Wabunge Wanawake walimhoji ,walimuuliza, walielezea Kwa Uelewa mkubwa, wakijiamini kiasi kwamba Mwanamama akabaki kulia lia.

Soma Pia: Pre GE2025 - Kipindi hiki cha Uchaguzi wanawake wanapata nafasi ya kutosha kushiriki kwenye masuala ya uchaguzi?

Hao ndio Wanawake tunaowahitaji katika Nafasi za Kiuongozi na Kiutendaji.

Haingii Akilini Mwanamke apewe Nafasi hizo Kwa sababu tu ni Ke na anauwezonwa kusema "CCM hoyeeeeee, mama anafaa mitano tena" .

Popote pale panapoongozwa na mwanamke Dhaifu, Huwa panaharibika kwelikweli iwe ni kiuchumi, kijamii, kitamaduni, kisiasa n.k.

Lazima tuukwepe Huu mtego wa Kishetani unataka Wanawake wapewe nafasi za Kiuongozi na Kiutendaji Et kisa ni Wanawake.

Wanawake waendelee kupewa fursa za kusomeshwa , kutiwa nguvu ,kuwezeshwa lakini kwenye suala la nafasi hizo ni lazima waonyeshe UWEZO WAO.
 
Mimi nashauri Tanzania maisha yaendelee haya maswala sijui wanawake nini hapana. Mwanamke akipata nafasi unyama, akiwa hivi unyama. Wasipewe priviledge kiivo.
 
Back
Top Bottom