mjingamimi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2015
- 42,209
- 51,004
Huo ujumbe.
Umeandikwa na matapeli wa ccm.
Zanzibar bado ni koloni.
Umeandikwa na matapeli wa ccm.
Zanzibar bado ni koloni.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
![]()
Mbona huyo wapili kutoka kushoto anaonekana kachanganya damu?
Sasa kama waarabu walikuwepo kabla ya Sultan Seyyid Said kuja, hao (waarabu) waliomkaribisha walitokea wapi?Ndio maana yake, kwani aliechanganya damu anaitwa nani?
Bila shaka itakuwa mchanganyiko wa Mwarabu na Mwafrika,
kwa maana hiyo wale wanaosema kuwa kulikuwa na Ubaguzi wakati huo sio kweli kwani watu walikuwa wanaowana wana zaana bila ya kijali rangi ya ngozi zao
Katika hii picha huyu jamaa alievaa kilemba na koti jeusi ni mwarabu, huo ndio muonekano wa waarabu wa Oman
Mkuu, Warabu walikuwa wafanya Biashara Wakubwa, walikuwa wakiangaika na majhazi yao bahari yote ya Hindi kabla hata Mzungu kuanza kufanya hivyo..Sasa kama waarabu walikuwepo kabla ya Sultan Seyyid Said kuja, hao (waarabu) waliomkaribisha walitokea wapi?
Zanzibar kama ikiwa chini ya Oman wazanzibar wataneemeka sana na shida itakua ndio mwisho...na kwa mahusiano tuliyonayo hata bara tutanufaika sana...shida hapa ni siasa..means hapa znz itakua kama visiwa vya mayyote vilivyo chini ya mfaransa mambo shwari
Dola ya kilwa ilivunjika takriban miaka 500 kabla ya Sultani Seyyid kuja Zanzibar sasa atakuwaje kuwa ametokea Kilwa?Mkuu, Warabu walikuwa wafanya Biashara Wakubwa, walikuwa wakiangaika na majhazi yao bahari yote ya Hindi kabla hata Mzungu kuanza kufanya hivyo..
Historia inasema kabla ya Sultan Saidi kuhamia Zanzibar makaazi yake yalikuwa KILWA..
Kabla ya Sultan Said kuamua kuhamia Zanzibar, tayari Zanzibar ilikuwa na mchanganyiko wa Wageni ambao walikuwa wamefanya makaazi na waliokuwa wakipita njia kama wafanya Biashara
Walikuwepo Wachina, Wahindi, Warabu, Wasomali na Waafrika hasa makabila ya pembezoni ya Tanganyika, Wazaramo, Wadogo, Wasegeju, nk. Zanzibar ilikuwa cosmopolitan, ilikuwa na Mchanganyiko wa watu na makabila
Sayd Said alipokelewa na Warabu, Wahindi, Wachina, Waafrika hao wote walikuwa na jina moja ambao ni WAZANZIBARI
Vile vile na. Yeye Sayd alipohamisha makaazi yake kutoka KILWA na kuhamia Zanzibar alihamia na watu wengi wa makabila ya kusini hasa hawa wa kabila la WAYAO..
Hivi sasa CCM inajinasibu kuwa Zanzibar ni ya watu weusi tu, UBAGUZI umewajaa kwenye damu zao
Ilivunjika vipi? Mkuu unajua maana ya Usultani au Ufalme?Dola ya kilwa ilivunjika takriban miaka 500 kabla ya Sultani Seyyid kuja Zanzibar sasa atakuwaje kuwa ametokea Kilwa?
Navyofahamu alitokea Muscat moja kwa moja kutumia zile pepo za mansoon.
Hao wachina ulioongelea waliokuwa wakifanya biashara walifanya hivyo zamani sana kwenye karne ya 11. Walipokuwa wanakuja kufanya biashara ya dhahabu Kilwa iliyokuwa ikitoka ufalme za Zimbabwe. Sasa utakuwa unachanganya historia kumuweka Sultan na Dola ya Kilwa.
Sio Truth and Reconciliation Commission na Oman, ni Truth and Reconciliation Commission ya kuzipatanisha pande mbili zinazosigana Zanzibar kuhusu yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya 1964, waliofanya mapinduzi yale wanajitapa ndio ukombozi wa Mzazibari dhidi ya ukoloni wa Mwanarabu chini ya Sultani dhalimu, waliopinduliwa, walifanywa vibaya, kuna watu waliuliwa kinyama na kufanya kila aina ya vitendo vya kikatili, hivyo wako watu wangali na makovu ya mapinduzi yale, wakiyaita ni mauaji ya kimbari ya Waarabu. Ili Zanzibar is stabilize, kiukweli kabisa Truth and Reconciliation Commission inahitajika, kama ilivyofanya GNU, ni kuwaleta pamoja tuu, lakini watu walikuwa ndani ya GNU huku wana makovu na visasi, ndio maana Mwarabu kila siku anashinda na hapewi kwa kuhofia retaliation, lazima kwanza Wazanzibari msemezana na muambiane ukweli wa kilichotokea ile 1964, msameheane, ndipo muelewane na kwenda pamoja. Amini usiamini, usalama na amani ya Zanzibar imeshikiliwa na huu muungano adhinu tuu, bila hivyo mgechinana mpaka basi!.
P
Katumwa na CCM huyoHili wanalosema watetezi wa Waarabu kuwa eti Zanzibar ilikuwa haina mwenyewe kabla ya kuja wa Omani haingii akilini
Kuvunjika/kuanguka kwa dola inamaana waliokuwa wakiendesha himaya (washirazi) walishindwa kuiendeleza kama zamani. Hata sarafu yake haipo tena kwakuwa dola hiyo ilianguka. Waarabu na wareno walipokuja Kilwa walikuta himaya hiyo haipo tena, ndiyo maana waliweza kuikalia walivyotaka.Ilivunjika vipi? Mkuu unajua maana ya Usultani au Ufalme?
Utawala wa kisultani au wakifalme kufa kwake ni kuuuwa ukoo wote au kuwamisha sehemu moja kwenda nyengine..
Mkuu, inategemea ni historia gani unaypisoma, kwani Kilwa imewahi kutawaliwa na Washirazi mwaka 956 mpaka 1277
Wakaja Waajemi 1277 mpaka 1495
Kuanzia hapo Kilwa ilianza kukaliwa sio kutawaliwa na vikundi tafauti, Warabu Wareno nk, ilikuwa wakati wa mwenye nguvu mpishe..
Sasa mwenzangu sijui unazungumzia historia ipi??au dola ipi?
U may be right.The best way forward to heal the scars of1964 Zanzibar revolution trauma, is the establishment of peace and reconciliation commission like the one of post apartheid South Africa led by Bishop Desmond Tutu.
Sasa wewe unaongelea dola ipi iliyovunjika miaka 500 kabla kuja Sultan Sayd Said?, ya Washirazi, ya wa Yemeni, au ya Sayd Said..Kuvunjika/kuanguka kwa dola inamaana waliokuwa wakiendesha himaya (washirazi) walishindwa kuiendeleza kama zamani. Hata sarafu yake haipo tena kwakuwa dola hiyo ilianguka. Waarabu na wareno walipokuja Kilwa walikuta himaya hiyo haipo tena, ndiyo maana waliweza kuikalia walivyotaka.
Mkuu, Watanganyika na vibaraka vyao walivyovipandikiza Zanzibar wana siasa za kibaguzi sana, wameirejesha Zanzibar nyuma kimaendeleo, wameleta chuki baina ya Wazanzibari..Tatizo hapa la mchanganyiko wa waafrika na waarabu kubaguana,limetoka Tanganyika,
Wazanzibari wenyewe hawalijuwi hilo,ndo maana wanaodai kuulinda Muungano kwa nguvu ni Watanganyika ,
Waenezaji wakubwa wa propaganda ya Utumwa na ukatili wa waarabu ni Watanganyika,
Huku zanzibar hata baada ya mapinduzi kuwisha, waarabu walishirikishwa kwenye shughuli mbali mbali za kinchi,na walitambulika kuwa ni wazanzibar bila ya kuwabagua KARUME HAKUENDEKEZA SANA UBAGUZI ,Lakini kuna Watu wenye asili ya kutoka Tanganyika ndo walikuwa wakileta madhara ya ubaguzi hadi hivi leo.
Sijui kama Munajuwa kuwa Katibu wa ASP alikuwa Mwarabu?
Zanzibar ilikuwa marufuku kusomesha somo la historia hasa ile ya Utumwa na kurudisha machungu.
Ni Tanganyika ndowalotuletea miaka ya karibuni somo hilo, wametuletea Habari hizi ili Kueneza chuki ili wao watimize mradi wa wao wa 'DIVIDE AND RULE'
KUHUSU OMAN KUSAIDIA ZANZIBA
Omani Ilitaka kuijenga Bandari Kubwa ya Zanzibar hivikaribuni lakini Tanganyika imekataa kuidhinisha Mradi Huo.
Nadhani haya yako wazi,Lilisemwa dani ya baraza la wawakilishi ,
Bora niache tuu
lakini Omani haina interest yoyote ya kuja kutawala Zanzibar,kwani hawana sababu,wala hakuna cha kuwavutia hapa,ila wao wanatuhurumia sisi kwa kuwa ni Ndu zao wa damu na walitamani na sisi tuwe na Neema kama wao lakini Tanganyika Inaweka Kauzibe.
Semeni ukweli musitafute kichaka cha Utumwa na Uarabu.Muna lengo gani na Zanzibar?
Historia Ilikwisha zamani Mataifa yote duniani yana sehemu ya Historia Mbaya,Lakini Kioja ni hii ya Zanzibar tuu.?
Ila iwe Dhambi Zanzibar tuu kushirikishwa Utawala mtu mwenye damu tuu ya Kiarabu?
Semeni Agengda yenu?
Hata Huyo Karume alijiolea Chotara wa Kiarabu na Kihindi ili kuondoa Fitna,
Lakini watanganyika ado tuu kila uchao wanatuchonganisha Wazanzibari ili tuozane.
Namkumbuka Myere aliposema Kuna Upemba Na Uunguja, Yeye alikuwa wa kwanza kulisema neno lile.Hatimae Salimini akaendesha siasa za Kibagizi kwa kuwatowa watu kazini kwa Mfano ule wa Nyerer.
Tena Mkapa akasema Machotara hapa si kwao,Wakome vijukuu vya Masultani, Picha ndo hiyo hapo juu uchaguzi ulopita.
Sijawahipo kumsikia Dr.Sheni kutowa kauli za kibaguzi ,wala Mzee Mwinyi Wala Mzee Wkili, Wala Jumbe,
Semeni Ukweli wenu Watanganyika Muna Aajenda ya Siri!
Acheni Ubaya huooooooo.
Waznzibari ni Watu mchanganyiko wa damu za kishirazi,ki Afrika, kiarabu ,Kichina,na Kihindi wenyewe tunajuwana wala hatubaguani,Tuna sali pamoja,tunaowana,tunafanya shughuli zetu zote pamoja bila ya Bughudha, na hili ndo lilikuwa lengo kuu la Mapinduzi kama hamujuwi.
lakini Watanganyika Mumetushika, Hebu tuacheni Tupumue.
Anapambania kuwa daraja la pili kwamba wakija atakuwa atakuwa chini ya meza kuokota makombo,nashangaa hao waafrika weusi tiii sijui watakuwa wapi.Ndugu zangu tumbo halijawahi mkomboa mtu zaidi ya kumtia utumwaniMaalim seifu sharifu aka the separatist anapenda hata kesho warudi anawapendi kuliko weusi kama we
State agent
The word Zanzibar came from Arabic zanjibār (زنجبار [zandʒibaːr]), which is in turn from Persian zangbâr (زنگبار [zæŋbɒːɾ]), a compound of Zang (زنگ [zæŋ], "black") + bâr (بار [bɒːɾ], "coast"), cf. the Sea of Zanj. The name is one of several toponyms sharing similar etymologies, ultimately meaning "land of the blacks" or similar meanings, in reference to the dark skin of the inhabitants.Hili wanalosema watetezi wa Waarabu kuwa eti Zanzibar ilikuwa haina mwenyewe kabla ya kuja wa Omani haingii akilini