Mr Tyang
JF-Expert Member
- Sep 30, 2018
- 1,728
- 6,806
Mkuu ndo maana nikatumia neno "kikosi" na siyo usajili.Lakini mkuu we unaona usajili mpya wa Yanga utaweza ku perform kwenye Mechi kubwa kama hii ya daby Kama wameshindwa kuperform kwenye friendly Mechi juzi na Vipers?
Asilimia kubwa ya vikosi vitakavyoanza siku hiyo, vitakuwa na wachezaji wenyeji (wa msimu uliopita) ambapo yanga ana advantage kubwa kwasababu wachezaji wake tegemezi wengi hawajaondoka na wana uzoefu na derby ukilinganisha na Simba sc ambayo ndo ipo kusuka kikosi kipya baada ya wachezaji wake kadhaa wa kikosi cha kwanza kuondoka.
Yanga kufungwa na Vipers siyo kipimo cha ubora wao, na simba kuifunga Saint George siyo kipimo cha ubora wao. Ubora wa timu unapimwa kwa ubora wa mchezaji mmoja mmoja, mbinu za kocha, Muunganiko wa timu, n.k, na yawezekana kufungwa kwa yanga ndo kukawafanya waje na spirit ya kushinda ili kuwapoza mashabiki wao kwa kile kilicho tokea juzi.