Kuelekea mechi ya 'TPL' Azam FC dhidi ya Yanga SC, Mchezo wa Vuta Nikuvute Kugombea Nafasi ya Pili.!

wewe timu inawaachia John boko, kapombe, manula na Nyoni hiyo akili au matope
Hawa jamaa itawachukua muda mrefu kupata timu yenye muunganiko mzuri ili wachukue ubingwa.
Ukiachana na NYONI, KAPOMBE, MANULA na BOCCO... Pia walioondoka CHECHE, MAO MKAMI, DILUNGA N.K
Imeleta CHIRWA, NGOMA, WADADA na KUTINYU,
 
Hivi Mfano Simba tungesonga nusu fainali CAF CL ligi ingemalizika ndani ya muda kweli?.. Tungekuwa na viporo hadi vimoro kabisa.
TFF + BODI YA LIGI wabovu kichwani.
 
Azam itaifunga Yanga ikiwatu haita mchezesha Abubakari Salum a.k.a Sureboy.
Huyo hadi anatoaga pasi kwa wachezaji wa Yanga.
Anaipenda Yanga kumzidi Mrisho Ngasa.
Mchezesheni mechi nyingine na sio ya Yanga.
Mkimchezesha tu mjue Yanga itakuwa na wachezaji 12 na mtabakiwa na wachezaji 10 uwanjani, 9 dimbani.
Hakika nawaambia
 
Hivi Mfano Simba tungesonga nusu fainali CAF CL ligi ingemalizika ndani ya muda kweli?.. Tungekuwa na viporo hadi vimoro kabisa.
TFF + BODI YA LIGI wabovu kichwani.
Ligi inaendeshwa kihuni
 
Hii mechi wala si ya vuta nikuvute mechi nyepesi mno kwa wana lambalamba
Azam 3 Yanga 0
 
salehjembe.blogspot.com

AZAM YAKANUSHA SURE KUPOKEA MILIONI 3 KUTOKA YANGA



2 minutes






UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, unapenda kukanusha vikali taarifa zinazoendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’, amepokea fedha kutoka kwa kiongozi mmoja wa Yanga.

Taarifa hiyo ya kutengenezwa inasambaa wakati ikiwa imebakia siku moja kabla ya Azam FC haijacheza na Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) unaotarajia kufanyika Uwanja wa Uhuru, kesho Jumatatu kuanzia saa 10.00 jioni.

Ujumbe huo unaeleza kuwa “Mchezaji wa Azam atumiwa milioni 3 na mjumbe wa Yanga.

Mchezaji wa Azam, Sure Boy, amekutwa na milioni 3 kutoka kwenye namba ya mmoja kati ya wajumbe wa kamati iliyoteuliwa ya muda ya Yanga, mjumbe huyo ambaye jina tunalo (tutalitoa mkihitaji) alituma pesa hizo juzi majira ya saa 3:52:23 kupitia kwa wakala mwenye jina la Thobias Kiwavi jijini Dar.

Ikumbukwe kuwa Yanga wana mechi na Azam siku ya Jumatatu,” ilinukuliwa kutoka chanzo cha Sports EM.

Azam FC tunaamini ya kuwa taarifa hizi ni uzushi mtupu na zinakuja ili kumwondoa mchezoni mchezaji wetu na kuwachanganya wachezaji wetu kuelekea mechi hiyo, hivyo tunawaomba mashabiki wetu mzipuuze.

“Uongozi wa Azam FC unapenda kuutahadharisha umma kuwa uzushi unaoendelea kwa mchezaji wetu, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, kuwa amepokea pesa Tsh 3,000,000 kutoka kwa mmoja wa viongozi wa Yanga unafaa kupuuzwa na kwamba una nia mbaya kwa mchezaji wetu,” uongozi wa Azam FC ukitolea ufafanuzi suala hilo.
 
Mkuu si rahisi kihivyo..Kumbuka Azam FC wana Mamluki kutoka bakuli, kwahivyo wapambane kweli
Hii mechi wala si ya vuta nikuvute mechi nyepesi mno kwa wana lambalamba
Azam 3 Yanga 0
 
Hapana, hapo lazima mmoja agaragazwe.. Ni kama kusema kuwa Man City na Liverpool kama inapigwa mechi ya kuamua ubingwa, lazima mmoja achapwe kulingana nafasi katika kugombea ubingwa
Ngoma droo leo
 
Na azam leo anamkalisha nje ndani, maana hawatapitia mlango maalumu hivyo waandae 3m ya faini NA kipigo
 
Sisi Yanga tunauliza hii nafasi ya pili inatupeleka CAF Champions 2020/2021 kwenye zile nafasi 4 tulizotafutiwa na Simba?
Timu mbili zimefanikisha hilo.
Simba = 15 pts.
Young Africans = 3 pints.
Kwa hiyo tukiingia Champions league ni halali yetu, ni matokeo yaliyochangiwa na timu yetu pia.
 
Kwani CAF wao walihitaji pointi ngapi?
Timu mbili zimefanikisha hilo.
Simba = 15 pts.
Young Africans = 3 pints.
Kwa hiyo tukiingia Champions league ni halali yetu, ni matokeo yaliyochangiwa na timu yetu pia.
 
Kwani hujui kuna kiwango cha alama zinazohitajika ili kupata fursa kwa Nchi kupata uwakilishi wa timu nne..?

Au unaelewaje hapo...na kwanini Yanga alikusanya pointi 3 lakini hazikutosha?
 
Ko mmepokeza kutoa povu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…