TandaleOne
JF-Expert Member
- Sep 4, 2010
- 1,644
- 709
Kuelekea Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaotarajia kufanyika tarehe 23th July 2016 mjini Dodoma, tayari zipo taarifa za kuaminika juu ya Viongozi wakubwa wa Vyama vya Upinzani kuazimia kujiunga na CCM katika siku hiyo.
Taarifa iliyotufikia inamtaja Mbunge mmoja maarufu wa CHADEMA ambae mpaka jana alikuwa anamaliza mazungumzo ya mwisho na viongozi waandamizi wa CCM juu ya utaratibu wa mapokezi yake na hatma yake kisiasa.
Wengine ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Pia yupo Mgombea Uenyekiti wa BAVICHA na mgombea Ubunge wa Moja ya Majimbo ya Kaskazini. Pamoja nao yupo aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, pamoja na Makatibu kadhaa wa Mikoa wa Chama cha ACT.
Ukiachilia mbali Viongozi hao wa wapinzani ambao idadi yao kwa ujumla inakaribia 18, wapo waliokuwa wa CCM na wakahama na kumfuata LOWASSA upinzani, Viongozi hao nao wameendelea kubembeleza ili waweze kupokelewa tena ndani ya CCM. Watatu kati yao tayari wako Dodoma wakiongozwa na aliyekuwa "Mtoto na Msiri" wa Lowassa ambae pia alikuwa ni KATIBU wa CCM Wilaya ya Monduli.
Wakati Viongozi hao wakijiandaa kujiunga na CCM, maandalizi ya Mkutano Mkuu yameendelea kukamilika na kufikia hatua nzuri, ambapo jana Katibu Mkuu wa CCM alikagua hatua ya maandalizi na kujiridhisha kuwa Mkutano Mkuu utakuwa wa mafanikio makubwa kutokana na kukamilika kwa maandalizi ya Mkutano huo kwa sehemu kubwa.