Tetesi: Kuelekea Mkutano Mkuu wa CCM: Mbunge, Wajumbe na Katibu wa Mikoa wa Upinzani kujiunga CCM

Tetesi: Kuelekea Mkutano Mkuu wa CCM: Mbunge, Wajumbe na Katibu wa Mikoa wa Upinzani kujiunga CCM

Kuelekea Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaotarajia kufanyika tarehe 23th July 2016 mjini Dodoma, tayari zipo taarifa za kuaminika juu ya Viongozi wakubwa wa Vyama vya Upinzani kuazimia kujiunga na CCM katika siku hiyo.

Taarifa iliyotufikia inamtaja Mbunge mmoja maarufu wa CHADEMA ambae mpaka jana alikuwa anamaliza mazungumzo ya mwisho na viongozi waandamizi wa CCM juu ya utaratibu wa mapokezi yake na hatma yake kisiasa.

Wengine ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Pia yupo Mgombea Uenyekiti wa BAVICHA na mgombea Ubunge wa Moja ya Majimbo ya Kaskazini. Pamoja nao yupo aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, pamoja na Makatibu kadhaa wa Mikoa wa Chama cha ACT.

Ukiachilia mbali Viongozi hao wa wapinzani ambao idadi yao kwa ujumla inakaribia 18, wapo waliokuwa wa CCM na wakahama na kumfuata LOWASSA upinzani, Viongozi hao nao wameendelea kubembeleza ili waweze kupokelewa tena ndani ya CCM. Watatu kati yao tayari wako Dodoma wakiongozwa na aliyekuwa "Mtoto na Msiri" wa Lowassa ambae pia alikuwa ni KATIBU wa CCM Wilaya ya Monduli.

Wakati Viongozi hao wakijiandaa kujiunga na CCM, maandalizi ya Mkutano Mkuu yameendelea kukamilika na kufikia hatua nzuri, ambapo jana Katibu Mkuu wa CCM alikagua hatua ya maandalizi na kujiridhisha kuwa Mkutano Mkuu utakuwa wa mafanikio makubwa kutokana na kukamilika kwa maandalizi ya Mkutano huo kwa sehemu kubwa.
Be careful with oppurtunists... Tabia ya nyumbu ni kufuata malisho. ccm isijali sana wingi wa wanachama ila ubora wa wanachama. Wenye kujileta kutaka kupokewa kwa mbwembwe ccm wawe wamechunguzwa wasije kuvuruga azma ya jpm kukirejesha chama kwenye mstari. Ubora wa wanachama ndio siri ya ushindi kwenye uchaguzi.
 
Kama itakua ni kweli si habari njema, huwa sivutiwi na wanaotanga tanga katika vyama, maana unaweza kumpokea Leo, ikifika 2020, akikosa nafasi ana hama tena, wajasiriamali wa kisiasa sivutiwi nao.. Bora tubaki na wanachama wachache Lakin ni wavumilivu katika shida na raha


Piga kazi Ndugu yangu
 
TandaleOne,

Ni aibu kwako na kwa Chama kwa kupiga ramli humu,Ila sishangai ndio maana Pia kuna wazee hapa Dom wanataka Upewa Ukatibu Mkuu.
 
Mboe anaogopa kumtimua Lowasa! Lowasa yupo kwaajili ya kuuwa upinzania huko ndani ya chadema anajenga makundi yenye nguvu kiasi kwamba mboe siyo lolote tena
 
1469084112319.jpg
 
Waende kwa dicteta uchwara waoga wakubwa.
Dicteta atawahonga ukurugenzi labda. Wengine watalipwa kwa ukuwadi kwa mirupo has a yule wa mjengoni aka the skimmer
 
Kwa kasi hii ya Magufuli hamna haja ya kukaa kwa vipinzani uchwara.


Upinzani Leo ndio watetezi wakubwa Wa majizi na Mafisadi ,sasa unabaki huko kutafuta nini??
hujui ukisemacho. Upinzani wa bongo ni halisi unaotoka kwenye mioyo ya wanachama wao. Uliza popote Africa mashariki juu ya cdm na cuf. Kamuulize Shein kule Zanzibar kisha muulize Lubuva juu ya nani alishinda kwani data halisi anazo japo wao walitangaza wakiwa chini ya ulinzi wa dola.
 
sina cha kuchangi hapa, ila kasi ni nzuri maana unafika haraka, ila ukigonga kidole umekwisha, unaanguka kama gunia
 
Wera weraaaaaaaaaa! Lazima UKAWA wafe kifo cha Mende
 
Mbunge akihama chama na ubunge hana.......hiyo ndiyo katiba ya Tanzania. Strict party discipline.
Akihama na jimbo hana!
 
Back
Top Bottom