Kuelekea pambano la kukata na shoka Jumamosi Februari 16, 2019 la watani wa Jadi
(Kariakoo Derby) katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Tanzania 'TPL'
Simba SC Mnyama, Wekundu wa Msimbazi dhidi ya
Yanga SC Vijana wa Jangwani, ni kama kusema tayari Yanga ameshafungwa, yaani wamekwishapoteza mchezo huo wa TPL.
Wa kimataifa Original Simba SC Taifa Kubwa
Ni kutokana na ubora wa kikosi cha Simba SC, na thamani yake pamoja na safu hatari ya ushambuliaji ikiongozwa na Streika Matata uwanjani
Meddie Kagere MK 14, akiunda Muunganiko wa
Emmanuel Okwi, John Bocco na kiungo mshambuliaji ambaye anaudambwi mwingi mpaka anakuwa Kero uwanjani
Cleoutus Chota Chama 'Triple C'
Mwana Kulitaka Mwana Kulipewa
Kocha Patrick Aussems baada ya ushindi dhidi ya Al Ahly SC katika Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) amesema umewaongezea morali Vijana wake kabla ya kuwavaa Vijana wa Yanga akiweka wazi mipango ya kumaliza kazi ya kuwasambaratisha watani hao mapema kabisa.
Simba iliitambia Al Ahly ya Misri kwa kuifunga bao 1-0 na kurudia ilichokifanya timu hiyo katika michuano ya CAFCL miaka 33 iliyopita katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kwa muktadha huo 'ikiwa mwarabu amefungwa basi Vijana wa Jangwani watatepeta kama mate ya mlevi, Simba imechapwa Klabu bora inatakuwa Vijana wa Jangwani bhana' na hasa ukizingatia Septemba 30 ilikuwa tia tia maji mwana ukome kufuata wakubwa. Ushindi ndo lengo letu la kwanza iwe Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) au Tanzania Premier League TPL..
Tukutane National Stadium kwa MCHINA kama unaweza kuzuia kipigo cha kufedhehesha.View attachment 1022213View attachment 1022214View attachment 1022215
Sent using
Jamii Forums mobile app