Tulishasema humu serikali ya Ccm itaforce kila angle ili kupata uhalali wa kutimiza agenda yao ya uchaguzi hewa kupitia ushawishi wa vyombo vya habari, watumishi wa serikali hasa walimu, dini hasa makanisa na baadhi ya wasanii.
Haya makanisa hasa makubwa yanatumika kupitisha agenda za serikali hivyo hata matamko yao na mahubiri yao tegemea kusikia maombi ya uchaguzi wa amani(which is propaganda/plan za CCM) automatic anayeombea amani hana tofauti na yule anayehalalisha upigaji kura hewa au wale wanaosema tusiharibu amani kisa kufuata maandamano ambayo ni haki kikatiba.
Hakuna amani inayotakiwa kuombwa maana watawala wenyewe wamegoma majadiriano kabla ya uchaguzi sasa kuna amani hapo au kulazimisha furaha feki?, linalotakiwa kuombwa ni Kupatikana suluhisho la haki kwa pande zote kabla ya uchaguzi pia maombi ya kuomba litokee linalopaswa kutokea ili kuileta hiyo amani ya kweli na sio amani ya kufake na kudanganya wananchi wakati huo watawala wanaendeleza mambo yao haramu.
Ukiona popote panahubiriwa amani wakati haipo badala ya kuombwa kwa suluhisho la kuleta Haki kwa pande zote, huo upande ni batili kaa nao mbali.
NARUDIA TENA, amani ya kweli italetwa kwa kutimiza mahitaji na maombi ya pande zote bila kuegemea upande mmoja, hiyo ndio amani, lkn kuegemea upande wa watawala wanaohitaji kutimiza mambo yao huku wakiharibu kwingine hiyo si amani bali UHARIBIFU AMBAO UTALIPWA TU NI SUALA LA MUDA.
SAMIA na magenge yake wameiharibu hii nchi, ipo siku hawatoamini.