Uchaguzi 2020 Kuelekea Oktoba 28: Ujio wa Dkt. Magufuli mikoa ya Kaskazini wawa gumzo!

Uchaguzi 2020 Kuelekea Oktoba 28: Ujio wa Dkt. Magufuli mikoa ya Kaskazini wawa gumzo!

Elitwege

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
5,294
Reaction score
10,970
Kuelekea tarehe ya uchaguzi mkuu hapo October 28, ratiba ya Rais Magufuli inaonyesha atamalizia kampeni zake mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga ambako taarifa hizi zimezua gumzo kubwa mtaani kila kijiwe wananchi wanajadili ujio wa Magufuli na jinsi watakavyompokea kwa kishindo.

Tangu mwaka 2015 Rais Magufuli amewafanyia makubwa watu wa Kaskazini ikiwemo kufufua reli yao, barabara za kimataifa pale Arusha pamoja na kumuibua billionea wa Tanzanite bwana Laizer.

Kwa jinsi gumzo la Magufuli lilivyo huku mtaani utafikiri CHADEMA haijawahi kuwepo kabisa kanda hii!!

Ama kweli kasi ya Magufuli itaenda na wengi, kwa heri Lema Arusha kwaheri CHADEMA kanda ya Kaskazini na karibu CCM mpya yenye kujali wanyonge.

Pole sana Mbowe baada ya kuangushwa na konyangi sasa chama chako kinaenda kuangushwa na kufutwa kabisa Kaskazini na mtumishi wa wanyonge Rais Magufuli.

IMG_20201016_125326.jpg
 
Ni kweli tunamuhitaji mgombea wa CCM aje kaskazini lakini sio kwa sababu hizo bali ni kwa sababu nyingi nyingine.

Mfano, wilaya ya Moshi vijijini ni wilaya kongwe ila haijawahi tengewa fedha za kujenga jengo la mkuu wa wilaya, polisi wilaya, hospitali ya wilaya, mahakama, hata gereza. Kwa kifupi hakuna jengo lolote la wilaya. Sasa wapo kolila sekondari.

Shule za msingi na sekondari zimechakaa haswa, tunatibiwa na makanisa kama serikali haipo.

Uteuzi unaongea wenyewe. Hatumo!

Ajira ndo usiseme.
 
Mbona Chadema kama hamtaki kusikia kabisa hili Jambo katika hii kanda mnayoita ni Ngome ya CHADEMA.

Uchaguzi huu..CHADEMA mtafail kwa kishindo.
Kama amekataliwa Chato aliko wapelekea maendeleo. Atapokelewaje Kaskazini aliko waambia wasubiri kwanza ainue mikoa mingine?
Atapokelewaje na watu alio wabagua kwenye utawala wake?
Muulize tangu awe rais amekwenda mara ngapi Arusha na Kilimanjaro??
Halafu bahati mbaya aliyo nayo ni kwamba Wachagga hawa shobokei muziki..
 
Kuelekea tarehe ya uchaguzi mkuu hapo October 28, ratiba ya Rais Magufuli inaonyesha atamalizia kampeni zake mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga ambako taarifa hizi zimezua gumzo kubwa mtaani kila kijiwe wananchi wanajadili ujio wa Magufuli na jinsi watakavyompokea kwa kishindo...
Habari ya huku ni LISSU tulishajitambua longtime...Fiesta peleka dodoma

Watu wanamachungu sana na ugumu wa maisha...huku mnajisumbuwa
 
Back
Top Bottom