BAKIIF Islamic
JF-Expert Member
- Jul 11, 2021
- 600
- 1,843
Kuchinja mnyama siku hii ya Eid ni moja ya ‘ibadah za Kiislam ambayo inatukumbusha namna ya kumpwekesha Mwenyezimungu (Subhaanahu wa Ta'alaa) na Baraka Zake kwetu, pamoja na kutupa mafunzo ya utiifu wa baba yetu Ibraahiym kwa Rabb wake na kumpwekesha Mwenyezi MUNGU. Hivyo ‘ibadah hii ya kuchinja ni muhimu sana kwa Muislamu, na inatupasa tuizingatie kwa makini na kuitekeleza.
Ni kuchinja kondoo, ngamia au ng'ombe au mbuzi siku ya 'Iydul-Adhwhaa na siku za Tashriyq (siku ya 11, 12, 13 Dhul-Hijjah) ili kujikurubisha kwa Mwenyezi MUNGU (Subhaanahu wa Ta'alaa). Kuchinja ni Sunnah Muakkadah (Sunnah iliyosisitizwa), pia kuchinja ni waajib kwa kila mwenye uwezo.
Kondoo wawe ni kondoo ambao wamekamilisha umri wa mwaka mmoja takriban. Mbuzi wawe wamekamilisha umri wa mwaka mmoja na kuingia mwaka wa pili. Ngamia wawe wamekamilisha umri wa miaka minne na kuingia wa tano. Ng'ombe wawe wamekamilisha miaka miwili na kuingia mwaka wa tatu. Mnyama ssiwe na kasoro yoyote.
Muda wa kuchinja asubuhi ya siku ya 'Iyd' ni baada ya Swalah. Hairuhusiwi kuchinja kabla ya Swalah. Inapendekeza kuigawa nyama kwanza kwa familia yako, na pia kuwagawia swadaka masikini, majirani, marafiki, n.k.
Kuchinja mwenyewe ni bora zaidi:
Inapendekezeka Muislamu achinje mwenyewe na akimuwakilisha mtu kumchinjia pia inaruhusiwa
Haifai Kumpa Chochote Katika Nyama Mchinjaji Kama Ni Ujira:
Hairuhusiwi kumlipa mchinjaji aliyewakilishwa kuchinja baadhi ya nyama kama ujira wake. Ukichinja AL-HADYI, mchinjaji hapewi katika nyama alioichinja lakini anapewa ujira wake. AL-HADYI ni kuchinja na wewe upo katika Hajj huko MAKA.
Ukichinja UDHWHIYAH, mchinjaji anaweza akapewa katika nyama hiyo aliyoichinja kama swadaka ikiwa ni masikini. UDHWHIYAH ni kichinjo kwa wale wasiokuwa katika Hajj. Walio katika Hajj kichinjo kinaitwa AL-HADYI.