Elections 2010 Kuelekea uchaguzi: Jeshi lawatisha wananchi

Elections 2010 Kuelekea uchaguzi: Jeshi lawatisha wananchi

Tamko la wanausalama linaeleweka vzr ila ni hao wanaojiita wanaharakati hawakulielewa na wameamua kulitafsiri vibaya. Hizi siyo civil societies ni vyama vya siasa. Wanajeshi wanahusika pia na usalama wa raia ndiyo maana hata wakati wa maafa wanajishughulisha na uokoaji. Kwenye tamko lao wamewaonya wanaotaka kuleta vurugu na siyo kuingilia uchaguzi. MSITUCHANGANYE!
 
Wanaharakati walichokisema ni sawa!Wewe unayeamini kuwa amani ya Tanzania bila CCM haiwezekani ndiye mwenye mawazo mgando.Amani ya Tanzania imejengwa na watanzania wenyewe tangu enzi za mababu zetu na wala si CCM.Hivi kwa nini wananchi wanapoonekana kujaribu kutaka kuitoa CCM madarakani, hapo ndiyo swala la amani linapamba moto?
Tanzania,Amani bila CCM inawezekan!:llama::llama::llama::llama:
 
Huyu MS si alisema anajitoa JF sababu ya udini, uchadema n.k bado upo tu nafikir una matatizo ya akili iyo maralia imefika hadi kwenye ubongo
 
haya. na jeshi letu ndio maana linajizatit kupambana na wakorofi yaani chadema.
thanks jeshi letu

Hujui kitu kuhusu jeshi wewe. Mtu kama Shimbo ni kibaraka tu. Na atashughulikiwa na wanajeshi wenzake huko huko kambini. Subiri uone
 
sasa hapo ndipo mnaponiacha hioi? unauhakika gani alifanya yeye? sasa kama mnapiga kelele hizo? kwanini jeshi letu liszuie machafuko?
Ongea na kamanda SHIMBO ahakikishe anarudi huyo Ghailani unayemtetea. Naamini jeshi linaweza kumrudisha wakitaka ila kwa kuwa macho ya jeshi yamehamia ndani ya tanzania na siyo nje, usisubiri wanaharakati kumpigia chapuo mtu ambaye ameamua kwa hiari yake kuviolate sheria za kimataifa
 
Kama watz tuliowengi tunataka amani ibaki, idumu na iendelee kudumu.
Mataifa mbalimbali hutafuta amani kwa njia ya gahrama kubwa.tz mungu ametupa.
kitendo cha wanaharakati kuanza kupayuka kuhusu amani yetu kinatutia mashaka
watu wenye kutunza amani ni vyombo vya usalama.
baadhi ya nchi wanaharakati huwa ndio chanzo cha migogoro na kuhatarisha amani.
baadhi ya mataifa wanaharakati wamewekewa sheria kali.
baadhi ya nchi baadhi ya taaisisi za wanaharakati zimefungwa.
nadhani sisi watz wenye amani tusifike Huko. lkn na sisi watz wanyonge tunaotaka amani tusikilizwe na wanaharakati. tunataka amani ilindwe na vyombo vyetu vya usalama.
leo hii kuna mtanzania anashatkiwa marekani. hakuna mwanaharakati aliejitokeza kuzungumza, hakuna alienyanyua mdomo. huyo ni mtanzania, amezaliwa tanzania

Haki ya kutoa maoni kama ulivyofanya ni haki ileile iliyowafanya wanaharakati walaani jeshi la ulinzi kutumiwa vibaya kisiasa kwa kuwatisha wapiga kura. Wanaharakati wanajua wenye haki ya kikatiba ya kushughulikia mambo ya uchaguzi ni tume ya uchaguzi na wadau wengine na polisi wanalinda usalama wa raia na mali zao wakati jeshi la ulinzi linalinda mipaka ya nchi ili tusishambuliwe na maadui wa nje. Dr Slaa aliwapa siku 7 kuwakamata wanasiasa wanaodaiwa kuleta umwagaji damu kama mnadhimu mkuu wa jeshi alivyodai lakini hadi leo hatujasikia kama kuna watu wamekamatwa au la. Jeshi la ulinzi si mdau wa uchaguzi bali ni chombo cha kuhakikisha nchi iko kwenye amani. Mamlaka ya kutoa tamko kama hilo yametoka wapi na ni kwa ajili ya nini? Jeshi la polisi linafanya nini? Tume ya uchaguzi inafanya nini?

Ni kama askari waone majambazi na badala ya kuwakamata waende kwenye vyombo vya habari na kutanganza: "Kuna majambazi yamepanga kufanya uhalifu na ole wao wafanye huo uhalifu." Kwako wewe ikitokea hivyo itakupa picha gani: kwamba ni kweli kuna majambazi au igizo? Kwa hiyo, kama jeshi la ulinzi wao wenyewe wameshindwa kuthibitisha kauli yao kupitia mnadhimu mkuu wa jeshi hilo ni wazi Watanzania wakereketwa na wanaoona mbali lazima wawaone wanatumika vibaya kisiasa.

Sababu ya mnadhimu mkuu wa jeshi kusema kama alivyosema bila kuonesha hayo mazingira ya hatari ni nini kwa vile ulinzi wa nchi ni wa Watanzania wote? Mbona wakati wa vita ya Kagera kila Mtanzania alihamasishwa kuwa mlinzi wa nchi dhidi ya Idd Amin na washirika wake wakionesha njia mbali mbali ambazo maadui wanaweza kushambulia na wakasema mtu yeyote akiona au akihisi kuna mtu asiyejulikana vizuri anatoka wapi au anafanya nini atoe taarifa polisi na hapakuwa na mafumbo?

Kwa vile jeshi limeona kuna mipango kama hiyo ya umwagaji damu lingeifichua ili Watanzania wawe macho na kila mbinu inayofanyika na hao wanaotaka umwagaji damu. Lakini kutoa tu kauli ya kuogofya watu na baadaye kukaa kimya ni lazima watu wenye akili wahoji. Na ndicho wanaharakati walichokifanya na siyo kwamba wao hawaoni umuhimu wa amani na utulivu. Kwa hiyo, hata wewe hukuwaelewa walichosema na pia hukuelewa mnadhimu mkuu wa jeshi alichosema na ndiyo maana unawashangaa wanaharakati wakati wao wenyewe ndiyo inabidi wakushangae wewe.
 
Tamko la wanausalama linaeleweka vzr ila ni hao wanaojiita wanaharakati hawakulielewa na wameamua kulitafsiri vibaya. Hizi siyo civil societies ni vyama vya siasa. Wanajeshi wanahusika pia na usalama wa raia ndiyo maana hata wakati wa maafa wanajishughulisha na uokoaji. Kwenye tamko lao wamewaonya wanaotaka kuleta vurugu na siyo kuingilia uchaguzi. MSITUCHANGANYE!
Wewe na Malaria Sugu ndio hamuelewi, acheni watu wenye akili timamu waendelee kutetea haki inayoporwa na CCM wakisaidiwa na vyombo vya usalama na wagonjwa kama ninyi
 
Penye dhuluma ya ufisadi hakuna amani wala utulivu hata chembe ile.

Pokea tiba hii ya Malaria Sugu upone na wewe utamtukuza Muumba wa vyote
 
nasikitika Shimbo ameamua kumhujumu JK kwa ktoa kauli zinazoashiria kufanyika kwa uchaguzi usio huru na wa haki. Sioni mantiki ya jeshi kupinga elimu ya uraia kwa wapiga kura, yeye alitaka NGO zifanyeje, alitaka tuendelee na idadi kubwa ya kura zilizoharibika? alitaka idadi ya wapiga kura iendelee kuwa asilimia 50 tu ya walijiandikishaa?
Hapo Meja jenerali Shimbo umechemsha, kwako wewe ni kwenye medani sio jukwaani, siasa umeanza lini? wenzako wameshakuweka kwenye rekodi ya kuingilia masuala ya kiraia kwa kuwa mnajimu. Usiangalie mambo katika mtazamo mmoja tu wa kuwabana wanaodai haki zao, tafuta chanzo na ujue jins ya kuepusha shari na kuvurugika kwa upendo kwenye nyoyo za watanzania. Dhulma na ukandamizaji ndio sumu ya amani
Wewe unataka kuendeleza vurugu hizo, shauri yako!
 
Kama watz tuliowengi tunataka amani ibaki, idumu na iendelee kudumu.
Mataifa mbalimbali hutafuta amani kwa njia ya gahrama kubwa.tz mungu ametupa.
kitendo cha wanaharakati kuanza kupayuka kuhusu amani yetu kinatutia mashaka
watu wenye kutunza amani ni vyombo vya usalama.
baadhi ya nchi wanaharakati huwa ndio chanzo cha migogoro na kuhatarisha amani.
baadhi ya mataifa wanaharakati wamewekewa sheria kali.
baadhi ya nchi baadhi ya taaisisi za wanaharakati zimefungwa.
nadhani sisi watz wenye amani tusifike Huko. lkn na sisi watz wanyonge tunaotaka amani tusikilizwe na wanaharakati. tunataka amani ilindwe na vyombo vyetu vya usalama.
leo hii kuna mtanzania anashatkiwa marekani. hakuna anaefuatilia na angalau tu kutoa tamko.
hawa ndio wanaharakati wetu. sitaki niamini kama wanafanya kazi kwa shindikizo

hivi kuna dawa gani nzuri sana ya malaria siku hizi? mtu mwenye malaria sugu hudhani mbu ni jitu kubwa ambalo hata hawezi kulishinda....amani haitunzwi kwa kutumia nguvu bali kwa uelewa wa jamii husika.....hauna uelewa ndo maana unataabika....tulionao hatuna shida na amani feki iliyopo hapa Tz, mtu amelima mahindi bila kusaidiwa na kidudu mtu kiwacho chote,amevuna anapangiwa jinsi ya kuyatumia eti asiuze nje ya nchi kwa kuwa wakazi wa masaki na oysterbay siku wakichoka kula baga na chips za south africa watashindwa kupata unga wa kula ugali! watu mahindi yanawaozea huko rukwa halafu wewe unaita wana amani??! amani gani bwana weye?
wenye akili na wasio na akili,wenye malaria na wasio nayo wote kwa pamoja tunawaambia .....HATUDANGANYIKI 2010......
 
Angalia hiyo highlighted!! Hivi wewe ulimsikia generali fisadi Shimbo alivyosema? Alisema kuwa yapo mashirika ya kiraia ambayo yanashughulika na siasa na kuhatarisha amani. Tumemsikia akisema hayo kwa maneno yake mwenyewe. Sasa wewe na mimi tujiulize je, tumesikia mashirika yoyote ya kiraia yakifanya kampeni? Na kama yanafanya kazi ya kukataza kufanya kampeni ni kazi ya Jeshi au ni kazi ya Tume na Msajili wa Vyama vya siasa? Ukimaliza kujibu hayo maswali mawili utaelewa kwa nini wanaharakati wametoa tamko lao.

Wanajeshi kazi yao ni kukaa kambini. Wao wanalinda mipaka ya nchi isivamiwe. Kazi ya kudeal na mashirika yasiyo ya kiserikali ni ya msajili wa NGO, Polisi na usalama wa Taifa. Wanajeshi wanahusikaje? Usije ukakuta lengo lao ni kuchochea vurugu.

Kama watz tuliowengi tunataka amani ibaki, idumu na iendelee kudumu.
Mataifa mbalimbali hutafuta amani kwa njia ya gahrama kubwa.tz mungu ametupa.
kitendo cha wanaharakati kuanza kupayuka kuhusu amani yetu kinatutia mashaka
watu wenye kutunza amani ni vyombo vya usalama.
baadhi ya nchi wanaharakati huwa ndio chanzo cha migogoro na kuhatarisha amani.
baadhi ya mataifa wanaharakati wamewekewa sheria kali.
baadhi ya nchi baadhi ya taaisisi za wanaharakati zimefungwa.
nadhani sisi watz wenye amani tusifike Huko. lkn na sisi watz wanyonge tunaotaka amani tusikilizwe na wanaharakati. tunataka amani ilindwe na vyombo vyetu vya usalama.
leo hii kuna mtanzania anashatkiwa marekani. hakuna anaefuatilia na angalau tu kutoa tamko.
hawa ndio wanaharakati wetu. sitaki niamini kama wanafanya kazi kwa shindikizo
 
Kama watz tuliowengi tunataka amani ibaki, idumu na iendelee kudumu.
Mataifa mbalimbali hutafuta amani kwa njia ya gahrama kubwa.tz mungu ametupa.
kitendo cha wanaharakati kuanza kupayuka kuhusu amani yetu kinatutia mashaka
watu wenye kutunza amani ni vyombo vya usalama.
baadhi ya nchi wanaharakati huwa ndio chanzo cha migogoro na kuhatarisha amani.
baadhi ya mataifa wanaharakati wamewekewa sheria kali.
baadhi ya nchi baadhi ya taaisisi za wanaharakati zimefungwa.
nadhani sisi watz wenye amani tusifike Huko. lkn na sisi watz wanyonge tunaotaka amani tusikilizwe na wanaharakati. tunataka amani ilindwe na vyombo vyetu vya usalama.
leo hii kuna mtanzania anashatkiwa marekani. hakuna anaefuatilia na angalau tu kutoa tamko.
hawa ndio wanaharakati wetu. sitaki niamini kama wanafanya kazi kwa shindikizo

:A S 112::horn:
 
MIMI KAMA DAKTARI NAWEZA DIAGNOS KWAMBA MALARIA SUGU NI GENIUS KIASI KWAMBA HATA YEYE MWENYEWE HUWA HAELEWI ANACHOKIONGEA.mara nyingi gift kama hizi huwezi zaliwa nazo labda kama ulidondoshwa wakati mtoto mchanga,but huwa inadevelop jinsi unavokuwa especialy kama uliingia jela ya watu wazima wakati we ni mtoto. naomba madaktari wengine wamsaidie huyu mtoto.
 
Back
Top Bottom