Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,750
Uyo kamanda afaamu tu kuwa hata ndani ya jeshi wapinzani wamo na wamejaa tele ,humo ndani si wote wanaipendelea ccm ,bali wengi wao wanafahamu kwa undani ni nani mwizi na ambae anaewasababishia wanapomalizia muda wa kulitumikia jeshi wanarudi wakiwa wamechoka na hawana hata kiinua mgongo cha kuwasaidia muda wao wa uhai uliobakia ,ni wangapi walikwenda kupigana vita ya uganda hadi hii leo hawakupata malipo ,wakidai wanaambiwa walijitolea au wakamtafute nyerere ,ni bora mtumie busara katika kuutumikia umma huu wa WaTanzania ambao wameanza kufahamu kuwa nchi yao ni TAJIRI na hawana sababu ya kulala na njaa,kukosa matibabu kukosa mlo na mambo mengi tu.