Elections 2010 Kuelekea uchaguzi: Jeshi lawatisha wananchi

Elections 2010 Kuelekea uchaguzi: Jeshi lawatisha wananchi

Unajua utawala wa JK umekuwa kama ulimwengu wa Kambale ata kakambale kadogo nako kanazaliwa kana tundevu.
Yaani hakuna discipline kabsaaaaaaaaaaaa.
Yaani mtu akishahongwa anabwabwaja tuu bila kujari anaongea nini na wapi?
Kama mna hamu ya kupigana si mwende somali au sudani.
Naona tukishazipiga Tz ndo discipline itakuwepo

Mhariri aseme yake, yule Hiza aseme na huyu naye aseme, na mwanae nae aseme, orodha ni ndefu mno.
 
Kumbe wamejua matokeo yanayoptakiwa kutangazwa? Basi hata kuapishwa aapishwe usiku kama kenya. Tunajua kuhesabu na kujumlisha yakitangazwa yaliyotokea kwa nini tuwe na wasiwasi wa kukubali? Watu hawakubali matokeo yanayotangazwa. Huwa wanakubali kutangazwa kwa kilichotokea kweli. Kila kituo kinapobandika tunaweza kujumlisha na sio kazi ngumu. Yakitangazwa hayo wala hakuna haja ya kuhimizwa kuyakubali. Mkilazimisha nani kasema mungu analazimishwa kuwekewa mtu ambaye hakumtaka? Akipita kikwete ni sawa. Akipita slaa ni sawa ila kitangazwe kilichotokea sio kitangazwe kinachotarajiwa.
 
Ninyi hamjui kwamba tunatawaliwa kijeshi.
Rais ni mwanajeshi na wanajeshi wana umoja. hawawezi kumwacha mwenzao aende na maji ndo maana wameanza mazoezi ya KUUA raia watakaopinga uchakachuliwaji wa kura
 
Badala ya kuonya kwamba kura za raia zisichezewe kwa maana ya kuibiwa wanawatishia watakaoibiwa kutii. Badala ya kuonya vikundi vya kigaidi vinavyofadhiliwa na vyama vya siasa kama green guard ya ccm vifutwe wanawatishia wanaokatwa mapanga na hawa magaidi wasijitetee. Muumba yupo upande wa mwenye kudhulumiwa haki, goliath wetu amefikia maangamizi yake, whether he likes or not!!
 
pr-logo-250x148.jpg
PEOPLE'S RESISTANCE
Let's take back our country
 
Shimbo anadai wamebaini kundi la kukataa matoke. that mean wamesha identify mshindi atatoka kundi gani na wakataa matokeo watakuwa kundi gani.

Matamshi ya jesi yanaashiria kuwa matokea yamesha pangwa na mshindi wamesha mjua.

japo si kazi ya jeshi la wananchi kuingilia mambo ya ndani lakini kutokana na mazoea na ubovu wa mfumo wa siasa,Jeshi lie chukua jukumu lisilo lake kwani this time hawatakwenda zanzibar kama walivyo zoea.
 
Anohofia kitumbua chake kuingia mchanga

Kama afande ni mkweli aende Jimbo la Busanda tumepata taarifa kupitia vyombo vya habari mtu anayesadikika mshabiki wa chadema amekatwa sikio na green guards vijana wa chama tawala sisiemu na damu ikamwagika UPO HAPO?Sasa mmejipanga vipi kuzuia damu ipi na ya nani isimwagike huo ni mfano mmoja tu. Amani idumishwe kwa kutangaza matokeo yasiyochakachulwa, ujanja ujanja usipewe nafasi MUNGU IBARIKI TZ & UCHAGUZI WETU TAREHE 31/10/2010 MWINUE MTEULE WAKO ASHINDE ATUKOMBOE WATZ MIKONONI MWA MAFISADI AMINA:rain:
 
jwtz ni vyema likajifunza yaliyotokea kenya. Uchaguzi ni suala la kisiasa na kamwe hauwezi kuwa ni ufumbuzi namnadhimu huyo mkuu kujitokeza hadharani na kuongea matope basi ajue ameonyesha upeo mdogo alionao.



utabiri wa sumaye baada ya kujeruhiwa na mbinu chafu za kikwete mwaka 2010...unakuwa kweli...alisema hivi...."....anayetumia kalamu kuingia madarakani..atatumia bunduki kusalia madarakani..."

that was the greatest qoute from sumaye.....and that is what is definately going to happen.....sasa jk anatumia kalamu na soon bunduki kuweza kusalia madarakani..."
 
Wakohofia huwa ni wanajeshi rank za chini siyo haya mafisadi. Ranki za captain na chini wanaweza kuwa upande wetu...Anyway sisi lengo ni mapinduzi ndani ya box hayo ya wizi wa NEC ni yao
 
Mwaka huu tutaskia mengi sana bado na wengine watajitokeza tu Hatishiki mtu hapa mpaka kieleweke...
 
Huyu Luteni Jenerali Abdurahmani Shimbo amekosea. Alipaswa kusema vyama vyote vilivyounda majeshi mf. Green Guard ambao wanampango madhubuti wa kuvuruga uchaguzi ikiwa ni pamoja na wizi wa kura wasijaribu kwa sababu wataona cha moto. kwanini wawalazimishe wananchi kukubali matokeo tu?? Yako mambo mengi ya kukemea.
 
Kapitwa na wakati. Huyu bado anaishi 60's & 70's.
 
Mbinu za CCM kuiba kura zimeonekana mapema kabisa,kwanza wanatumia njia za zamani sana kiasi kwamba zitafahamika kwa wana nchi.
1.wameanza kuwa aminisha watu kuwa MGOMBEA WA CCM atashinda kwa kishindo zaidi ya asilimia 80.Si kweli.
2.Wameanza kufanya maandalizi ya kuhakikisha masanduku ya kura wataifadhi katika ma hall yenye singboard,ili wapandishe watu na mabox ya kura za kupika na wakati wa usikuwapate nafasi ya kuyabadili kwa urahisi.
Njia ya kwanza hapo juu ni ya ki propaganda zaidi,Watanzania wa leo wapo makini haitafanikiwa na njia ya pili mwaka huu hamna hata kwenda kula mpaka kieleweke.
 
mbinu za ccm kuiba kura zimeonekana mapema kabisa,kwanza wanatumia njia za zamani sana kiasi kwamba zitafahamika kwa wana nchi.
1.wameanza kuwa aminisha watu kuwa mgombea wa ccm atashinda kwa kishindo zaidi ya asilimia 80.si kweli.
2.wameanza kufanya maandalizi ya kuhakikisha masanduku ya kura wataifadhi katika ma hall yenye singboard,ili wapandishe watu na mabox ya kura za kupika na wakati wa usikuwapate nafasi ya kuyabadili kwa urahisi.
Njia ya kwanza hapo juu ni ya ki propaganda zaidi,watanzania wa leo wapo makini haitafanikiwa na njia ya pili mwaka huu hamna hata kwenda kula mpaka kieleweke.

kwanza siku hiyo ya uchaguzi chadema mutanyweshwa pombe ile mbaya kisha usiku wakati wa kuhesabu kura umeme utakatika ghafla!! Sasa huku mukiwa mumelewa chakari, na taa zimezimwa mpaka usiku wa manane ndio utarudi wakati huo mumesha lala fofofo!!! Kitaeleweka nini? Na huku mumelala?
 
Umeshapangwa mkakati wa hali ya juu wa wizi wa kura. Mjiandae kununua vyakula kwa wingi maana mkong'oto unaweza kutembezwa na curfew kuwekwa watu wasitoke ndani kwa wiki kadhaa.
 
Kila tusi kubwa hapa duniani ni lako we Shimbo!!!
 
Baba yake Shimbo na Baba yake Kikwete walifanya kazi pamoja ,Kikwete na Shimbo wamekuwa pamoja kwa hiyo rafiki yakejakaya amemtuma aseme hayo,Alipomteua Mwamumunyange ilikuwa ni geresha mambo mengi alikuwa anamwagiza Shimbo nyuma ya mgongo wa Mwamunyange mpaka mwamunyange alipomkoromea ndipo akanza kumpa heshima yake .
Shimbo kuna mfano wa thailand and wafilipino wananchi walipoamua kuchukua nchi yao kutoka kwa wahafidhina na mafisadi hawakujali Jeshi ,Nchi hii siyo ya mamako Shimbo ni yetu sote tupo tayari kwa lolote nyakati za vitisho zilishapita.
Katiba inasema wanajeshi hamruhusiwi kuwa wanasiasa kwa hiyo munataka kuilekeza tume kwa mtutu wa buduki wa mtangaze kikwete kwamba ameshinda halafu museme akishatangazwa huwezi kupinga
SHIMBO damu ya mtanzania yeyote ikimwagika wewe ndio wa kwanza tutalala mbele na wewe,tuachie nchi yetu
huna busara kabisa waroho wa madaraka wakubwa
 
Huyo Shimbo ana kabinti kake kazuri kweli, zamaniii kalikua kanasoma pale Jangwani. wadau kuna mtu amekaona hivi karibuni
Kwenye institution yoyote mayb. Nataka nimpe ka msg kake.:A S wink::A S 11:
 
Yaani kuna matayarisho ya jeshi kulazimisha matokeo yakubaliwe hata kama sio ya haki? Shimbo hajui kwamba haki ya wananchi kujiamualia wenyewe nani awaongoze ni shina la UHURU wao, na kama UHURU huo unaingiliwa inabidi upiganiwe?

Kulinda amani ni kazi ya jeshi la polilisi. Na amani huhitaji haki. Bila haki, hakuna amani. Amani ya mtutu sio amani. Waliijaribu Makaburu wakashindwa. Anataka Shimbo kuijaribu Tanzania kwa niaba ya Kikwete? Does Kikwete want to continue to be President AT ANY COST?
 
[FONT=Arial, sans-serif]Hii nimeipata sasa hivi
[/FONT]
Vyombo vya ulinzi na usalama nchini Tanzania vimewataka viongozi wa vyama vya siasa nchini kukubali matokeo ya uchaguzi mkuu yatakayotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi NEC na kutothubutu kupinga matokeo hayo na kusababisha vurugu.

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Luteni Jenerali Abdurahmani Shimbo ametoa tamko hilo leo Jijini Dar-Es-Salaam kufuatia kuwepo kwa taarifa za vyama vya kisiasa kujiandaa kukataa matokeo yatakayotangazwa na tume ya uchaguzi.

Luteni Jenerali Shimbo amesema vyombo vya usalama vimejipanga kukabiliana na hali yoyote ya vurugu ambayo itajitokeza na kuwaonya watu kutoshiriki katika vurugu zozote baada ya kutangazwa matokeo.

Huyu General should watch his steps. Huku anakotaka kuingia sio kurahisi kama anavyotaka kufikiri. Mfupa uliomshinda fisi, mbwa hata uweza. Lakini as usual, we are free to chose our own peril, including Gen. Shimbo.
 
Back
Top Bottom