Unajua utawala wa JK umekuwa kama ulimwengu wa Kambale ata kakambale kadogo nako kanazaliwa kana tundevu.
Yaani hakuna discipline kabsaaaaaaaaaaaa.
Yaani mtu akishahongwa anabwabwaja tuu bila kujari anaongea nini na wapi?
Kama mna hamu ya kupigana si mwende somali au sudani.
Naona tukishazipiga Tz ndo discipline itakuwepo
Anohofia kitumbua chake kuingia mchanga
jwtz ni vyema likajifunza yaliyotokea kenya. Uchaguzi ni suala la kisiasa na kamwe hauwezi kuwa ni ufumbuzi namnadhimu huyo mkuu kujitokeza hadharani na kuongea matope basi ajue ameonyesha upeo mdogo alionao.
mbinu za ccm kuiba kura zimeonekana mapema kabisa,kwanza wanatumia njia za zamani sana kiasi kwamba zitafahamika kwa wana nchi.
1.wameanza kuwa aminisha watu kuwa mgombea wa ccm atashinda kwa kishindo zaidi ya asilimia 80.si kweli.
2.wameanza kufanya maandalizi ya kuhakikisha masanduku ya kura wataifadhi katika ma hall yenye singboard,ili wapandishe watu na mabox ya kura za kupika na wakati wa usikuwapate nafasi ya kuyabadili kwa urahisi.
Njia ya kwanza hapo juu ni ya ki propaganda zaidi,watanzania wa leo wapo makini haitafanikiwa na njia ya pili mwaka huu hamna hata kwenda kula mpaka kieleweke.
[FONT=Arial, sans-serif]Hii nimeipata sasa hivi
[/FONT]
Vyombo vya ulinzi na usalama nchini Tanzania vimewataka viongozi wa vyama vya siasa nchini kukubali matokeo ya uchaguzi mkuu yatakayotangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi NEC na kutothubutu kupinga matokeo hayo na kusababisha vurugu.
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Luteni Jenerali Abdurahmani Shimbo ametoa tamko hilo leo Jijini Dar-Es-Salaam kufuatia kuwepo kwa taarifa za vyama vya kisiasa kujiandaa kukataa matokeo yatakayotangazwa na tume ya uchaguzi.
Luteni Jenerali Shimbo amesema vyombo vya usalama vimejipanga kukabiliana na hali yoyote ya vurugu ambayo itajitokeza na kuwaonya watu kutoshiriki katika vurugu zozote baada ya kutangazwa matokeo.