Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Elections 2010 Kuelekea Uchaguzi mkuu CHADEMA Sept. 2009

Status
Not open for further replies.
Sahihisho, Kwenye kikao Ndesamburo hukuweko (yuko moshi). Bali alikuwepo Mzee Jafari Kasisiko kutoka kigoma na balozi Ngaiza kutoka kagera. Halima Mdee aliingia kama legal advisor kwa kuwa Tundu Lissu hakuweza kufika.

Zitto ameandika barua ya kujitoa kwenye kugombea uenyekiti. Kama wapambe wake wanasema anaendelea na kampeni basi anaenda kinyume na barua aliyoiandika kwa mkono wake yeye mwenyewe na kui sign.
 
Date: 8/29/2009
Zitto sasa ataka nafasi ya mwenyekiti agombee Dk Slaa

Na Fred Azzah

MOTO wa Uchaguzi wa nafasi ya uenyekiti wa Chama cha Demokarsia na Maendeleo (Chadema), bado unazidi kuwaka baada ya Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe kukataa mapendekezo ya wazee wa yeye kuwa Katibu Mkuu ili kumpisha Mbowe na badala yake kutoa masharti mapya ya kujitoa.

Habari zilizopatikana jana kutoka makao makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam zinaeleza wazee walieleza kuwa mgawanyiko uliotokana na vigogo hao wa Chadema, Zitto na Mbowe kuchukua fomu kuwania uenyekiti ni hatari kwa uhai wa chama.

Walisema ili kukinusuru chama hicho walipendekeza Katibu Mkuu wa sasa, Dk Willibrod Slaa agombee nafasi ya Makamu Mwenyekiti na Zitto awe Katibu Mkuu wa chama ili kumwachia Mbowe kusimama kugombea uenyekiti.

Kikao hicho kilianza saa 4:00 asubuhi na kumalizika kikishirikisha Mwasisi wa Chama hicho, Edwin Mtei, Mwenyekiti mstaafu, Bob Makani, Victor Kimesera, Phillemon Ndesamburo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilibrod Slaa na Mbunge wa Viti Maalumu wa chama hicho, Halima Mdee.

Ziito ndiye alianza kuingia katika kikao hicho saa 9:00 alasiri huku Mbowe akingia baadaye saa 11:00 jioni.

Pia inaelezwa kuwa moja ya ajenda kubwa ya kikao hicho ilikuwa ni kujaribu kukinusuru chama kwa kumtaka Zitto akubali kuondoa jina lake katika kinyang'anyiro hicho ili kumpisha Mbowe aweze kugombea ili kulinda hadhi ya chama.

Hata hivyo, taarifa za ndani zinaeleza kuwa Zitto alikataa pendekezo hilo na kuwaleza wazee hao kuwa yupo tayari kujitoa iwapo Mbowe na yeye atajitoa kugombea nafasi hiyo ili ichukuliwe na Dk Slaa kwa lengo la kuleta umoja ndani ya chama hicho.

Inaelezwa kwamba Zitto alipinga mapendekezo ya wazee kwa madai kuwa kama Mbowe ataendelea kugombea nafasi ya uenyekiti wakati amekuwa akimchafu kuwa ni fisadi, umoja katika chama hicho hautakuwapo.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinasema kwamba Zitto alipendekeza badala yake wote wawili—yeye na Mbowe, wajitoe katika kinyang’anyiro ili kukinusuru chama kugawanyika na nafasi hiyo ichukuliwe na Dk Slaa ambaye alikuwa katibu wa kikao hicho cha wazee.

Vyanzo vyetu vya uhakika vinasema Zitto aliwaeleza wazee hao kuwa yupo tayari kutokuwa na cheo lakini chama kibaki salama.

Hata hivyo, wazee waliamua kuwapa muda wa kujadili mapendekjezo ya wazee Dk Slaa, Mbowe na Zitto leo saa 3:00 asubuhi kabla ya kikao cha kamati kuu hakijaanza. Mkutano huo ulimazika saa 12:45 jioni.

Zitto alipotakiwa kutoa ufafanuzi wake alikataa na badala yake akataka aulizwe Slaa ambaye alikuwa katibu wa kikao hicho cha wazee.

Msimamo huo wa Zitto unatokana na kikao cha awali alichokaa na viongozi wa kambi yake kwenye Hoteli ya Tamali iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Katika mkutano huo wapambe wake walimtaka Zitto kukataa wazo la kumpisha Mbowe kwa kuwa ni haki yake ya kikatiba kugombea nafasi hiyo.

Katika kikao hicho kilichoelezwa kuwa ni cha kuweka mikakati ya kuendesha kampeni wafuasi wake hao walisisitiza kuwa hawatakubali mgombea wao ajitoe.

Mwandishi wa gazeti hili ambaye alikuwapo katika hoteli hiyo alishuhudia Zitto akiingia saa 5:00 asubuhi katika hoteli hiyo na kwenda kukaa pamoja na baadhi ya viongozi wa chama hicho.

"Mwandishi tunaomba utupishe tunataka kuzungumza mambo yetu," alimwambia mmoja wa viongozi hao wa chama hicho ambaye awali walikuwa wamekaa pamoja kabla ya Zitto kuingia hotelini hapo.

Kikao hicho kilichokuwa na watu watano, akiwamo, Afisa Uhusiano wa Chama hicho, David Kafulila na Msafiri Mtemelwa kilifanyika nje ya vyumba vya hoteli hiyo.

Hata hivyo, baada ya kikao hicho, mmoja wa watu hao walimdokeza Mwandishi wetu kuwa Zitto hatakubali wazo la kumpisha Mbowe kugombea nafasi ya mwenyekiti katika kikao cha baraza la wazee kilichokuwa kikifanyika makao makuu ya chama hicho na kwamba walikuwa wanaendelea na kampeni za mwisho kwa wajumbe wa mkutano mkuu ambao wameanza kuingia jijini Dar es Salaam.

Wakati juhudi za wazee hao zikiendelea, habari za ndani ya Chadema zinaeleza kuwa Zitto anaendelea na kampeni zake na hadi sasa anaungwa mkono na mikoa 15 na Zanzibar na kwamba ana nguvu kubwa iwapo jina lake litapitishwa kugombea nafasi hiyo. Leo Kamati Kuu ya chama hicho inakaa na kesho uchaguzi wa baraza la vijana na wazee.
 
Sasa hii ni kuonyesha UKOMAVU.

Shida sio madaraka, ila mwenyekiti ni MBOVU

BIG up Zitto!!
 
Jamani hata mie naunga mkono Chama atawale Dr Slaa. Nyie mnalionaje hili?
 
Unajua this whole thing is nonsense (so FMES would say).

Hivi tatizo ni nini haswa? Zitto kugombea si ni haki yake jamani? Mbowe kugombea si ni haki yake?Any Chadema member who meets creteria naamini anaruhusiwa kugombea. jamani let the people contest..washindanishe hoja. Atakayeweza kutoa hoja maridhawa basi wajumbe watamchagua. Hii kelele ya umoja wa chama na bla blah nyingine ndo zinadumaza siasa za dunia ya tatu... Infact kwa mtu kama Mbowe angeiona hii kama opportunity ya kuona kama anaungwa mkono au vipi. NA KWA VILE YEYE NI INCUMBENT, basi huu uchaguzi ungekuwa referendum kwa utendaji wake wa miaka mitano inayomalizika. He should be happy!

Hebu Chadema mtuondolee hii aibu. We expect more from you. Kwa nini muwe waoga na siasa za ushindani? Unless kuna kitu sikijui..lakini sioni mgawanyiko katika chama utatoka wapi kama uchaguzi ukifanyika kwa uhuru na haki. Kwani si ni hawa hawa viongozi wanaotwambia demokrasia kuna kushinda na kushindwa?

Hapana naona hapa hizi siasa za namna hii ndo zinatufanya wengine tuwaone wapinzani kama CCM ya akina Chiligati tuu..lead by example. Anayetaka kugombea agombee. WAJUMBE WATAAMUA. Na wale ambao kura hazitatosha..basi wavunje kambi wamsaidie mwenyekiti kukijenga chama kwa ajili ya 2010.


Hivi jamani hawa jamaa hawana strategists? Honestly ukiona mtu ana aspire kuongoza watu million 40..na bado anashindwa kufanya maamuzi madogo kama haya...sasa hiyo nec ya Chadema inayoshauri watu waachiane nafasi..itakuwa tofauti gani na nec ya Makamba?

Kila la kheri wagombeaji wote.

Masanja,
 
eti kuhatarisha umoja wa chama no!bali ni kuhatarisha maslahi ya kina mbowe,mtei,suzan lyimo,kiweru na wengine wengi list ni ndefu
 
...sasa hiyo nec ya Chadema inayoshauri watu waachiane nafasi..itakuwa tofauti gani na nec ya Makamba?

Masanja,

NEC ya Chadema inakutana kesho jumapili. Kikao cha leo kilikuwa cha wazee wa chama cha kuchambua majina ya wagombea ambayo yatawasilishwa kwenye kikao cha kesho. Wazee walimweleza Zito athari ya kuwa na makundi kwenye chama na kwamba hakiwezi kwenda kwenye uchaguzi mwakani kikiwa kimegawanyika. Habari zilizokuwa zinaandikwa kwenye magazeti zimewaogopesha hawa wazee na waliona wasingeweza kupatanisha hizi kambi mbili baada ya uchaguzi. Zitto baada ya kuyasikia hayo akakubali huo ushauri akajitoa.

Hoja ya Zitto kwamba Dk Slaa awe mgombea uenyekiti na yeye (Zitto) na mbowe wajitoe wala haikujadiliwa. Labda ilikuwa ni strategy ya kambi ya Zitto lakini hakuiwasilisha.
 
Wana JF si kawaida yangu kuandika sanasana na imenilazimu leo... Tangu zamani niliamini kuwa CHADEMA kinaweza kuwa chama cha 'Demokrasia' na daima kitaruhusu 'Demokrasia' kuchukua mkondo wake lakini tunapoelekea inaelekea sivyo.

Naam, nazungumzia kikao kilichofanyika leo na 'wazee' wa CHADEMA kuanza 'kumshinikiza' Zitto Kabwe kuondoa jina katika kinyang'anyiro cha Uenyekiti.

Ndiyo, nilikuwa sioni sababu ya Zitto kugombea mwanzoni lakini kwakuwa alishaweka jina nilitarajia atapewa nafasi kuweza kudhihirisha kuwa demokrasia imeweza kuchukua mkondo wake ndani ya CHADEMA.

Nasisitiza, napinga kwa sana njia hii inayotumika kuhakikisha Freeman anabaki mgombea pekee, inawezekana kwa maslahi ya chama chenu mmefanya hivyo kukinusuru chama (kama mnavyodhania) lakini binafsi (si msimamo wa JF) naamini ndio mnakizika chama... Bado mna muda, mwacheni Zitto agombee na akishindwa ashindwe kidemokrasia...

Kama ni kuondoa basi wote wawili (Zitto na Freeman) waondoe majina na ifikiriwe namna mpya.

Katika hili, mmechemsha!

UPDATE: 1

Baada ya kuwasikiliza kwa makini mzee Mtei, Dr. Slaa na Zitto mwenyewe, nimegundua kuwa Zitto anakiri HAJALAZIMISHWA na amefanya hivyo kwa dhamira yake mwenyewe... Taarifa za vyombo vya habari zitafuatia kuhusiana na mkutano wa viongozi wa juu wa CHADEMA na waandishi wa habari uliofanyika leo (Jumapili Agosti 31, 2009).
 
Sasa nimetambua, uchaguzi ni tishio kwa kila kiongozi.
 
Sad indeed, CHADEMA wametuangusha sana, ktk hali kama hii ni vema Mbowe akaondoa jina lake, hapo nitaweza kurudisha imani yangu kwa CHADEMA. Woga wa kupambana kidemokrasia ni woga unaojenga udikteta. Bado tupo mbali kuliko tunavyofikiria.
 
Sad indeed, CHADEMA wametuangusha sana, ktk hali kama hii ni vema Mbowe akaondoa jina lake, hapo nitaweza kurudisha imani yangu kwa CHADEMA. Woga wa kupambana kidemokrasia ni woga unaojenga udikteta. Bado tupo mbali kuliko tunavyofikiria.
Kuna vijana kadhaa ndani ya CHADEMA walikuwa wamekomalia kuhakikisha Zitto haendi mbele, imenisikitisha sana. Na tuna nakala ya kila kilichoongeleka katika kikao cha jioni ya leo, baada ya kusikiliza mara kadhaa nimejikuta nakosa imani KABISA! Lakini, muda bado unaruhusu.... Mruhusuni Zitto agombee nafasi ya uenyekiti, acha unyanyasaji kwa kisingizio cha ujana!

Yawezekana kugombea kwake kama angeshindwa kungesababisha 'Anguko lake' ambalo nadhani si 'Anguko la CHADEMA' kama ilivyokwishatabiriwa... Niwahakikishie kuwa kwa kumlazimisha aondoe jina ni kupelekea Anguko la CHADEMA.

Napata wasiwasi ndiyo sababu iliyomfanya Kubenea kuamua kuingia ulingoni kwa kupitia CCM, hajaona 'difference'.
 
Taarifa nilizonazo mimi ni kwamba, Zitto aliwasilisha barua ya kujitoa hata kabla mahojiano hayajamalizika. Alichofanya baada ya kufanya hivyo alipendekeza na Mbowe naye ajitoe ili kuleta mshikamano ndani ya chama chao. Hata hivyo wazo hili halijakubalika.
 
Kuna vijana kadhaa ndani ya CHADEMA walikuwa wamekomalia kuhakikisha Zitto haendi mbele, imenisikitisha sana. Na tuna nakala ya kila kilichoongeleka katika kikao cha jioni ya leo, baada ya kusikiliza mara kadhaa nimejikuta nakosa imani KABISA! Lakini, muda bado unaruhusu.... Mruhusuni Zitto agombee nafasi ya uenyekiti, acha unyanyasaji kwa kisingizio cha ujana!

Mzee unaonaje uki-release hiyo nakala hapa JF ili tujadili vema?Itakuwa poa sana.
 
Hii ni Ticket ya Zitto kukamilisha form za usajili za No.1, huyu bwana wanamtaka sana watu wa nambari one.
 
chadema watafanya kosa kubwa sana kama utamzuia zitto asigombee na hii swala ndio tumeona huleta mipasuko mikubwa sana kwenye vyama vya upinzani.
 
Taarifa nilizonazo mimi ni kwamba, Zitto aliwasilisha barua ya kujitoa hata kabla mahojiano hayajamalizika. Alichofanya baada ya kufanya hivyo alipendekeza na Mbowe naye ajitoe ili kuleta mshikamano ndani ya chama chao. Hata hivyo wazo hili halijakubalika.
Kibanda, unaweza kutuwekea barua yake ya kujiondoa hapa? Nakala yake nimeambiwa nitatumiwa lakini kesho, kama unayo inaweza kuwa vema ukatushirikisha hapa. Elewa kuwa, hii inaweza kupelekea watanzania wengi kukosa imani kabisa na upinzani! Inaumiza kichwa SANA
 
Hii ni Ticket ya Zitto kukamilisha form za usajili za No.1, huyu bwana wanamtaka sana watu wa nambari one.
Wanajiita nambari one kwa kwa uchafu wao... kama Zitto ana mpango wa kujaza form zao ajaze lakini huko kwenyewe pameoza.....

Mimi nashauri atatue matatizo yaliyoko kwenye chama chake kuliko kuyakimbia..
 
Nimepata kuongea direct ni kwamba kesho saa tatu ndiyo itajulikana .Nadhani hali sasa si hali kabisa .Chadema naamini katika viongozi wote 2 na nadhani sasa tulipo fika is a point of no return.Nasema ikishindikana basi iwe Slaa achukue Chama na Mbowe na Zitto waondoe majina yao .Au la basi waachiwe Mbowe na Zitto waingie huko jamani Chadema maana yake nini ?
 
Nimepata kuongea direct ni kwamba kesho saa tatu ndiyo itajulikana .Nadhani hali sasa si hali kabisa .Chadema naamini katika viongozi wote 2 na nadhani sasa tulipo fika is a point of no return.Nasema ikishindikana basi iwe Slaa achukue Chama na Mbowe na Zitto waondoe majina yao .Au la basi waachiwe Mbowe na Zitto waingie huko jamani Chadema maana yake nini ?
Lunyungu, ndo maana nimesisitiza kuwa "Bado wana muda". Kufikia kesho wawe wamefanya maamuzi ambayo yatabadili hali hii... Nimemwona Kitila mitaa hii, naona amekosa usemi kabisa!

Hii inaweza kupelekea wazalendo kadhaa kuanzisha chama kipya cha siasa... Kama hawaamini wafanye kosa kipindi hiki waone.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom