Sio kweli mkuu tatizo jamaa alilinda masrahi ya DOWANS maana Zito sasa hivi dhambi hii ndio inayo mtafuna kwa taarifa yako asingejihusisha na hili alikuwa na kila sababu ya kuwa Mwenyekiti.
No kwa upande wangu mim nadhani jamaa bado hajakomaa vya kutosha kuongoza taasisi anakurupuka kwenye baadhi ya maamuzi.
Hapa hakieleweki kitu baba, Lugha ni moja tu: Uongozi ubaki moshi, nukta. Chimungunyi wala chitemi.Demokrasia si photocopy wadau, kumbukeni katika nchi maskini kama tanzania mchakato wa demokrasia ya kweli unajumlisha vitu vingi, hatuwezi tu kuamua mambo eti kwa vile demokrasia inaruhusu mtu yeyote mwenye sifa husika agombee nafasi husika...tanzania haijafikia demokrasia ya kiwango hicho, ndio maana kwa maendeleo ya kweli na dhati anahitajika dikteta ama kikundi cha watu wenye dira sahihi...ili kukuza demokrasia, kwa hatua tuliyopo, alichofanya zitto ni sahihi kabisa, kaonyesha anaweza, lakini pia kaonyesha ana usikivu na busara....kwa kifupi, kajiwekea imani kubwa sana ya baadae....chadema inatakiwa ikuze demokrasia nchini, hivyo inahitaji utulivu wa kweli, mbowe na zitto nadhani wamelielewa hilo...chadema msituangushe baada ya hili tukio, tunawategemea kwa sababu tu mnazo busara na mnajua kusoma nyakati....
Sio kweli mkuu tatizo jamaa alilinda masrahi ya DOWANS maana Zito sasa hivi dhambi hii ndio inayo mtafuna kwa taarifa yako asingejihusisha na hili alikuwa na kila sababu ya kuwa Mwenyekiti.
Nyie wachagga kama wakikuyu tu mumelawiti demokrasia changa
Wapiga kura wataliona hilo, kwani hawamjui Zitto. DJ ndio kakomaa. Alikabidhiwa chama hakuwa na uzoefu na CV kama ya Zitto leo hii. Tusidanganyane. Moshi, kituo, hakuna mjadala.Mimi sidhani kama alichosema ZITTO kuhusu Dowans ndicho kinamponza. No kwa upande wangu mim nadhani jamaa bado hajakomaa vya kutosha kuongoza taasisi anakurupuka kwenye baadhi ya maamuzi. Anaitaji busara zaidi thats why nikasema kuwa wamuandae ka baadaye. Chadema sasa hivi iko kwenye matatizo je ataweza? au ndiyo wataogeza mengine?
Acheni uzushi wenu huo maana kila wakati chadema sio chama cha kikabila. Wanafanya kazi nzuri sana
FL,nina mpango wa kumshawishi kaka yangu Sikonge ili atuongoze,maana haya ya Kaskazini mwa TZ yanatuchosha sasa.Huyo Magufuli mwache abaki huko huko alikozoea! WE NEED CHANGE na itoke kwa watu tofoauti na hawa waliopo sasa (Magufuli et al).Nyamizi labda Magufuli wao lazima chama lishinde na tushike dola.SHY,MZA na TBR bado watani zetu hawaaingia ndani lazima ushindi
kwani wapare wanatokea moshi????Lidhwani, JK na Salma wote wako ndani ya CCM na wote viongozi .
Mleta habari umesema Ndesa alipata kura 49 na hakuwa na mpinzani , sasa kama hakutokea mtu kupingana naye je ? Ukiona mzee anapita means anakubalika ambao ndiyo ukweli .Kwamba wapare hawakusimama sasa hii ni shida kubwa ya ukabila naona unakubana sana kaka .Sisi twende tukalazimishe makabila kuingia Siasa nakuoma kugombea ?
Wapiga kura wataliona hilo, kwani hawamjui Zitto. DJ ndio kakomaa. Alikabidhiwa chama hakuwa na uzoefu na CV kama ya Zitto leo hii. Tusidanganyane. Moshi, kituo, hakuna mjadala.
Tusidanganyane Hii ni NGO ya wenyewe. Zitto ameshawaonya kuwa ili kukinusuru chama au kukiunganisha chama basi lazima Mbowe ajiengue.
Na lugha yake mbona nyepesi sana: tujiengue sote wawili, sasa anachoshindwa Mbowe ni nini?
Halafu angalia, Mwanakijiji naye kaingia mtini, atacoment nini na mambo yameshaeleweka?
kwa hiyo mkuu ulitaka msukuma akagombee moshi halafu kwao amwachie nani?????
Lucy Owenya.
Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo na mtoto wake, Lucy Owenya, wamechaguliwa bila kupingwa kukiongoza chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Kilimanjaro kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Ndesamburo alichaguliwa tena kukiongoza chama hicho mkoani hapa baada ya kuibuka na ushindi wa kura 49 kati ya 50 za wajumbe wa mkutano huo wakati mtoto wake, Lucy, aliibuka na ushindi wa idadi ya kura kama hizo katika uchaguzi mkuu uliofanyika jana mjini hapa.
Katika uchaguzi huo, Basil Lema, alichaguliwa kuwa Katibu wa chama hicho huku Deogratius Munishi, akichaguliwa kuongoza Baraza la Vijana wa chama hicho na Seranus Mushi alichaguliwa kuongoza Baraza la Wazee wa chama hicho.
Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Ndesamburo alisema ushindi wake ni ishara kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwamba bado anakubalika na kamwe hata katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu hapo mwakani, atajitahidi kutetea kwa udi na uvumba kiti chake cha ubunge.
Alisema anashangazwa na propaganda za viongozi wa CCM ambao wamekuwa wakidai kuwa yeye ni mzee na hivyo hatagombea tena kiti cha ubunge Jimbo la Moshi Mjini jambo ambalo si la kweli.
"Eti wanasema mimi ni mzee, kibabu nimechoka sitagombea tena ubunge...Huo ni uzushi wao na ushindi wangu wa leo ni indiketa ya kwamba uchaguzi mkuu ujao nitatetea jimbo langu na kumbwaga mgombea wa CCM, alisisitiza Ndesamburo.
Naye Lucy Owenya ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) akizungumza na waandishi wa habari baada ya ushindi huo, alitoa wito kwa wanawake mkoani Kilimanjaro kujitokeza kwa wingi na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Owenya alisema wanawake hawana budi kuacha woga wa kuwania nafasi za uongozi kuanzia serikali za mitaa, madiwani na hata ubunge ili kuweza kufikisha uwakilishi wa asilimia asilimia 50 bungeni na halmashauri.
CHANZO:
Ndesamburo na Mtoto wake hawakuwa na wapinzani kama itakavyokuwa kwa Mbowe hatakuwa na Mpinzani.
kingine wagombea wote ni wachagga kwani Kilimanjaro si kuna wapare pia?